
MBUNIFU wa kimataifa wa kitanzania, Rosemary Kokuhilwa Rwechungura ameandaa onyesho maalum nchini Marekani ambalo litafanyika Ijumaa hii kwa ajili ya kuchangia mradi wa watu wasiosoma wa Bisila Bokoko.
Rose mwanamitindo ambaye alitokea kampuni ya Face International iliyokuwa chini ya marehemu Amina Mongi, kwa sasa anaishi Marekani akimiliki kampuni yake iitwayo FASHIONJUNKII ambapo pia anaendesha Blog inayohusisha mambo ya mitindo na urembo.
Akizungumza kutoka Marekani, Kokuhilwa alisema hili ni onyesho la kwanza kuandaliwa na FashionJunkii likihusisha wabunifu na wanamitindo mbalimbali kutoka pande mbalimbali duniani.
“Kutakuwa na wabunifu nane ambao ni maarufu duniani, wataonyesha nguo ambapo pia kutakuwa na zaidi ya wanamitindo 36 kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya onyesho hilo litakalofanyika Chuo cha Teknolojia ya Mitindo (FIT),” alisema.
Aliwataja wabunifu watakaoonyesha mavazi yao ni pamoja na
MATAANO, Amparo Chorda, Louda Collection, African Mosaique, Thula Sindi, David Tlale, Nike Kondakis, and Prajjé Couture.
Alisema onyesho hilo mbali na kuwapa waalikwa nafasi ya kuona utamaduni wa sehemu mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani, onyesho hilo pia litasaidia kuwakutanisha watu mbalimbali maarufu ambao wako kwenye fani ya mitindo kwa muda mrefu.
“Onyesho hili litasaidia pia waalikwa kuona mavazi ambayo mengi yao hayaweza kuonekana.”
Kokuhilwa alisema onyesho hili ni la kwanza kwa ajili ya kusaidia jamii na kwamba wanatarajia kulifanya kila mwaka kwa kushirikisha wadau mbalimbali.
mbona hamjaweka nguo zake tuone zikoje? manake mi naishi marekani ila bado sijawahi kumwona huyu dada, ila congrats, tuonyeshe na sie tuige mfano.
ReplyDeleteWakuu,
ReplyDeleteTunashukuru sana kwa kutuhabarisha. Tunaomba matangazo ya namna hii yaweke bayana ni wapi onyesho hilo litafanyaka.Ukisema "antikisa Marekani" pekeyake haitoshi kwani ni kubwa sana. Akiondoka mtu DC kwenda Amsterdam anatangulia kufika (masaa 8) kuliko mtoka DC kuelekea Honalulu Hwaii(msaa 10). Hata ukitaja chuo kikuu cha mitindo bado haitoshi maana uki-google vyuo vikuu vinavyofundisha mitindo Marekani utapata utitiri wa vyuo. Tupo tayari kuchangia ila tunaomba mtusaidie anuani ili tuwasaidie wenzetu kule nyumbani
Ok Kaka Michuzi, huyu dada namfahamu mtafutaji sana na anaipenda fani yake. Lakini yeye sio mbunifu yeye ni stylist wa ma stars na watu wenye hela zao Marekani. Nakuvaa anajua sana huyu.Hata ukienda kwenye fashionjunkii utaona amesema yeye ni stylist na make up artist lakini sio blogger. Sisi tunamwita FJ wapenda fani yake. sasa ubunifu naona kama mnamislead waungwana humu blogini. Lakini hata hivyo bado yuko juu sana tuu na maringo hana yeye huwa anamind ya kwake sio wengine kutwa kwenye sahani za watu wataka chovya. DC sio mbali achamie niende NY nikafute ukoko machoni. FJ wa wa wa!
ReplyDeleteNi kweli we mdau wa hapo juu!Nami m curious to see her work..maana tangu aanze sijawahi kuona akionyesha or akiadvert kokote?tuonyeshe basi what you got na sio maelezo mengi hata contact hakuna..
ReplyDeleteeeh hivi ni mbunifu wa kimataifa? nilikuwa sijui attii..jamani wapi nitaona hayo mavazi aliyobuni?
ReplyDeleteIt was nice talking to u the other day. Keep it up and I'm so proud of you.
ReplyDeletesio mbunifu ni STYLIST/MAKE UP ARISTS wa models na watu binafsi wenye hela zao marekani. She is a former model her self, naona umemislead watu kaka michuzi. tembelea www.fashionjunkii.onsugar.com utamuona
ReplyDeleteNadhani FTI wanamaanisha Fashion Institute of Technology hapa Downtown Manhattan,New York.Mwaandishi ameandika kiushabiki na kushindwa kuhighlight vitu muhimu kama place,venue,time,cover fee etc.
ReplyDeletehahahahha wabongo jamani kupeana sifa kusipo stahili. subiri msifiwe sio kujiweka upwani kutafuta kusifiwa kwa nguvu. huyo millen kwanza sio supamodo . na huyo rosemary ndio mbunifu wa nini hamtuambii na ni yupi kati ya hapo?. na huyo grace ndo nani na yupi kati ya hao? nifahamisheni wadau basi nipo mbali naona wadada tu natoka mate siwatambui.
ReplyDeletekujitangaza kinguvu. lmao
ReplyDeletembunifu wa mastaa gani? name one itasaidia
ReplyDelete