Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea Haki za Watoto nchini, Nimka Lameck (11) akiwa katika jukwaa la siasa akiwa anahutubia na kutoa sera mbalimbali ambazo wananchi wanatakiwa kuzifuata ilikuepuka kuwanyanyasa watoto pamoja na kukemea ukatili dhidi ya watoto nchini.

Na Ripota Wa Globu Ya Jamii.

JAMII na mamlaka husika zimetakiwa kuchukua hatua ya haraka ya kuhakikisha inawalinda watoto ilikuepuka matatizo mbalimbali ikiwemo vitendo vya kilaghai na ukatili vinavyofanywa na watu wasio jali hutu wa watoto.


Akiongea na Globu ya Jamii jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea Haki za Watoto nchini, Nimka Lameck (11) alisema kipindi hichi kumekuwapo na vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto wadogo huku jamii ikinyamaza.

Nimka alizitaka mamlaka kuchukua hatua za haraka ikiwemo kuwalinda watoto waliohitimu elimu ya shule za msingi hivi karibuni hususan watoto wa kike ambao kwa asilimia kubwa wapo hatarini kushawishika na walaghai hao maafu kama ‘Mafataki’.

“Watoto wanahitaji kuangaliwa kwa umakini na kulindwa kuepuka matatizo ya kutendewa mahovu kwa jamii isiyo na hutu wa watoto wadogo ambao wanakatisha ustawi wa watoto nchini” alisema Nimka.

Alitoa wito kwa wazazi kuwa na mwamko wa kuchunguza mienendo ya watoto wao mara kwa mara ikiwemo kuwakataza tabia hatarishi ambazo wanaweza kukumbana nazo kipindi wawapo majumbani.

Katika hatua nyingine, Nimka alikemea na kurahani vitendo vya kikatili vilivyolipotiwa kwenye vyombo vya habari juu ya watoto wadogo kuuwawa kikatili ikiwemo na kubakwa vilivyofanywa na watu wazima.

“Vitendo vilivyolipotiwa vimesikitisha,vimetikisa watoto wengi si wa Tanzania tu, bali hata dunianikote kwani watoto waliotendewa unyama huo walikuwa hawana hatia tunaomba sheria kali dhidi ya wahusika” alisema Nimka.

Aidha, alisema kwa sasa yupo katika hatua ya mwisho kuandaa mpango maalum juu ya kutoa changamoto kwa watoto hapa nchini utakaoitwa ‘Haki Mtoto’.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. MKUU WA WILAYA YA NANIHII. NAKUTAKIA HERI YA IDD. Pia nadhani kichwa cha habari hapa juu kina maana WATOTO WANATAKIWA KULINDWA DHIDI YA WALAGHAI. Hapo juu nadhani ina maana kwamba tuwape walaghai wawalinde watoto wetu.

    Mdau,
    Ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Raisi Kikwete kesha sema kwamba wanaopata mimba ni kutokana na kiherehere. hivi huyu mtoto anapingana na Raisi wake?

    ReplyDelete
  3. yeye mwenyewe anatakiwa kulindwa kwa sababu haki zake za kimsingi zimevunjwa. miaka 11 hatakiwi kutumiwa kwenye majukwaa ya siasa.

    ReplyDelete
  4. Acheni watoto wawe watoto jamani, msiwahusishe na majukwaa yenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...