Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza Mh. Damian Green


Waziri wa uhamiaji atasema, idadi ya wanafunzi wa kigeni wanaoruhusiwa kuingia Uingereza "haikubaliki."

Katika hotuba itakayotolewa baadae, atahoji iwapo Uingereza inawavutia wanafunzi bora- ikiwa nusu tu ya visa zinazotolewa kwa wanafunzi zimetolewa kwa wale wanaosomea elimu ya juu.


Kauli za Bw Green zinatolewa huku utafiti wa wizara ya mambo ya ndani zikisema moja ya tano ya wanafunzi bado wako Uingereza, miaka mitano baada ya kupewa viza.

Wizara hiyo imewafanyia utafiti wahamiaji ambao hawatoki Ulaya waliokuja Uingereza mwaka 2004.

Kundi kubwa zaidi- takriban watu 185,000- walikuwa wanafunzi, na asilimia 21 bado walibaki nchini hata miaka mitano baadae.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya mambo ya ndani Danny Shaw alisema, pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wa kigeni, Bw Green ameamua suala la mabadiliko ya uhamiaji wa wanafunzi kulipa kipaumbele

'Shagalabagala'
Mawaziri pia wana nia ya kutathmini viza za kufanyia kazi kwani mbili ya tano ya kundi hilo wamebaki Uingereza baada ya miaka mitano.

Kabla ya hotuba yake, Bw Green alisema: " Hatuwezi kuhisi tu kuwa kila anayekuja hapa ana uwezo ambao Uingereza hauna."

Aliiambia kipindi cha redio cha BBC Radio 4: " Sitaki kuingilia mafanikio yaliyopatikana kwenye vyuo vyetu."

Bw Green alisema: "Kwanini wanabaki? Wanabaki kufanya nini? Hili ni jambo tunalotakiwa kuliangalia kwa upana zaidi hasa katika mfumo wa uhamiaji."

Ofisi ya takwimu za taifa zilizotolewa mwezi uliopita zilionyesha uhamiaji umeongezeka kutoka 33,000 hadi 196,000 kwa mwaka 2009.

Idadi ya viza zilizotolewa kwa wanafunzi zimeongezeka kwa asilimia 35 hadi kufikia 362,015.

Bw Green alisema takwimu hizo ni ushahidi tosha kuwa serikali ya muungano ilirithi mfumo wa uhamiaji ambao uko "shagalabagala"

Alisema, " Takwimu hizo zinaniambia kwamba tunatakiwa kuangalia njia nyingine zote zinazotumiwa na watu kuingia nchini, labda kwasababu ya elimu, sababu za kuungana na familia, na pia, hasa, njia zinazowapa ukaazi wa kudumu."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. TANZANIA PIA IONGELEE KUHUSU WAENGEREZA WANAOKUJA NCHINI TANZANIA NA UJASIRIMALI WA KIZUSHI.

    ReplyDelete
  2. mmmmh kazikweli kweli kama ulaya nimeshakuona nimalizie course yangu mie nirudi kwetu kama hatutakiwi tunang'ang'ania nini?...watanzania wenzangu mliokuja huku miaka 10 iliyopita bongo sio kama mlivyoiacha rudini nyumbanbi hata kama utapata shidi ni miezi 2 au 3 tu na kama una vyeti vyako utakula bata tu....najua kuna waosha vinywa wataanza kuchonga ila ukweli ndio huo...na kama hamtaki kurudi nani ataendeleza taifa?

    ReplyDelete
  3. HILI NENO "BEBA BOKSI" LIBADILISHE NINADHALILISHA. MIMI NIMEMALIZA KARIBUNI MASOMO NA NAKAA UK BAADA YA KUPATA BARAKA ZOTE ZA SERIKALI. KAZI NINGEPATA TZ NDIO LAKINI NIMERIDHIKA NA HAPA NA MWANANGU ANAKWENDA SHULE. NDUGU ZANGU VILE VILE NAWASAIDIA WAJE HUKU KUPATA ELIMU. MIMI NINA KAZI YANGU NA TATEKELEZA MAJUKUMU YANGU. TAFADHALI SANA USINIITE MBEBA BOKSI..!!

    ReplyDelete
  4. Hao ndio Conservative aka Torries aka washikaji wa Chadema. Hivi uchaguzi wa mwaka huu Torries hawajawapa mapesa Chadema? Au ni kutokana na ukata walionao uliosababishwa na depression lakini wanasingizia wahamiaji?

    Hawa sera zao tangu zamani hawataki wahamiaji ingawa PM wao alikwenda kujikosha India kwa wahindi ila wanawashikia bango wahamiaji kutoka Afrika. Wabaguzi kama nini hao wajomba zao Chadema!

    ReplyDelete
  5. tutabanana humuhumu maisha bora kwa wote, huduma nyeti ndo zinafanya tusirudi home, ambazo huko home zimekuwa ni kitendawili miaka karibia 50 ya uhuru, maji ya shida, umeme wa shida, huduma mbofumbofu, mifoleni asalaaleh, hospital mh! ebu niambie kweli ndio umepata kazi nzuuuri umetoka job, umerudi nyumbani no maji no umeme mbu wanakusubiri aaah, hii laifu ni ya vijijini na sio mjini, hata vijijini inawaboa sana ni basi tuu, kweli huko hata kwa winch siji, ngoma inogile

    ReplyDelete
  6. Mdau wa pili tatizo sio kwamba hawataki kurud weng walikimbia kilichowaleta sasa watarud vip na story walizowaisha, afadhali yako wewe bado upo shule ila asilimia kubwa huwa wanabwaga shule mim nipo USA na haya mambo wamefanya hata watu wangu wa karibu waliokuja mwaka huu., jaman ndugu zangu tufate kilichotuleta haya mengine hata bongo yapo tutaosha wazee wao mpaka lini

    ReplyDelete
  7. endeleza mwenyewe we ushapata pound unajishaua, rudi kivyako tuache kabisa,

    ReplyDelete
  8. Harudi mtu ng'oooooooooooo. Maboksi tutabeba. Wazee tuwahudumia kwa kuwabadirisha Diaper, lakini haondoki mtu. Maisha ni popote. Kazi ni aina yoyote ile, ili mradi tu inalipa. Mbona Tanzania watu wanauza, machungwa, mchicha, karanga, kuni, korosho, maembe, na wengineyo mengine. Kazi ni kazi ili mradi nisibague kilicho mbele yangu. Mimi hata niwe nafanya nini sirudi Tanzania kabisa zaidi ya kwenda kusalimia ndugu zangu. Haya mambo ya kudanganyana eti Tanzania maisha ni mazuri sitaki kusikia. Tutabanana hapa ULAYA na USA. Labda waniweke kwenye Ndege wenyewe, lakini mwenyewe hivi hivi harudi mtu.
    Nilitoka Tanzania na ka RN nalipwa TSHS 60,000/Mwezi. Sasa hivi nalipwa angalau $32.50/hr. Uniambie eti nirudi Tanzania!! Kufanya nini? Hata kama ningelikuwa nafanya kazi ya NURSING ASSISTANT siwezi kurudi Tanzania. Mshahara wa NURSING ASSISTANT ni mkubwa sana kuliko hata wa FULL PROFESSOR pale CHUO KIKUU. Sasa nirudi kutafuta nini huko kwa Mafisadi.

    Nitawafuta wazee mkojo na mavi, lakini Tanzania ni kwenda kusalimia tu.

    Mdau Kansas- USA

    ReplyDelete
  9. aisee kimenuka sasa!karandinga za uhamiaji zinafanyiwa sevisi litazoa kwanzia mitaa ya mjii wa kusoma hadi cardiffu haponi mtuu mwaka huu jamani.mdau hapo juu mbona wazungu kibao wanaishi tz bila kua na vibali na hamna anae wauliza wanaitwa sir na madamu !wanalipia visa ya miezi mitatu badaaa ya hapo wanapeta tu hivi hivi.makubwa sasa

    ReplyDelete
  10. wewe mdau wa pili ngoja mimi nisafishe kinywa kwa ufupi hujarudi ila maisha yalikushinda either because you were not qualified enough to get a good job to sustain yourself in uk or jibu unalo. nadanganya au i just hit the point isn't it? ofcourse you can't admit it. I'm in a same position dear i got a masters degree here and don't tell me i'll be just so happy to pack my luggage to come back to tanzania, kama nchi yangu is so happy kunipokea na kunipa kazi i'll do that tomorrow. the country is rotten. i will never ever look forward to come back only if i'm forced to do so but not for my own wish. i'm sure all of you out there you feel the same regardless of the posh life you live out there. IT sucks, the country is run by.....it is the shame that we were the one who suppose to share knowledge and experience but unfortunately we don't get the opportunities from our selfish corrupt system. i worked so hard to sponsor my studies of course i need to recover my cost before i live the country lakini kama baba yangu fisadi na alinilipia ada na shule hata nikashidwa kwenda akacha kunitumia pocket money kwanini nisirudi nyumbani how would i survive na hata cheti sina? lakini amenipromise nikirudi nyumbani atanipatia kazi BOT...why shouldn't i come back.....people think before ujaongea watu tuna hasira. it is just so sad we came here from the first place . we learned so much which is so not practical in our country. we just see so much wakati ndugu zetu wamelala.

    ReplyDelete
  11. Speak for yourself kila mtu ana maisha yake na anajua kinachomweka huko nchi za nje. Wengine ushambenga tu na kuona wivu wenzao wakiwa nje. Nilikwenda majuu nimekaa miaka 10 nimerudi mwaka jana na mimi nasema kama unaona home utamake zaidi ya huko njoo, lakini usisikilize ya mtu fuata moyo wako na siku ikifika unataka kurudi nyumbani tu na watu watakupokea kwa mikono miwili..NYUMBANI NI NYUMBANI...lakini mtu asikwambie kitu. Bongo hapa ni majumba mengi tu mazuri na wanayoyajenga ni hao hao wachache lakini maudhi na mambo ya kijinga jinga kama 1999. Kitu kidogo watakuzungusha mpaka ujiulize ni kwa nini. Watu wana viswahili virefu sana kila mtu anataka hela ya chai. Ukifanyiwa kidogo kitu hela ya chai sijui mikate itanunuliwa lini. Kwanza naona hata ni mambo mabaya kuliko 1999 umeme , maji, internet, simu, barabara ndio usiseme...Hospital mwee afadhali uishi USA bila insurance....I am telling the real truth nyumbani ni muhimu kurudi lakini mimi nawaambie niliyeishi huku na huko. Ukiona huko kumeshinda njoo nyumbani lakini hamna jipya huku...

    ReplyDelete
  12. Powa kaka mm nilikuwa huko mwaka na nondo zangu nilikuwa nazo Vyeti vya akili ila sijapata kazi zaidi ya £1000.00 kodi nyumba wanataka Laki 3 kwa mwezi academy ndio hizo kifupi nashangaa watu wanapenda sana kuwapa ushauri wenzao warudi wafanye nini hapa kila mtu kaja kivyake ukichoka anzaaa life kokote ndio maana JK akija huku hawaambi watu warudi nyumbani kwa vile anajua hamna kitu huko....

    Mm mzee wangu alikuwa Europe sana miaka ya 70's akaruidi TZ akapiga kazi akawa na nyumba gari nk maisha fresh 1990 kampuni ikauzwa hamna pension wala dole ndio tumekimbia maisha hayo. Tanzania sio kihivyo nimewakuta washikaji kibao wako makazini magari ya kukopa na mjengo wangu wa apartment mbili kodi kuipata zengwe huu mwaka wa tano nimeipangisha wapangaji wakihama mpaka taa wanang'oa ukiwa huku unadanganywa kazi nyingi lakini nenda ndio utajua na wanabakia kule wengi waliondoka hawakuchukua nongo au waliunguza visa.... nyie tangulie tutakuja tukiwa tayari ila acheni kudanganyana ukipata opportunity hapa tumia mbeba box sio wengi wetu tumetoka kwenye familia masikini lakini tumefanya kazi tumeweza kujenga vijumba, kujisomesha na kusomesha ndugu zetu powa ila life kokote sijawahi sikia mzungu amezamia kwenda Africa kutafuta maisha bora ..

    ReplyDelete
  13. tutaosha wazee wao mdau mpaka watakapokua hawatulipi.....harudi mtu...kuhusu shule...sio wote wanalipiwa km ww mdau mwingine..ngoma ngumu,...kama hakijaeleweka uk, usa o canada ndio kitaeleweka bongo wadhani....
    sio wote baba zetu wapo serikalini...habar ndio hio

    ReplyDelete
  14. Watu warudi Bongo kufanya nini? ukiosha mzee unapata pesa ya uhalali, ukibeba box unapata pesa ya jasho lako. Sasa tukirudi wote bongo kama si kuchanganyikiwa ni kitu gani, haswa sisi watoto wa wakulima, baba zetu wameishia kijijini hujui mtu mjini au kiongozi nani atkuangalia wewe usoni na kukupa kazi? Kuna watu wanavyeti vyao lakini hata kacontract ka bada la kuku huwezi kuapta ni mapka umjuwe mtu ule nae, wakati huu umekaa zako watu wankukimbilia kukupa kazi za kubeba mabox zaidi, ukizeeka ukirudi nyumbani unaweka mguu juu unakula pesa zako za uzee za uhakika unakwenda tu ubalozini unapewa cheak yako ya uhakika unarudi nyumbani kwako kupunga upepo. Huna wasiwasi wa kupata sh. elfu moja kama kiinuwa mgongo chako. Hata hiyo sh. elfumoja wengine wameikosa kwani wanaambiwa hawajawahi kuipata uzeeni. Hali inatisha sana, haswa kwa sisi watoto wa wakulima ambao hakuna naetuangalia zaidi ya kutaka kura zetu.

    ReplyDelete
  15. Tarehe Tue Sep 07, 12:03:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous AnonymousNimekusoma jamaa nakunyaka si unakaa kwa mtogole, poa mkuu upo kiulayaulaya kwenye blog ya michuzi wakati unakaa tandale, shenzi kabisa sasa unalrimgia nini kuchamba vizee na kupiga deki miaka hamsini hakuna maendeleo wewe mwenyewe umeshindwa kuwawekea wazee wako umeme home akuendelezee shosti wa mama

    ReplyDelete
  16. anon wa 8:11:00 AM
    we ndo kidaka mate kweli alokwambia mie mwanaume nani?? mie ni demu naishi canada kwa raha zangu zote, nimejengea wazazi wangu nyumba ya ukweli!
    sasa kama una darubini ya mbao pole zako na dhiki zako, utajibeba kweli mwaka huu usinifananishe na wewe hunifikii hata ukucha najua we ni mwanaume mmbeba lumbesa tuu, na shenzy ni wewe huna mbele wala nyuma kurukia mambo ka chakubimbi, kama wakaa tandale sogea sogea hadi gongo la mboto,
    umefulia wewe tuma namba nikutumie vidolari na western union!!!
    nikalale mie byee
    mdau, mamaaa ya canada!!!

    ReplyDelete
  17. Mdau wa KANSAS-USA...asante sana mkuu umeongea ukweli mtupu.Blessed!!!
    Mdau-Mji wa Kusoma!!!

    ReplyDelete
  18. Jamani kwa mpango huu bora chama cha 'LABOUR' kirudi madarakani Lol hawa 'CONSERVATIVE' wanavyotaka sifa...eeeh Mnyaazi Mungu tunakuomba uwe nasi daima!!!
    Mdau-Mji wa Kusoma!!!

    ReplyDelete
  19. HAMNA LOLOTE STRESS TU ZINAWASUMBUA! ULAYA MY FOOT!M TATOA SABABU CHUNGU MBOVU NDO MAANA MNAPATA MATATIZO HUKO NA KUKAA SIKU KIBAO MKISUBIRI MICHANGO MSAFIRISHWE KURUDI BONGO!KUNA WENGINE HAPO HAWAWEZI HATA KUJA KUZIONA FAMILIA ZAO,HADI MISIBA YA WATOTO NA WAZAZI WAO WANAISIKILIZIA KWENYE SIMU!LAANA TUPU ZIMEWAJAAA,HALAFU MNAJIDAI MAISHA MAZURI...WANGA NYIE MMELOGEWA ULAYA..HAYA LAMAANA LIPI MNALOFANYA HUKO?STRESS ZINAWASUMBUA NA ULIMBUKENI...BLALIFUUUUUUUUUUTS WOTE MNAOJIDAI ULAYA NDO KUNA MAISHA.

    ReplyDelete
  20. HAMNA LOLOTE STRESS TU ZINAWASUMBUA! ULAYA MY FOOT!M TATOA SABABU CHUNGU MBOVU NDO MAANA MNAPATA MATATIZO HUKO NA KUKAA SIKU KIBAO MKISUBIRI MICHANGO MSAFIRISHWE KURUDI BONGO!KUNA WENGINE HAPO HAWAWEZI HATA KUJA KUZIONA FAMILIA ZAO,HADI MISIBA YA WATOTO NA WAZAZI WAO WANAISIKILIZIA KWENYE SIMU!LAANA TUPU ZIMEWAJAAA,HALAFU MNAJIDAI MAISHA MAZURI...WANGA NYIE MMELOGEWA ULAYA..HAYA LAMAANA LIPI MNALOFANYA HUKO?STRESS ZINAWASUMBUA NA ULIMBUKENI...BLALIFUUUUUUUUUUTS WOTE MNAOJIDAI ULAYA NDO KUNA MAISHA.

    ReplyDelete
  21. SAfi sana watimue wote hao kazi tu kikimbia makwao na kuanza kutumikia wazungu wakati NChi yenu ndo imeasomesha, ni kweli waziri watimue wote warudi makwao.

    Kuna wengine hata haya hawana eti huduma bora ziko ulaya wewe unaakili kama za dagaa anayefuata chambo kwenye mwanga, Hao waingereza walijengewa na nani miundo yao mizuri, kazi kukwepa majukumu tu #$^^$#@(*&*^%@! WEE? WAONE.

    Tunahangaika na kupiga kura wewe tu unang'aa na macho huko, badala ya kuja tuungane tujenge nchi.

    Shule zenu kweli zimewasaidia.

    WAZIRI watimue wote warudi kwao kama walivyofanya ufaransa. Wanawamalizia hewa yenu mliyoipata kwa jasho.. NATAMANI TIMBWILI TIMBWILI LIANZE KESHO

    ReplyDelete
  22. Nitafungua matawi ya CCM na Chadema na CUF mie na washirika wangu ili wazee wakija ughaibuni tujikombekombe watuone na watukumbuke tukipigwa bomba kurudi bongo.
    Hiyo ndugu zangu ughaibuni ndio strategy na ushauri wa bureeeee
    Njaa haina bouncer

    ReplyDelete
  23. Nadhani tatizo la msingi ni hili hapa
    http://thegraduati.blogspot.com/2010/08/future-of-university-graduates.html

    go and read it.

    ReplyDelete
  24. http://thegraduati.blogspot.com/2010/08/future-of-university-graduates.html

    there you will learn about our problem.

    me
    Tz

    ReplyDelete
  25. Wazungu wamehamia Afrika wapo wengi tu kwa sasa Tanzania na wanpigiwa magoti na kila mtu, na wanapata kila kitu hata trafik barabarani hamkamati kwani akiongea tu kingereza Polisi anmuachia, nimeona mwenyewe kuanzi uwanja wa ndege hwaguswi, nenda arusha Njiro uone wanchokifanya kwa mabinti zetu ni huzuni tu. Kwani kaka zetu na wenyewe wameanza biashara za kuuza dada zao kwa wazungu, aibu kali. Nenda mrogoro kuna mashamba thanks God ndugu zetu wanapata kibaruwa na wakina mama wanapat pesa ya kununuwa maziwa ya watoto.Hata wazungu wanzamia Afrika pia lakini wanitwa jina lingine.

    ReplyDelete
  26. Hata wanitwishe jiwe zito la namna gani nimesema na kusema Tanzania sirudi, zaidi ya kwenda kusalimia ndugu zangu nakurudi. Hivi mimi ndo najua jinsi kufuta wazee mkojo na mavi vinavyolipa. Kila mtu anatamani kufika huku kufanya kazi ya aina yoyote. Mtu nimetoka Tanzania sijui kuendesha na kagari sina, leo hii nina gari kangu nilikokapata kutokana na kazi yangu ya kussaidia wazee, sasa leo hii mtoto wa kike uniambie nirudi kwa mafisadi si unanitafuta maneno jamani!!!!! Wanaotaka kurudi nyumbani ni uvivu tu wa kubagua kazi. Na wakirudi nyumbani wanapata shida kama. Mimi nawaona Madakitari wanaotoka KCMC, BUGANDO na MUHIMBILI kuja kujifunza jinsi ya kutumia vifaa mbali na kufanya research. Wanapita pembeni wanakuomba uwatafutie kibarua hata cha $ 6 ili mtu akirudi nyumbani awe na chochote mfukoni. Sasa watu mnasema eti turudi Tanzania kwa kazi gani na kufanya nini? Jamani kubeba maboksi na kusafisha wazee ni kazi nzuri sana na yenye FULL BENEFIT. Waulize FULL PROFESSOR pale CHUO KIKUU ni wangapi wana angalau BIMA YA AFYA? Jamani Watanzania wenzangu naomba tuache kudanganyana kuhusu suala la kurudi Tanzania. Tulieni hapa ULAYA na USA mkafanye kazi ya aina yote inayokuja machoni kwako. Msibague kazi. Tanzania hakuna chochote. Wale wanaorudi nyumbani ni wavivu wa kufanya kazi na wengine ni watoto wa mafisadi amabo anajua kamaliza shule huku ataenda mzazi wake fisadi amtafutie International Job. Lakini wewe amabye unajua ulitoka familia ya namna gani na unaelekea wapi katika maisha yako usichague kazi. Huyo anayekuja kwako kukwambia kuwa yeye anarudi Tanzania ni PEPO KIKOTI. Acheni kusikiliza maneno ya watu wengine. Kumbuka kwanza ile siku ulipopewa Visa wenzako wakanyimwa na mlikuwa wangapi? Hizi nafasi za kuja ULAYA na USA watu wengi wanazililia sana. Lakini kupata VISA ni ngumu sana. Mimi nimeisha sema sirudi Tanzania ng'ooooooooooooooooo labda waniweke kwenye ndege wao wenyewe, lakini eti nifanye upumbavu wangu na kimbele mbele kama mkojo wa asubuhi eti narudi Tanzania kamwe sitorudi. Tutabanana na wazungu kwa weusi.
    Nilizunguka na BAHASHA YA KAKI nikiwa Tanzania natafuta kazi nikachoka. Hadimtu akaniambia dada kama humjui mtu yeyote Wizara ya Afya huwezi kupata kazi wala shule. Inabidi utoe chochote. Na hapa nilienda Mnazi Mmoja Hospitali na Amana. Acha tu niwafute wazee mkojo na mavi kazi ni kazi.

    Mdau KANSAS -USA

    ReplyDelete
  27. Hata wanitwishe jiwe zito la namna gani nimesema na kusema Tanzania sirudi, zaidi ya kwenda kusalimia ndugu zangu nakurudi. Hivi mimi ndo najua jinsi kufuta wazee mkojo na mavi vinavyolipa. Kila mtu anatamani kufika huku kufanya kazi ya aina yoyote. Mtu nimetoka Tanzania sijui kuendesha na kagari sina, leo hii nina gari kangu nilikokapata kutokana na kazi yangu ya kussaidia wazee, sasa leo hii mtoto wa kike uniambie nirudi kwa mafisadi si unanitafuta maneno jamani!!!!! Wanaotaka kurudi nyumbani ni uvivu tu wa kubagua kazi. Na wakirudi nyumbani wanapata shida kama. Mimi nawaona Madakitari wanaotoka KCMC, BUGANDO na MUHIMBILI kuja kujifunza jinsi ya kutumia vifaa mbali na kufanya research. Wanapita pembeni wanakuomba uwatafutie kibarua hata cha $ 6 ili mtu akirudi nyumbani awe na chochote mfukoni. Sasa watu mnasema eti turudi Tanzania kwa kazi gani na kufanya nini? Jamani kubeba maboksi na kusafisha wazee ni kazi nzuri sana na yenye FULL BENEFIT. Waulize FULL PROFESSOR pale CHUO KIKUU ni wangapi wana angalau BIMA YA AFYA? Jamani Watanzania wenzangu naomba tuache kudanganyana kuhusu suala la kurudi Tanzania. Tulieni hapa ULAYA na USA mkafanye kazi ya aina yote inayokuja machoni kwako. Msibague kazi. Tanzania hakuna chochote. Wale wanaorudi nyumbani ni wavivu wa kufanya kazi na wengine ni watoto wa mafisadi amabo anajua kamaliza shule huku ataenda mzazi wake fisadi amtafutie International Job. Lakini wewe amabye unajua ulitoka familia ya namna gani na unaelekea wapi katika maisha yako usichague kazi. Huyo anayekuja kwako kukwambia kuwa yeye anarudi Tanzania ni PEPO KIKOTI. Acheni kusikiliza maneno ya watu wengine. Kumbuka kwanza ile siku ulipopewa Visa wenzako wakanyimwa na mlikuwa wangapi? Hizi nafasi za kuja ULAYA na USA watu wengi wanazililia sana. Lakini kupata VISA ni ngumu sana. Mimi nimeisha sema sirudi Tanzania ng'ooooooooooooooooo labda waniweke kwenye ndege wao wenyewe, lakini eti nifanye upumbavu wangu na kimbele mbele kama mkojo wa asubuhi eti narudi Tanzania kamwe sitorudi. Tutabanana na wazungu kwa weusi.
    Nilizunguka na BAHASHA YA KAKI nikiwa Tanzania natafuta kazi nikachoka. Hadimtu akaniambia dada kama humjui mtu yeyote Wizara ya Afya huwezi kupata kazi wala shule. Inabidi utoe chochote. Na hapa nilienda Mnazi Mmoja Hospitali na Amana. Acha tu niwafute wazee mkojo na mavi kazi ni kazi.

    Mdau KANSAS -USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...