MWANDISHI WETU
Dar es Salaam
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Mark Mwandosya, amesema kuwa bado serikali inakabiliana na changamoto kubwa ya kuhakikisha kuwa Watanzania wengi zaidi wanapata huduma ya maji safi na salama.
Akifungua mkutano wa kimataifa wa siku tatu wa taasisi ya African Civil Society Network on Water and Sanitation (ANEW) jijini Dar es Salaam jana, Prof. Mwandosya alisema kuwa upatikanaji wa maji bado ni tatizo kwenye baadhi ya maeneo nchini Tanzania licha ya jitihada zinazoendelea kufanywa na serikali kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema kuwa hivi sasa maeneo ya mijini Tanzania yanapata huduma ya maji kwa asilimia 84.
Dar es Salaam inapata maji kwa asilimia 68 wakati maeneo ya vijijini yanapata huduma hiyo muhimu kwa wastani wa asilimia 58.7, alisema.
Malengo yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa kupitia malengo ya Millenia ni kuhakikisha kuwa idadi ya watu duniani wanaokosa maji safi na salama inapungua kwa zaidi ya nusu ifikapo mwaka 2015.
Malengo yaliyowekwa na Umoja wa Kimataifa ni kuhakikisha kuwa asilimia 65 ya watu wa vijijini wanapata huduma ya maji safi wakati kwa mijini lengo ni kufikia asilimia 90.
Umoja wa Mataifa umetamka hivi karibuni kuwa upatikanaji wa maji safi na salama sasa ni jambo la haki za binadamu.
“Tunatambua kuwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji imekuwa ni changamoto kubwa kwa nchi nyingi za Afrika,” alisema Prof. Mwandosya.
“Tunafahamu kuwa serikali zinahitaji ushiriki wa asasi zisizo za kiserikali, sekta binafsi na washika dau wengine ili kukabiliana na mahitaji yanayokuwa ya maji.”
Amesema kuwa tatizo la maji sasa linatishia ustawi wa kimataifa na uchumi wa dunia, huku nchi za Afika zikiwa hatarini zaidi.
Mwandosya aliongeza kuwa vyanzo vingi vya maji barani Afrika vinatumiwa kwa pamoja na nchi mbalimbali, hivyo kuwepo kwa uwezekano wa kutokea kwa migogoro ya kimataifa kuhusu vyanzo vya maji.
“Kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Kimataifa la Afya (WHO), idadi ya vifo 32,700 hutokea Tanzania kila mwaka kutokana na tatizo la maji na usafi. Hivyo basi, serikali iliandaa sera mpya ya maji mwaka 2002 yenye lengo la kuhakikisha kuwa watu wote nchini wanapata huduma ya maji kwa umbali usiozidi mita 400 kutoka wanapoishi,” alisema.
Naye Katibu Mtendaji wa ANEW yenye makao yake makuu nchini Kenya, Jamillah Mwanjisi, alisema kuwa mkutano huo wa kimataifa unaofanyika Dar es Salaam utatoa fursa kwa asasi za Afrika zinazofanya kazi kwenye sekta ya maji kuweza kubadilishana uzoefu.
“Mheshimiwa waziri, asazi zisizo za kiserikali ziko tayari kufanya kazi na wewe na mawaziri wengine wa maji wan chi za Afrika ili kukabiliana na changamoto tunazokabiliana nazo leo na kuchukua hatua za pamoja za siku zijazo,” alisema.
Mwakilishi wa Mtandao wa Tanzania wa Maji na Usafi (TAWASANET), Nyanzobe Malimi, alisema kuwa shirika lake limeweza kutoa mchango mkubwa kwenye sekta ya maji tangu lianzishwe mwaka 2008.
Hata hivyo, amesema kuwa ufinyu wa bajeti umekuwa unaifanya TAWASANET ishindwe kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.

fungua macho na vaa miwani prof na tizama ramani ya dunia, tanzania ndo nchi ya kwanza duniani yenye vyanzo vya maji vingi kuliko nchi yoyote ile duniani.
ReplyDeletetuna ziwa victoria, tanganyika, nyansa,manyara ni miongoni mwa maziwa makubwa duniani.
na tuna mito mingi, maji ya kuchimba ,mvua za masika tele na bahari ya hindi bwerele
ziwa moja tu la victoria linatosheleza kwa matumizi ya maji kwa tanzania nzima
waarabu hawana maziwa israel wana kijibwawa na kimto jordan ambacho ni hafifu lakini wanajitosheleza kwa maji.
egypt/misri wana kimfereji kinachoitwa river nile kinachotokea kwennye ziwa letu victoria wao wana kitumia kwa kilimo na kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.wananchi wao hawana shida ya maji kama sisi. tunalalamika nini wakati tunavyanzo kuliko nchi yoyote ile duniani???
acha porojo profesor maji marefu.
tunataka kusikia unaplani kubwa ya kutumia mito na maziwa tulionao ya kuwa sambazia watanzania wote maji majumbani mwao.
sikutegemea prof mzima kama huyu kutuleteahabari za majonzi
njoo na mikakati ya kulinda hivyo vyanzo na nchi ambayo haijapakana na maziwa hatuna haja ya kugawana nao maji ila kuwauzia tu.
mbona waarabu wamejaaliwa mafuta kwani tunagawana nao wanatuuzia,.
mto nile ukikauka itabidi tuwauzie egpty na sio kuleta undugu wa kusema inabidi kugawana nao maji na kama ni vita/migogoro jiandaeni, tunajeshi kubwa tu lililojikaalia mpaka askari wanvitambi.
mi namashaka na huyo prof bilashaka ni wa kudesa na nyenzo.
je tungekuwa tunaishi jangwani prof angelalama vipi????
Bongo tambarare watu 37,00 kila mwaka?
ReplyDeleteGo and vote people vote vote vote
Don't be just a spectate be a part of it ....don't just stand on a side line and watch ...kila kura ina umuhimu katika taifa letu...Usipo vote usimlaumu mtu...
Nilituma article iliyo toka kaika kijarida Norway kuhusu maji safi mengi saaaaaaana kugunduliwa Dar es Salaam chini ya ardhi na NORCONSULT, ankal ukaitia kapuni! Loh!
ReplyDeleteHuwezi ukamwaga kijiko cha sukari baharini ukategemea utapata sukari, ugonjwa ni mkubwa kuliko tunavyofikiria! Unaanzia kwako wewe ambaye unajiita mlala hoi, mara ngapi unadanganya ili kufanikisha mambo fulani fulani?
ReplyDeletehaya matatizo yanatatulika kama sirikali ya ccm itaacha politiki na kufanya kazi.tuna mito inayo tiririka mwaka mzima na kuishia baharini...sio mto mmoja ipo zaindi ya mito 20 mikubwa ambayo ingetoa maji na hapo acha maziwa makubwa yenye maji yafaayo kwa matumizi ya binadamu.Jamani tunaweza rekebisha hili suala TWENDENI TUKAPIGE KURA....(halafu michuzi unanibaniaga commenst zangu...najua unaowaogopa)
ReplyDelete