Hii ni team ya Precision Air ikiwa na team ya ATR (France) kabla ya sherehe ya kukabidhiana ndege mpya aina ya ATR 72-500 nchini Ufaransa katika mji wa Toulouse. Katikati ni Group Managing Director and CEO wa PW Bwana Alfonse Kioko na kulia kushoto kwake ni President wa ATR. Ndege hiyo mpya iliyobatizwa jina la Kilimanjaro, tayari imeishatua jijini Dar es Salaam na inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho katika uwanja wa Julius Nyerere International Airport (JNIA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Asangalwisye KununukukulyaSeptember 23, 2010

    Alfonse Kioko tafadhali fanya uchunguzi wa soko kama linaruhu kutuma ndege huku Mbeya, nyanda za juu kusini, tumechoka kusafiri kwa barabara masaa zaidi ya 12 (kumi na mbili)kwenda na kutoka Dar!! Tunakaa kwenye mabasi mpaka staili zote zinaisha!!

    ReplyDelete
  2. Bwana Alfonse hao uliofuatana nao mbona hawajavaa kiitifaki, sehem kama hizo ni muhimu na ni Image ya kampuni yako lazima wangevaa kulingana na umuhim wa tukio na ingezingatiwa na watu mlioenda kukutana nao nikiangalia hiyo picha wengine casual sana pia kama vile uliwashtua hiyo safari au utafikiri uliwaomba watu toka mtaani wakusindikize tujaribu kuwa serious jamani hebu oneni wenzenu hapo walivyo smart hii inaonyesha ni kwa kiasi gani hatuko serious na mambo tunatake easy kila kitu.

    ReplyDelete
  3. Kwanza kulia kama vile A. Mfinanga?!
    Kama ni wewe hongera sana ndugu yangu maana ndoto zako za kuwa karibu na ndege hatimaye zimekamilika. Ni mimi kija wa Mzee Poti (ARUSESCO)

    ReplyDelete
  4. ATCL kwisha habari?

    ReplyDelete
  5. hao walio casual ni baadhi ya wakali wenyewe wa mambo hayo hapa nchini (the practical men). na huyo ni A.Mfinanga mwenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...