Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Yohana Balele (mwenye suti nyeusi) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Singili (kulia) wakizindua rasmi tawi la benki hiyo la Kahama mkoani Shinyanga mwishoni mwa wiki, anayeshuhudia kushoto ni Kaimu Mwenekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo Andulile Mwakalyelye.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Yohana Balele (mwenye suti nyeusi) akipokea maelezo ya utendaji wa benki ya Azania kutoka kwa Meneja wa tawi jipya la benki hiyo la Kahama Evaresti Muhogosi alipofungua tawi jipya la benki hiyo mjini Kahama mkoani Shinyanga mwishoni mwa wiki.
Kikundi cha Sanaa cha Kahama Medical Cultural Troup cha mjini Kahama mkoami Shinyanga kikitumbuiza wakati wa hafla ya ufunguzi wa tawi jipya la Benki ya Azani la mjini Kahama mwishoni mwa wiki.

***** ****** ******

Na Mwandishi Wetu, Kahama

BENKI ya Azania imeendelea kujiimarisha kwa kufikisha mtaji wa sh. bilioni 18.4/- katika miaka kumi ya kujiendesha tangu mwaka 1995. ilipoanzishwa rasmi ilipokuwa na mtaji wa milioni 700.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa tawi jipya mjini Kahama mkoani Shinyanga uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Charles Singili alisema benki hiyo inaendelea na mikakati kuhakikisha kuwa huduma zao zinaendelea kuimarika kadri miaka inavyosonga mbele.

Alisema mafanikio waliyofikia ni matokeo ya kazi na usimamizi mzuri wa menejimenti ya benki hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kibenki wakiwemo wateja wanaounga mkono huduma zao ambapo alitoa shukrani kwa jamii nzima ya kitanzania inayotumia huduma hizo.

Benki hii ilianzishwa na watanzania,lakin kwa saa hivi ina wamiliki wenye hisa. Hawa ni NSSF 35%, PPF 30%, PSPF 12%, NAPF 14%, EADB 6% na wadau wengine wa kawaida wa kitanzania wanaomiliki 3% ya hisa za benki hiyo.

Singili alisema kuwa wanaendelea na mipango ya kupanua huduma zao katika maeneo mbalimbali nchini ambapo kwa sasa wametoa kipaumbele katika miji ya Geita, Katoro na Kagongwa ili yaweze kupata huduma za benki hiyo kwa lengo la kufungua matawi mengine katika ukanda wa Ziwa.

“Sanjari na maeneo hayo ya Kanda ya Ziwa lakini pia benki hiyo inatarajia kufungua matawi mengine katika mikoa ya Dodoma,Morogoro, Ruvuma na Mbeya katika mji wa Tunduma”, alisema Sinjili .

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinganya Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Balele ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisema, serikali inaunga mkono jitihada zinazofanywa na benki ya Azania katika msingi wa kuelekea mafanikio ya kiuchumi kwa watanzania na taifa kwa ujumla.

Balele aliongeza kwa kusema kuwa mbali na huduma nyingine zinazotolewa na benki hiyo ni mikopo kwa wajasiriamali wadogowadogo ambao wanatumia huduma hiyo kama msingi wa kujiletea maendeleo na kukuza pato la taifa.

Tunaipongeza benki ya Azania kwa kuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo lakini taasisi hii ihakikishe kuwa inafungua matawi mengine katika ukanda huu na tunaahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kufanikisha mipango hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Benki hii wenyewe ni akina nani?

    Naomba tufahamishwe

    ReplyDelete
  2. MICHUZI mwaka 95 dola 1 ilikuwa sawa na shillingi 350 kwa hiyo jamaa walianza na msingi wa dola million mbili sasa hivi dola moja ni 1500 kwa hiyo wana msingi wa dola milioni 12..took them 15 years to get to that point..akili kukichwa

    ReplyDelete
  3. Wenyewe ni nssf, ppf, lapf, pspf, eadb na wafanyakazi wake wana 4 % ya shares. kwa maelezo zaidi ingia kwenye website yao.azaniabank.co.tz. Ni moja ya benki za kizalendo kabisa kwa mtanzania.

    ReplyDelete
  4. Jamani huyo mkuu wa mkoa sio brigedia mstaafu,huyo bado ni mwanajeshi na bado ana muda mrefu wa kulitumikia jeshi la wananchi

    ReplyDelete
  5. Misoup hii usipo toa basi na wewe ni fisadi wa maendeleo. Hiyo benki wananchi wanatakiwa waelekezwe kua ni benki yao ya wazawa waitumie wasiogope na kwa fununu fununu tu ni kwamba wakurugenzi wake ni vichwa vya kuotea mbali wanajua kazi ya benki inatakiwa iendeshwe vipi. Namba zote ni waadilifu na wana machungu na akiba za watanzania. Share holders wenyewe umewaona hapo kuna kufilisika hapo amkeni wananchi hiyo ndio benki ya kuweka akiba zenu. HAINA MAKELELE LAKINI MAMBO YAKE MMEYAONA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...