Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advocate Nyombi


Na Mohammed Mhina, Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, limemkamata na kumfikisha Mahakamani mfanya biashara mmoja ayetoa taarifa za uongo kuwa katika eneo la Tunduma mpakani mwa Tanzania na Zambia kulikua na gari lililobeba nyaraka bandia na masanduku ya kupigia kura wakati huu wa kampeni za uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika(31 october) mwisho wa Mwezi huu nchini kote.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advocate Nyombi,amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Victor Mateni (32), mkazi wa Sikanyihu Tunduma wilayani Mbozi.

Kamanda Nyombi amesema kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo, kumetokana na taarifa zake alizozitoa kwa Mkuu wa Idara ya Forodha mpakani hapo za kuwepo kwa nyalaka hizo kutokua za kweli baada ya magari yaliyotajwa kufanyiwa upekuzi wa kina na kutopatikana kwa nyaraka na masanduku hayo kama ilivyodaiwa na mtuhumiwa huyo.

Amesema “ Jumamanne Oktoba 19, mwaka huu mfanyabiashara huyo alimwendea Bw. Jovitas Kanisha Charles ambaye ni Mkuu wa Idara ya Forodha mpakani hapo na kumwambia kuwa gari lenye namba za usajili T.288 BHR aina ya Iveco likiwa na tela lenye namba T. 966 BKS mali ya Kampuni ya usafirishaji mizigo hapa nchini ya AZANIA lilikuwa limebeba shahasa na mabokisi hayo bandia na vilikuwa vikiingizwa nchini kwa siri”alisema kamanda nyombi.

Amesema Mkuu huyo wa Idara ya Forodha mpakani Tunduma, aliwasilisha taarifa hizo kwa Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama hapo mpakani na kuitisha kikao cha dharura kuitathimini taarifa hiyo.

Kamanda Nyombi amesema wakati wa kikao hicho cha dharura kamati hiyo iliamua kufanya upekuzi wa kina katika gari hilo pamoja na tela lake ili kubaini ukweli wa taarifa hizo na kuchukua hatu za kiusalama.

Amesema wakati wa upekuzi huo, kamati hiyo pia ilimshirikisha mtoa taarifa ili naye ashuhudie kitakachopatikana lakini hadi mwisho wa upekuzi kulikuwa hakuna nyaraka ama masanduku ya kupigia kura yaliyobainika.

Amesema gari hilo lilikuwa na bidhaa mbalimbali za madukani ambazo ni za halali kwa kusafirishwa na kwa matumizi. Bidhaa hizo zilikuwa zikisafirishwa kutoka Afrika ya Kusini kwenda kwa wafanyabiashara wawili wa Jijini Dar es Salaam.

Kamanda huyo amesema baada ya upekuzi huo kutobaini kosa walimkamata mfanyabiashara huyo na kumfikisha mahakamani kwa kutoa taarifa za uongo na kesi yake imeahiirishwa hadi itakapotajwa tena Novemba 4, mwaka huu na mtuhumiwa amepelekwa rumande.

Huyo ni mtu wa pili kufikishwa mahakamani katika kipindi kisichozidi wiki moja kwa kutoa taarifa za uongo na kusababidha athari kwa watu wengine na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Kamanda Nyombi amesema makachero wa Polisi mkoani humo wanamsaka mtu mwingine ambaye pia alisaidia kueneza taarifa za uvumi huo.

Jumanne wiki hii, Mwenyekiti wa Wazee wastaafu wa iliyokuwa Afrika ya Mashariki Nathan Mlaki, alijisalimisha Polisi Jijini Dar es Salaam na kufikishwa Mahakamani kwa madai ya kutoa taarifa za uongo kuwa mmoja ya wazee wastaafu wa iliyokuwa Jumuia hiyo amefariki dunia baada ya kumwagiwa maji ya kuwasha na Polisi wakati walipofunga barabara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Lisemwalo lipo kama halipo basi laja

    ReplyDelete
  2. Advocate JashaOctober 21, 2010

    Ankal ulikua kimya zilipipatikana taarifa hizo kuhusu karatasi hizo.zZiwe za uzushi au la lakini umekua wa kwanza kuweka habari hii katika blog yako kuhusu kukamatwa kwa mtoa taarifa.Kuna maswali zaidi ya majibu.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  3. Tanzania hakuna haki wizi umetawala,hata km zimekamatwa ukweli hautangazwi kamwe kwa nchi yetu,masikini anazidi kunyonywa na tajiri mafisadi wanazidi kujiongezea kipato,Wasomi wanaona ona mbali hawakubaliwi kupiga kura huo ni wizi unyanyasaji wa khali ya juu.Mungu ibariki Tz wabariki wanyonge tenda miujiza.

    ReplyDelete
  4. Aisee Michuzi Huyu Kamanda Nyombi naweza kumpata vipi, alikuwa Mshikaji sana wakati anasoma sheria kule Athens, Ugiriki.Nipo nje ya Nchi vinginevyo ningemzukia mwenyewe huko Mbeya.

    ReplyDelete
  5. WAPEWE ADHABU KALI WATU KAMA HAWA IWE FUNDISHO MAANA WANGEWEZA KULETA MADHARA KWA JAMII, NA PIA KATIBU MKUU WA CHADEMA APEWE ONYO KALI ASIKURUPUKE TUU, NA KUTOA TAARIFA AMBAZO NI ZA HATARI INGAWA ANAJIPIGIA DEBE KWA STAILI HIYO. TENA HATA AKAOMBA RADHI WANANCHI KWA KUENEZA UONGO!!TENA ALIDAI KUWA KAPATA TAARIFA TOKA KWA VIJANA WAKE BAADHI WAKIWA TRA!!KWA MTU KAMA YEYE ILIKUWA KWANZA AFANYIE UCHUNGUZI KABLA YA KULITANGAZA HADHARANI.INANIJIA TASWIRA KUWA KTK MABOMU YAKE ANAYODAI KUKURUPUKA NA KULIPUWA NI NUSU KWA NUSU KUNA YA UKWELI NA UONGO AJIREKEBISHE

    ReplyDelete
  6. HUU NI UTOTO, YAANI HUYO JAMAA WAMEWEZA KUMKAMATA NDANI YA SIKU MOJA BAADA YA KUTOA HUO UZUSHI, NA BAAHI MBAYA ALIKUWA HAJULIKANI. MBONA REG. MENGI AMEWEZA KUWATAJA
    MASWALI MAGUMU: WABAYA WA MTOTO WAKE KWA MAJINA HAWAKUKAMATWA? BADALA YAKE TUME IMEUNDWA, SASA INACHUNGUZA NINI SI WANAJULUKANA? WAKATI JAMAA WANAJULIKANA? NA MBONA UCHUNGUZI UNACHUKUA MDA MREFU HUKU JAMAA WANAJULIKANA? LKN HUYO MSHKAJI ALIETOA UZUSHI UCHUNGUZI UMECHUKUA MASAA TU NA AMEKAMATWA? INJUSTICE, INJUSTICE, INJUSTICE THRU OUT? MTAMPONZA JK NYINYI.

    ReplyDelete
  7. Mambo ya vitisho yapo Tanzania haswa katika uwanja wa ndege Dar es Salaam, nakumbuka kuna msichana alifuatwa na jamaa walieyesema wanafanya kazi uhamiaji wakati anataka kugongesha passport yake, wakamwamwambia wazi,sisi tunafanya kazi hapa unaona wale maofisa wa uhamiaji na wote wengine pamoja hata ukilalamika hakuna ataekusikiliza hapa ndani au nje, sasa utapokwenda kugongewa passport uhamiaji tunataka uweke pesa katikati ya passport yako usipofanya tutakupakazia hata safari yako usiende.

    Yule msichana akamwambia sina pesa hapa ngoja nikamwite ndugu yangu nje akatoka na kumwita ndugu yake ambae aliambiwa maneno hayo hayo na akatoa pesa kwasababu hakupenda matatizo na safari yake ivunjike.

    Msichana akagongewa passport yake baadae akaenda kukaa,baada ya muda yule jamaa wakamfuata tena na kumwambia pesa zile hazikutosha tupo wengi unaona wengine wale, yule mama kwa kuogopa na kutokana na umuhimu wa safari yake ikabidi awape pesa nyengine dollar kati ya pesa ambazo alipanga
    kusafiri nazo.

    Kwahiyo naomba viongozi wachunguze saana mambo yanayofanyiwa airport kwa wasafiri wasishangae ya Mengi, wengi hawaripoti usumbufu wanaopata maana wanajua hakuna kitachofanyika ni kama kesi nyani unampelekea tumbili.

    ReplyDelete
  8. Mwandishi wa habari hii hajazingatia misingi ya taaluma ya habari. Ni taarifa ya upande mmoja kwakuwa hatujaelezwa maoni na maelezo ya mtuhumiwa. Kuna kila dalili kuwa kuna ukweli unafichwa hapa. Ninachoona ni kuwa zama za kuiendesha nchi mzobemzobe zinakaribia kwisha. Labda wawakamate Watanzania wote milioni 40+. Rashidi wa katika KULI alisema: "Yana mwisho haya"

    ReplyDelete
  9. KELELE ZA KITOTO ZIKOME, PENYE JUSTICE NI MAHAKAMANI PEKEE. KAMA ATAPATIKANA MTU NA HATIA, BASI ATAJUTIA KUROPOKA NA AKISHINDA ALIPWE GHARAMA ZA KUDHALILISHWA..... MDOMO ALIMPONZA KICHWA.

    ReplyDelete
  10. Hadj Drogba "mwana chelsea"October 22, 2010

    Huyo dogo victor mateni mi namjua,tulikua nae maisha ya sangu secondary mbeya 1990's lakini alikua nyuma yetu,kuna kipindi nadhani uchaguzi uliopita aligombea ubunge kupitia NCCR Mageuzi maeneo ya huko kwao mbozi.Ni mtoto wa hapohapo tunduma,amezaliwa na kukulia hapo border,nimeshangaa sana kusikia anahusishwa na tuhuma nzito kama hiyo,nadhani dogo hasira dhidi ya ccm ndio zimemponza mpaka kuzusha habari hizo,vijana wa tunduma hawaipendagi ccm miaka na miaka,hatari sana.

    ReplyDelete
  11. wadau kwa jinsi ninavyomjua huyu mkwele, huyo jamaa ataozea jela kama babuseya, haluuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  12. tz iko kinyume kweli.. sasa mnamkamata informer badala ya kumpongeza ili kesho wengine wakiona kitu suspicious wawape habari? kesho nani atawapa habari hata kama anaona watu wanaenda kulipua somewhere?? si kila mtu ataogoa kufungwa
    mi ntaishi hukuhuku ng'ambo

    ReplyDelete
  13. maskini Victor....yana mwisho haya-KULI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...