Balozi Peter Kallaghe akiongea na Watanzania wa Birmingham na vitongoji vyake.alikutana na Watanzania wa Birmingham na vitongoji vyake siku ya jumamosi tarehe 02/10/2010.Katika mkutano huo ,Mh. Balozi Kalaghe aliwaahidi Watanzania hao kushirikiana nao katika kipindi chake chote akiiwakilisha Tanzania kama Balozi katika nchi hiyo.Mh. Kallaghe aliwasisitiza Watanzania kuzidi kuwekeza katika sekta tofauti kama kilimo, biashara na taaluma mbalimbali nyumbani.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,Mh. Peter Kalaghe (pili kulia) na mkewe Joyce Kallaghe wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TA na wanafunzi wanaosoma lugha ya Kiswahili, huduma ambayo inatolewa na TA-Birmingham.
Watanzania wakimsikiliza Mheshimiwa Balozi Kallaghe
Mama Balozi, Joyce Kallaghe akiwa katika picha ya pamoja na kina mama na kina dada waliodhuria Mkutano huo.
Mh.Balozi Peter Kalaghe na mkewe Joyce Kallaghe waliwa katika picha ya pamoja na Watanzania wa Birmingham na Vitongoji vyake.

Unajua nilisomaga Primary na msichana anaitwa Joyce Kalaghe na kaka yake alikua anaitwa Peter Kalaghe. Baba yao alikua Traffic officer..
ReplyDeletejamani yani hakuna hata kitukimoja kinacho waonyesha nyiee ni wabongo, mlishindwa hata kuweka bendara kama siyo kuvaa tshirt za kibongo au kujitaidi kuonekana wa kibongo bongo
ReplyDeletemdau wa Oct 04 10:08:00pm unasema ulisoma na hao kina Joyce na Peter Kalaghe sasa sisi itusaidie nini?. na hao waliosoma na kina Chelsea Clinton na kina Prince Harry watasemaje ? wakati mwengine Michuzi utumbo kama huu usiweke kwenye blog yako .
ReplyDeleteMdau kumbe ulisoma naura primary eeh? manake peter kalaghe tulikuwa naye, na wewe mdau hapo juu acha mashauzi kwani kina chelsea clinton ndo ushuz gani ni binadamu na tena one day watakufa tuu kama watu wengine au unadhani wameumbwa na gold? acha kuabudu watu ufala mwingine bwana, we ndo uloandika utumbo wa bata na hii sio blog yako, mwenye blogu hajakereka dume zimaa kapike kisamvu huko.
ReplyDeleteBalozi wetu Mjamaa kweli, hana makuu maana karudia shati! alilivaaga kwenye shughuli fulani mahala fulani canada. haaa!
ReplyDeleteMbona tupicha kidogo wala hatuonekani sawasawa. Kamera bomu au??? Wabongo bwana!
ReplyDeleteYAANI HAO NDIO WABONGO WOTE WALIOKO B'GHAM? M AIBU, INGEKUWA ANAKUJA TONY BLAIR KUWAONA WABONGO MNGEJAA NA KUCANCEL SHIFT. LKN MAMBO YA NCHI YENU MNAYADHARAU, TUTAFIKA KWELI, THAT IS A VERY SMALL NUMBER OF TANZANIANS IN B'GHAM. HAYA TWENDE
ReplyDeleteWe Anonymous wa Oct 05,02:57:00AM macho yako ni mazima kweli? ebu tumuombe Michuzi atuwee hiyo picha ya Canada uone kama shati ndio lenyewe. Huyu jamaa hayo mashati anayo mengi sana sijawahi kumuona karudia shati toka yupo Ikulu.
ReplyDeleteAcha wivu wewe
Mon Oct 04, 11:47:00 PM uliyeandika, "na hao waliosoma na kina Chelsea Clinton na kina Prince Harry watasemaje ?"
ReplyDeleteWaache waseme! Kwa nini unakuwa msemaji wa hao wa Amerika ana Uingereza!
Wewe ndiwe uache UTUMBO!
Balozi na nyie wa B'ham, mliitana wa mtaa wa saba tu au nini? Mbona wengine siwaoni hapo na wapo hapo miaka mingi sana!
ReplyDelete