Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro (Pichani)amesema wanawake ni hazina na bila kumkomboa mwanamke basi maendeleo yatakuwa ndoto.

Akiwa mjini Nairobi katika uzinduzi wa muongo wa wanawake barani Afrika Asha Rose amesema Umoja wa Mataifa uko msitari wa mbele kusaidia ukombozi wa mwanamke barani Afrika.

Akizungumza na mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Irene Mwakesi amesisitiza haja ya viongozi wa Afrika kutoa fursa zaidi ya kuwawezesha wanawake ili kusaidia kizazi hiki na kijacho.

Binafsi amesema kama mama, mke na mwenye wadhifa wa ngazi ya juu duniani anajituma na anaamini kila mwanamke anaweza kuwa kama yeye hata zaidi ya yeye. Msikilize akinena na Irene.

kusikiliza moja kwa moja mahojiano hayo ingia http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/detail/114574.html au
http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/ na
http://www.facebook.com/UNRadioKis na kama una swali waandikie
nducha@un.org na kariukia@un.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mi ananifurahisha huyu dada asivyoishi kwa dawa ya nwyele.

    Nwele zake nzuri zaidi ya watia dawa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...