Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina (kulia) akikabidhi kikombe cha ushindi wa jumla kwa timu ya Intergrator iliyoibuka kidedea katika michezo mingi iliyofanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Michezo ya benki hiyo katika Viwanja vya Leaders, Dar es Salaam juzi.
Mchezaji wa mpira wa wavu wa timu ya Intergrator, Stanley Magulya akiruka kurudisha mpira wakati wa mchezo wa fainali dhidi ya timu ya Barclays Premier Life, katika maadhimisho ya Siku ya Michezo ya Benki ya Barclays kwenye Viwanja vya Leaders, Dar es Salaam juzi. Intergrator ilishinmda kwa seti 2-1.
Mchezaji wa timu ya netiboli ya Barclays Premier League, Wema Allan (katikati) akichuana na wachezaji wa timu ya Junior Eagle, katika maadhimisho ya Siku ya Michezo ya Benki ya Barclays kwenye Viwanja vya Leaders, Dar es Salaam juzi. Junior Eagle ilishinda.
Mchezaji wa timu ya soka ya Barclays Premier Life, Issa Omari (katikati) akichuana na wachzaji wa Scheme Loan, Denis Mwaruwanda na Tito Kisanga (kulia) katika maadhimisho ya Siku ya Michezo ya Benki ya Barclays kwenye Viwanja vya Leaders, Dar es Salaam juzi. Premier ilishinda kwa 1-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Jamanieh kwani SUMO ilishindaniwa pia?kama hapana niambieni hiyo picha ya kwanza huyo mchezaji anayepokea kombe alishinda mchezo gani...

    Mdau Istanbul

    ReplyDelete
  2. huyu naye anacheza mpira na lakuchumpa
    alafu anajidanganya anaupenda mpira.
    na sio kama hana pesa za vifaa.
    mambo mengine aaaah zinatoka tu.

    ReplyDelete
  3. ha ha haaaa, mdau wa istanbul mbavu zangu zinauma sana, umewaza nini ati sumo ilishindaniwa pia? kwi kwi kwiiiiiiiii

    ReplyDelete
  4. Issa Sekatawa, mido langu Mwenge Shooting kitambo!

    ReplyDelete
  5. hongera sana barclays Bank(T) kwa kushirikisha michezo mingine maarufu kama Volleyball, japo haina maendeleo kitaifa.safi sana.

    ReplyDelete
  6. Somesheni watoto shule nyie taifa liwe na wasomi mpaka vijijini. Na tusio tunajenge taifa la hewani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...