Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akiwaonyesha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa mataifa, Benki ya Dunia na washirika wa Maendeleo kitabu chenye taarifa za awali za utafiti wa Afya ya uzazi na mtoto ya mwaka 2010 leo jijini Dar es salaam .Wengine ni Mganga mkuu wa Serikali Dkt. Deo Mutasiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akipitia kitabu chenye taarifa za awali za utafiti wa Afya ya uzazi na mtoto ya mwaka 2010 leo jijini Dar es salaam.Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) nchini Dkt. Julitta Onabanjo , Mganga mkuu wa Serikali Dkt. Deo Mutasiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (kushoto).Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

=========================

Na Mary Kweka,Dar Es Salaam.

TAARIFA ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa 2009/10 imebaini kuwa vifo vya akina Mama vitokanavyo na uzazi na watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano vimepungua kwa kiwango kikubwa.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi Blandina Nyoni wakati alipokuwa akizindua taarifa za awali za utafiti wa afya ya uzazi na mtoto Jijini Da Es Salaam.

Bi Nyoni alisema takwimu zinaonyesha kuwa katikati ya miaka ya tisini vifo vya watoto wadogo chini ya miaka mitano vimepungua kwa asilimia 40 kutoka vifo 137 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai hadi vifo 81 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai kwenye kipindi cha miaka ya 2006-2010.

Aidha alisema kwa upande wa vifo vya akina Mama vinavyotokana na matatizo ya uzazi vimepunua kwa asilimia 21, hii ni kutoka vifo 578 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa hai kwa kipindi cha mwaka 2004-05 hadi vifo 454 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa hai kwa mwaka 2009-2010.

“Katika hatua hii pamoja na kuonekana kuwa Tanzania tumepunguza vifo vya watoto ambavyo ni lengo la nne la maendeleo ya milenia jitihada zinahitajiaka zaidi kufikia lengo namba tano la milenia ambalo linasisitiza kuboresha afya ya uzazi”alisema Bi Nyoni.

Pamoja na mafanikio hayo, Bi. Nyoni alisema mfumo wa ukasanyaji takwimu za Afya bado unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo jinsi ya kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi kwa kuboresha huduma kwa akina Mama wajawazito na huduma ya afya.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, changamoto nyingine ni pamoja na kupunguza vifo vya watoto wadogo, mijini na vijijini ili kuhakikisha kuwa watotowote hawapotezi maisha utotoni.

Alitoa wito kwa kuwaomba wadau wote hasa wale wanaoisaidia sekta ya afya kutumia kwa ukamilifu taarifa zinazotokana na utafiti huu wa Afya ya uzazi na mtoto kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

Pia Bi. Nyoni ameihimiza jamii kutumia takwimu hizo kwa ajili ya mipango bora na utekelezaji wa programu mbalimbali za afya katika ngazi zote za utawala kwa ajili ya mipango ya maendeleo ili kuboresha maisha ya watanzania wote.

Utafiti huu umefanywa na kuandaliwa na kikundi cha wataalamu wakiwemo Tanzania and Demographic and Health Survey Technical Working Group, wakishirikiana na Wizara ya Afya, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Wafanyakazi wa Serikali katika ngazi mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hafadhali, make nilisoma hii habari kwenye New York Times kuwa Tanzania inaongoza kwa vifo vya watoto na akina Mama wajawazito Africa nzima. Sababu ni "Infection Control" na uzembe wanaowafanywa kwa Madakitari na Manesi wakati mama anapokuja kwenye chumba cha uzazi. Hii habari ilinisikitisha sana. Na hii huwa wanafanya hivi endapo kama Mama Mjamzito hajatoa chochote ili apate huduma nzuri. Hii nimeishuhudia sana pale Muhimbili na Amana. Mgonjwa akiandikiwa kuongezewa maji, nesi anaenda kwenye hand bag yake kutoa maji ili amuulizie mgonjwa. Na manesi huwa hawanawi mikono mgonjwa hadi mgonjwa. KCMC wanaunafuu kidogo kwa sababu wauguzi wao mara nyingi wanaletwa hapa DUKE HOSPITAL - USA kufundishwa baadhi ya vitu kuhusu na namna ya kutoa huduma kwa mgonjwa kama ulivyofundishwa.

    Tukemee na kutokomeza uzembe kazini. Tuwe kama NIGHTINGALE"

    Mdau- ENGENDER HEALTH CARE INTERNATIONAL -NEW YORK, USA

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha sana...Bado tuna safari refu..Tufurahie pale tutakapo kua na single number au 0 number...Ndio maana Tanzania kufanya baby shower ni mwiko ati unachuria. kwa vile mtoto kuzaliwa hai au mtoto kuzaliwa haoi ni kama bahati vile.

    ReplyDelete
  3. Idadi ni kubwa kuliko miaka ya 6O, nakumbuka mama yangu alijifungulia kwenye basi ambulance ilikuja kumchukuwa kituoni akasema hiyo miaka imepita sasa ni shida, hakuna anedhamini wakina mama wajwazito. Wakina mama wengi wanjifunguwa bila Dr kuwa karibu, na hilo ni tatizo kubwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...