Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Elimu Elimu kwa Watoto (CHESO)Bw. Richard Shilimba (katikati) akizungumza jana jijini Dar es salaam na waandishi wa habari wakati akitoa wito kwa Serikali za Mataifa mbalimbali Duniani kuchangia mfuko utakaosaidia kukabiliana na magonjwa ya Kifua Kikuu , Malaria na UKIMWI. Wengine ni Mratibu wa Miradi kutoka Chama hicho Bibi Cartas Augustino(kushoto) , Mtalaam wa Elimu kutoka CHESO Devotha Lukuba (kulia).Picha na Tiganya Vincent-MAELEZo-Dar es salaam

Zahra Majid,Dar es Salaam

Serikali zote duniani na wadau wengine zimetakiwa kuweka fedha zisizopungua dola za kimarekani bilioni 20 katika mfuko wa fedha wa dunia kwa ajili ya kupambana na UKIMWI,Kifua Kikuu na Malaria.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Watoto (CHESO) leo jijini Dar es Salaam Bwana Richard Shilamba wakati akitoa taarifa kwa wanahabari na kuongezea kuwa mkutano huo utafanyika tarehe 4-5/10/2010 nchini Marekani

Bwana Shilamba alisema katika mkutano huo unalengo la kuchangia na kutoa ahadi kwa hiari katika Mfuko wa fedha unaojulikana kama Global Fund unajishughulisha na mapambano dhidi ya magonjwa ya Ukimwi,Kifua Kikuu na Malaria ambayo yanasumbua jamii.

Alisema magonjwa hayo ndiyo chanzo kikubwa cha watoto waishio katika mazingira magumu na fedha hizo zinatakiwa kusaidia katika kipindi cha miaka 2011 mpaka 2013.

“Kwa taarifa za Mfuko huo ambao ulianzishwa mwaka 2001, umekwishatoa fedha jumla ya dola za kimarekani bilioni 19.3 katika miradi mbalimbali ya kudhibiti UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria katika nchi 144 ambapo Tanzania ni moja ya wanufaika hao” alisema Shilamba.

Alitaja mafanikio ya mfuko huo kwa Tanzania kuwa fedha hizo zimeokoa maisha ya watu zaidi ya milioni 4.9 na zinaokoa vifo vya watu 3600 kila siku,ikiwa ni pamoja na kutoa matibabu juu ya VVU na UKIMWI kwa watu milioni 2.5.

Alisema fedha hizo pia zimetibu watu milioni 6 waliokuwa wakisumbuliwa na Kifua Kikuu na zimesambaza vyandarua milioni 104 vyenye dawa ya kudhibiti Malaria.

Kutokana na mafanikio hayo, CHESO kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na ARASA,Tanzania Networking of Women Living with HIV and AIDS (TNW+) na ARV Mategemeo Group,wanatoa wito kwa serikali zote duniani na wadau wengine kuweka kiasi cha fedha kisichopungua dola za kimarekani bilioni 20.

Bwana Shilamba alisema mfuko wa Global Fund unazihitaji feha hizo kwani zitasaidia kufanikisha Ajenda 10 za watoto zilizopitishwa na wadau wa haki za watoto nchini baada ya kuwasiliana na watoto wenyewe kote nchini na pia kwa kuwasiliana na serikali ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...