Asalaam Aleykum, Wasomaji wote wa globo hii

Baada ya Salaam, sisi ndugu zenu wa Leeds tunawapa mkono wa EID na kuwaombea afya njema furaha na amani katika kusherehekea sikukuu hii ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani, Sisi wakazi wa Leeds tumesherehekea kwa kuswali swala maalum ya EID iliyofanyika saa mbili asubuhi, Lincoln Green Mosque LS 9 LEEDS na kisha kupata futari ya pamoja katika ukumbi wa MABGATE.
Tunamuomba Allah, atupokelee funga zetu, awajaalie kila lenye heri duniani na kesho akhera

Wabilah Taufiq
Asalaam Aleykum
Mwenyekiti Amran Rashid na Sheirk Mahir Muandazi

BOFYA HAPA
kwa picha zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. sisi watu wa leeds tunajipendekeza kwa michuzi, mtu mwenyewe akija UK anaishia READING, kwenye uswahili mtupu UK gani ina mpaka tawi la chama cha CCM, utajifunza nini kutoka kwa hawa waingereza, unatakiwa utoke kabisa huko london ndio utajifunza mambo ya huku , huko reading ni kama uko bongo tu no meaning ya kuja Uingerza, next time njoo miji ya north kama leeds, scarborough, whitby na uende huko edinburgh, glasgow. Hapo kweli utakuwa umetoka uingereza. miji kama milton keynes, birmingham imefurikwa na wabongo tofauti na miji ya juu. karibu

    Mdau
    Headingley, Leeds,
    LS4

    ReplyDelete
  2. mdau umempa neno michu, london na miji ya karibu imevamiwa na wabongo, ndiyo maana london ni very multicultural huwezi kujifunza cultures za wazungu wanigeria, wajamaica hawa wamatumbi ndio mwake mwake , toka huko njoo huku bradford-leeds, newcastle, liverpool, utabadilisha mawazo, nilienda reading mara moja nilishangaa hivi huu mji uko UK ama. achaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  3. HAWA WA LEEDS INGEKUA KUTOKANA KUNARUHUSIWA NINGEWATOKANA HAWANA MPANGO WOWOTE CHUO KUSOMESHA WATOTO WANAJIFANYA KAMA ELIMU WANAYO WAO TU,MIKUTANO KILA SIKU JAMANI HAPA ULAYA LEO UMEITWA KAZINI KESHO HUJAITWA UJUE PROGRAMME ZA WATOTO ZINABADILIKA KUTOKANA NA MAISHA YA KAZI NA SIKAMA QUR-AN WATU HAWAIJUI - MTOTO ASIPOENDA SIKU MOJA CHUONI FINE POUND 20-PUMBAVU HIYO ELIMU NI BURE ITOLEWE AYA INASEMA"WALE WANAOFINYA KATIKA TULIYOYATEREMSHA KATIKA KITABU CHENYE UBAINIFU NA WAKAUZA THAMANI NDONGO NDOGO,HAWANA WANACHOKULA ILA MOTO KATIKA MATUMBO YAO"THAMANI NDOGO NDIO HIVO VIPAUNDI NA THAMANI KUBWA NI KUPATA PEPO MMEPEWA BURE TOENI BURE.

    ReplyDelete
  4. A/a Mtoa maoni kuhusu Leeds Madrasa nakuomba usiendelee nenda shule kwanza
    kabla hujaaza kutoa maoni Inaonekana huna darasa ama darasa Dogo kwa sababu
    1). Tathmini ya maoni yako inaonekana una upeo Mdogo
    wakielimu hata Kama unaishi UK ( aibu kwakweli
    You need go back to school elimu bure uk kwa watu
    Nyie)

    2. Wewe umesema Kama matusi yanaruhusiwa basi
    ungelitukana tayari umeiti watu wapumbavu tusi hili
    sheikh ( nenda shule maalim wangu)

    3 Aya uliotumia haiwahusu walimu wa Madrasa sio Leeds
    tu Bali Walimu Dunia nzima, aya hii ni kwa ajili ya
    washirikna ( eg. Wafanyaji herinzi nk)
    4. Ada yotote inayotolewa ikiwa ni £20, 40 ,50, niajili ya shughuli za chuo na ndoi maana ukaambiwa uhudhurie mkutano sheik ili ufahamu matumizi ya pesa za chuo.

    Lamwisho ujuwe kuwa unajukumu la kumpatia mtoto wako elimu kwa gharama yeyeto ( hata Kama mtoto Wa kulea au Wakambo ) Vilevile chuo kutoa elimu yawatu wazima unakaribshwa!! Watu Kama wewe mpo wengi lakini kumbuka we are very strong then you think we are!!!

    A/a

    ReplyDelete
  5. Hukmu ya Qur an BI USULIL JAMIA wala si Kwa ajili ya watu flani ikiwemo wewe na mimi na mwengine,Qur an haijaacha kuzungumzia washirikina kwa majina na ikija aya Inna ladhina basi utakua innal ladhina haduu INA MAANA imezungumzia mayahudi tu,lakini ikija Inna ladhina Yaktumuna HAKIKA YA WALE WANAOFICHA ndio nyinyi pia mnaingia hamtoi hadi mpewe chapaa,Ndio Qur-an imesema "Innal insana-layatuqha an raa-hu staghna"Hakika mwanadamu anajeuri,akijiona ana kipato.

    Ndio tunarudi tena Kipato kilichozungumziwa hapo si mali tu bali pia ni Elimu na kila mwenye kujiona sio watu flani.Njoo na wewe tukusomeshe usiropoke tu.

    Mdau amezungumzia kuhusu watoto kukosa chuoni kwa dharura kuwapiga fine na sio ADA tena ripoti mnapewa simu zenu zinaingia voice mail hayo malalamiko yapo kila sehemu na mnamtolesha fine kwa kuwa amemis au mzee hajahudhuria vikao vyenu mwezi mara 20- Bila hata ya kutoa taarifa nini kitazungumziwa that is bad management.

    Bora upeleke watoto kwenye PAY AS YOU GO wafereji kibao na elimu inapatikana,"Hamtofikia wema hadi mtoe vile mnavovipenda" na mpendelee ndugu yako kile unachokipendelea,sio umbanie.Someni uzuri au rudini na nyie mkasomeshwe.

    ReplyDelete
  6. Thats true Leeds chuoni mmezidi hata kama mna elimu ya kusomesha Alif-muwe na hekima kidogo,Go b2s or B2College,hiyo ni kazi yenu you need to introduce Work pattern which is flexibility in doing your job,

    mfikirie na mteja wako kama wewe una nafasi watu wengine hawana nafasi,hata mtu akileta excuse mara 100 ndio maisha ya ulaya jamani.Mungu akupeni hekima kama Alivompa Mtume S.A.W alipomwambia"Fabima rahmatun mina Allah lintalahu..."Kutokana na neema za MMungu umekua laini,lakini ingekua mkali mwenye moyo mmugu basi wangelikukimbia..... Mungu awape elimu zaidi na Hekima ya kuweza kupambanua.

    AMEEN,nikiwa na mtoto nitamleta Chuoni kwenu mkipata hekima lakini inshallah.

    ReplyDelete
  7. Hivi jamani waislamu mnalipa kusomeshana?

    Mathayo 10.8 inasema "Freely ye have received,freely give" Basi kama ada imepanda waleteni kwa wachungaji huku.
    Mdau (Napoli)

    ReplyDelete
  8. Baada audhubillahi minashaytani rajim,Hiki kitu kweli kinauma" Tilka ddaru l-akhirat naj-alha lilladhina la yuriduna uluwan fil ardhi wala fasada" Huo ni mji wa akhera(Pepo) tumeijaalia kwa wasiopenda ukubwa kwenye ardhi wala ufisadi" Basi Msiwe na viburi msikilize matatizo lakini na muweze kutoa mawazo kwa wazee nini cha kufanya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...