JK akiwasalimia wananchi wa Bugando alipowasili kwenye mkutano wa kampeni Nkome Wilayani Geita leo.

JK akisalimiana na maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye mapokezi yake kijijini Nkome leo

JK akipokea bendera ya CHADEMA, kutoka kwa mwenyekiti wa Wanawake wa chama hicho jimbo la Kwimba, Monika Jimotoli mara baada ya kutangaza kukihama chama hicho kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jimboni humo. Monika amehama chama hicho na wenzake 18.

Maelfu ya wananchi wa Nkome wakimshangilia JK alipokuwa anahutubia mkutano mkubwa wa kampeni leo Nkome.

**** **** **** ****

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM,Mheshimiwa Jakaya Kikwete amewasihi wananchi wa Sumve leo kuchagua CCM kwani hakuna Chama kama CCM kwa ubora wa sera, utekelezaji wa sera na mipango na jitihada za kuleta maendeleo kwa watanzania.

Japo Tanzania bado ni nchi maskini, alieleza Tanzania ya mwaka 1961 na ya sasa sio sawa. “Lakini cha msingi ni kwamba yale tuliyoyaahidi tutayafanya, tumeyatekeleza” alieleza Mgombea Urais wa CCM, Mheshimiwa Kikwete kwenye mkutano huo wa kampeni.

Kwa upande wa elimu, Mheshimiwa Kikwete alisema serikali ya CCM imekabiliana na changamoto kuu nne zilizojitokeza baada ya upanuzi mkubwa wa elimu nchi nzima.

Changamoto zilizopatiwa ufumbuzi ni ile ya upungufu wa walimu ambapo kila kata kuanzia mwakani itapata walimu wa tano. Changamoto ya nyumba za walimu zitajengwa za kutosha kwa sababu bajeti ya elimu imeongezwa mara tatu zaidi kukabiliana na tatizo hilo.

Na tatu ni changamoto ya vitabu vya sekondari ambapo Mheshimiwa Kikwete alieleza mipango imefanywa kushirikiana na Serikali ya Marekani ambapo wamesaidia kuchapisha vitabu vya sayansi vya sekondari. “Kwa hivyo kuanzia mwakani, watoto wetu wa masomo ya sayansi watakuwa na vitabu vya kutosha kwenye shule zote nchi nzima” alieleza Mheshimiwa Kikwete.

Kwa upande wa huduma ya afya, Mheshimiwa Kikwete alieleza mikakati ya serikali ya CCM kupambana na maradhi makubwa kama Malaria, UKIMWI na kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake. Kwa kansa ya shingo ya uzazi, Mheshimiwa Kikwete alieleza kwamba kuanzia mwakani wanawake wote wenye umri wa kupata chanjo hiyo watachanjwa bure ili kukabiliana na gonjwa hilo sugu nchini.

Kwenye mikutano hiyo miwili pia Mheshimiwa Kikwete alieleza kuwa CCM iliahidi kuboresha utoaji huduma ya maji ili kufikia asilimia 60 vijijini na asilimia 90 mijini. Mheshimiwa Kikwete alieleza kwenye wilaya ya Kwimba, utoaji huduma ya maji kwa sasa umefikia asilimia 55.5, na bado jitihada madhubuti zinaendelea kuboresha hali hiyo.

Mheshimiwa Kikwete alieleza kuwa kwa msaada wa marafiki wa Tanzania wa maendeleo, vijiji kumi na mbili vya wilaya ya Kwimba vitapatiwa huduma ya maji kwenye mpango mkubwa wa usambazaji wa maji nchini unaodhaminiwa na benki ya dunia.

Kwa upande wa kilimo, Mheshimiwa Kikwete alielezea mpango mkubwa wa kilimo kwanza ambao unalenga kwenye kuboresha mambo makuu manane ambapo yatamsaidia mkulima kupata faida kwa kilimo chenye tija ikiwemo upatikanaji wa ruzuku na utafutaji masoko kwa ajili ya mazao ya wakulima.

Mheshimiwa Kikwete alieleza wakazi wa wilaya hii pia kwamba ilani ya CCM kwa mwaka 2010 – 2015 inaelekeza kipaumbele kwenye uvuvi wa samaki na kuendeleza sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya wakulima.

Na kwenye mkutano wa kampeni huko Ngudu, aliyekuwa Mwenyekiti wa wanawake Chadema Wilayani Kwimba Mama Monica Jimotolo, amerudisha kadi ya chama hicho na kuingia rasmi CCM.

Mama Jimotolo alieleza sababu kuu iliyomfanya kuingia CCM ni kuchoshwa kwake na siasa za chuki na uchochezi ambazo zinalenga kuvunja amani na mshikamano wa nchi yetu.

Alieleza hadhara hiyo kuwa baada ya kufanya uamuzi huo, wengine kumi na saba wameongozana naye na kusema chama hicho kimekufa wilayani hapo. Wanachama hao walikaribishwa na Mwenyekiti wa CCM taifa na kupewa kadi za Chama Cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Kikwete aliwanadi wagombea udiwani na ubunge wa Chama Cha Mapinduzi. Aliwasihi wananchi wa Kwimba kupanga jozi iliyokamilika ya CCM ili kuleta maendeleo. Alitoa mfano wa kilimo cha punda na ng’ombe kwa kueleza kuwa unapoamua kulima utumie jozi ya punda au ya ng’ombe, lakini huwezi kuchanganya kwa kulima na ng’ombe na punda kwani punda atakapopiga mluzi, ng’ombe atasimama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Huyo alihama mbona mwanaume halafu Michuzi umwita Mwenyekiti wa Wanawake. Huko CHADEMA Wenyeviti wa Wanawake ni wanaume? WanaCHADEMA nipeni ufafanuzi.

    ReplyDelete
  2. Binafsi nimekosa haki ya kupiga kura kwa kuwa mbali na nchi yangu ila yote maisha.Wa TZ mumpigie kura Jakaya kwa kuwa ni chaguo la Mungu kama lilivyosema Kanisa,kikawaida chaguo la Mungu linakoma pale tu asipogombea.

    Tusiwe vigeugeu tusikilize kauli ya kanisa ya 2005 ya chaguo la Mungu.

    ZAUNUNU-AMSTERDAM

    ReplyDelete
  3. kikwete ndio rais wetu...oyeee kikwete..ccm oyeee

    ReplyDelete
  4. RAS JOB HAPA.

    TZ NI YETU SISI NI WATANZANIA TUPEANE UKWELI WADAU, NAMPENDA JK RICHA YA URAISI, ANAUWEZO NA NAJUA KWA SASA ANAHAMU YA KUFANYA NINI TZ, HUYU JAMAA SI MJINGA, WADAU WALE MAFISADI KWA NINI HAWAMSINDIKIZI HUYU JK, TATIZO NINI, KAKA JK UPO FITI KTK SOLUTION ZOTE, ENDELEA BRO, POLICE WANANYUMBA FRESH MBONA HUWAAMBII WATU, MUHIMBILI YA SASA MAFISADI KUWEKWA KIDOGO KEKO, UNAPENDEZA KIMATAIFA, HUPIGANI NA WANAOKUBEZA UNAWAHESHIMU(MFANO MJOMBA NYIMBO ZAKE, ZAMANI MASOUD KIPANYA ALIJARIBU AKAWA MPOLE GAFLA UNADHANI TULIKUWA HATUJUI, CV YAKO JK IPO OPEN KWA ANAYEIPENDA NCHI, NA NI BABA MWENYE UWEZO AMBAE ANAJUA WAJIBU WAKE, JK ILI UPATE NAFASI MBINGUNI WAWEKEE WATANZANIA MTU WAO MAANA BARABARA KAJENGA,NYUMBA NA MAKAZI KABORESHA HAKUNA SWALI UVUVI KASUMBULIWA ILA KAZUIA NET KUVULIA NA KUWAELEWESHA WAVUVI WASIOELEWA,MAKUFULI WAZIRI MKUUUUUU HILO NI OMBI BINAFSI WADAU, MNISAPOTI JAMANI, TZ SISI TUNATAKA TUAMBIWE UNATAKA KUFANYA NINI ILI IWE NINI NDIO TATIZO,MTUSAIDIE WAZEE POLE NA TATIZO LA KUBADILISHA WAZILI MKUU KATIKA KIPINDI CHAKO, ILA UKO SAFI SANA MAPUNGUFU NI KAWAIDA KWA WOTE MUNGU AKUSAIDIE AFYA NJEMA POLE NA UCHOVU KAKA, KITI UNAKIJUA TUNAOMBA USICHOKE, MANENO NAJUA SIO ISHU KWAKO, UMEBORESHA CCM HATA MIMI NINAHAMU YA KUJIUNGA, MUNGAI USIWE MBISHI ULIHARIBU ELIMU PUMZIKA VIJANA WAINGIE, MAKUFULI AKIKATAA INGAWA NAJUA HAKATAI KAZI YULE, BASI MPE SAMWEL SITA SSPEED KATULIA MZEE. AHSANTE JK. Ras JOB wa IR.

    ReplyDelete
  5. nimefuatilia sana comment za zaununu humu. Am sorry to say ni mdini na mp....vu.

    ReplyDelete
  6. Wewe unaejiita Zaununu ni muongo sana,aliyesema maneno haya ni nani?
    "Mimi si mwana CCM ila kura yangu nitaitoa kwa Jahkaya na huyu yakhe maana ndio viongozi haswa....." Sasa hapo juu tena unasema umekosa haki ya kupiga kura!!!Upige usipige sie haitusaidii kitu.

    ReplyDelete
  7. huyo ni mwanamke ndugu yangu. Anaitwa Monica. Au kwa sababu amekata nywele kimtindo? That is a Real African Beauty Woman. haitaji artificial hair kama ulivyozoea.
    Mwisho JK ndio chagua langu.2005 wakuu wa madhehebu ya dini walisema ni chaguo la Mungu, je safari hii Mungu kawaambia kuwa sio chaguo lake? Na kuwa kaleta chaguo jingine wakati chaguo la awali bado lipo?viongozi wa dini angalieni kauli zenu mtabaki makanisani peke yenu kama ilivyo ulaya.

    ReplyDelete
  8. Mwenye masikio na asikie:

    CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

    Lakini mwaka 2060, ng'atukeni muwapishe wapinzani, kama wapo!

    ReplyDelete
  9. Zaununu mtafute Kabila akupakate labda hayo mashetani nanihii yatakutoka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...