Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wa Kijiji cha Masai Kata ya Seng’wa Wilaya ta Maswa Mkoa wa Shinynga, wakati alipowasili kijijini hapo leo mchana kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Robert Simon Kasena leo
Wasanii wa kikundi cha ngoma ya asili cha Bugayangi cha Kijiji cha Ngongo Wilaya ya Maswa, wakicheza na nyoka wakati wa mapokezi ya mgombea mwenza wa urais wa CCM Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Masai kufanya mkutano wa kampeni leo
Mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimshikia kipaza sauti na kumuombea kura mgombea udiwani wa Kata ya Seng’wa Jimbo la Maswa Magharibi, Elizabeth Sangalali, ambaye anasumbuliwa na maradhi, wakati alipofanya mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Masai leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...