Home
Unlabelled
January makamba na vijana wa bumbuli
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hivi ni mie tu au kaka january anamwiga JK kutoa hoja??? au na yeye mbeleni atagombea uraisi nini?
ReplyDeletewadau?
Sijui Watanzania wenzangu mnaelewa nini kutokana na mazungumzo haya. Mazungumzo haya yanaonyesha kitu kimoja kikubwa kwangu:
ReplyDeleteJanuary na hao waomba pesa ni matabaka 2 tofauti kabisa. Waomba pesa priority yao na ambayo ni urgent kwao ni kula kwanza. Pengine hawakula usiku jana yake. Pengine hawajui watakula nini mchana.... Kwa hiyo Sh 500 ina maana kubwa sana kwao. Ukiwa na njaa huwezi kufikiria barabara kujengwa, au shule au nafasi ya kazi...la asha. Utafikiria kushiba kwanza halafu ndio ujenzi wa barabara kufuata.
Lakini kwa vile January alikunywa chai asubuhi hiyo na ameshiba anashindwa kuelewa kwa nini mtu anamwomba Sh 500. Kwa hiyo wako katika matabaka 2 tofauti.
Hata hivyo namuunga mkono January kwa kukataa kutoa hiyo Sh 500 lakini nina pointi kwamba wanasiasa kwanza waweke mazingira ambayo yatawawezesha watu kukidhi mahitaji yao ya msingi kwanza kama vile chakula, maji, malazi na mavazi kabla ya kuanza kuongelea mambo makubwa ya maendeleo kama vile barabara, shule nk nk. Mtu mwenye njaa hawezi kukuelewa unapoaongelea fursa. Kwanza ashibe ndio mtaanza kuongelea fursa na mkaelewana. Changamto kwenu wanasiasa ni kuweka mazingira sahihi ya Watanzania kuweza kujitafutia mahitaji yao wenyewe kwanza bila kuombaomba.
Hongera kijana January umekuwa mfano wa kuigwa,wanasiasa wengine wawe wakweli wanapokutana na wapigakura kama wewe.Ni kweli kabisa huwezi kumpa kila mtu jimboni shilingi 500 kila siku,na kwakweli wapiga kura wamezoezwa vibaya
ReplyDeleteKalikali wewe una ubongo mzuri katika kuchambua mambo.
ReplyDeleteLakini kwa taarifa yako tu wanasiasa haswa watawala wanajua sana hili. Kama mtu mwenye njaa hawezi kufikiri basi ni rahisi sana kumdanganya, yeye kila unalosema anapokea tu bila kufikiria faida na hasara zake. Mtu kama huyu ni rahisi sana kuendelea kumtawala. Hivyo ili uendelea kumtawala lazima uhakikishe ashibi kama wewe.
hahahah nimeikubali. Lakini kaka ungewaacha kidogo nina uhakika ulikuwa unayo hela mfukoni. Wamezoeshwa mshiko sasa mbunge mpya ukileta za marekani za misimamo huko Bumbuli utapigwa chini kwasababu washazoea.
ReplyDeleteHii mi naona kasumba tu, hawa jamaa ukiwapiga sachi wana zaidi ya 500/= mifukoni na chai wamekunywa, ila usanii tu akipita mgombea wa chama kingine pia wataomba 500/= vilevile, Bongo Bwana unafikiria ya leo tu, kesho mmmh. Saafi sana January hii ndio inatakiwa labda wataacha usanii waanze kufanya vitu vya maana.
ReplyDeleteUpinzani watapata kuongoza mwaka 2060!
ReplyDeleteJANUARI,
ReplyDeleteYour answer is so legit, or correct, but so incomprehensible to these folks. Unawarushia mpira watu ambao hawajatatua tatizo la msingi (njaa)?
CCM mnafanana. Mimi ningekuwa na muda, ningewaweka chemba hata dakika zaidi ya 5-10 kuulizia mazingira gani wanatoka, shughuli zao ni nini nk. Jaribu kuwapa mawazo ya msingi kwanza ambayo ni mepesi na siyo ya jumlajumla kama unavyowajibu.
Kwa mtindo huo viongozi wa ccm hamtakuwa mnaleta chochote kipya. Wape darasa ambalo wanaridhika na kulifurahia. Lakini hapo umewajibu upesi na hawajui wanakula nini. Ungekuwa hujala makamba ungezungumzia swala la fursa? Kwanza neno FURSA tu bado ni gumu, si wengi wanakuelewa kwa undani FURSA maana yake nini.