Ankal Michu,
Pole kwa kazi ngumu.

Naomba msaada tutani,kukaa kwa ndugu kume expire; Natafuta nyumba (self Contained) chumba kimoja maeneo ya Mbezi Beach,Kunduchi, Kawe, Masaki, Hoysterbay na Mikocheni.

Hasa servants quarter inayojitegemea , ili mradi liwe ndani ya geti. Hii ni kwa ajili ya mtu mmoja asiye na watoto na anayependa privacy. Ntashukuru iwapo tutawasiliana kupitia barua pepe kwa maelezo zaidi

Asante ,
Mtiifu
jbinagi@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. katika maeneo yote aliyotaja utapata kawe tu one bedroom oysterbay ?

    ReplyDelete
  2. JIELEZE KWANZA WW MWANAMKE AU MWANAUME NA UMRI WAKO NA AJIRA YAKO.BY THE WAY PRIVECE UMEJIFUNZIA WAPI NA WEWE NDIO UNANZA MAISHA.

    ReplyDelete
  3. Jamani Mabinti tuwafungie kwenye mageti na watu wazima wanjifungia wao wenyewe. Kuna nini kwenye maisha?Tunaficha kitu gani yani tunakuwa wafungwa sisi wenyewe.

    ReplyDelete
  4. Mume Wangu, Mikocheni bOctober 06, 2010

    Toa maelezo zaidi yanayokuhusu ili kunitoa wasiwasi kabla sijajaribu kukupangisha "servant quarter" yangu niliyonayo hapa Mikocheni karibu na Cine Club:
    Je unafanya kazi,wapi?/Unasoma wapi?
    Jinsia yako, Umri wako
    Wadhamini wako
    Uko tayari kuchukuliwa alama za vidole?
    Muda unaotaka kupanga.
    Uko tayari kutoa kodi ya miaka miwili au mitatu?
    Maswali na maelezo yote hayo ni muhimu na ni kwa nia njema tu hasa katika enzi hizi za utandawazi. Ni lazima kila mmoja wetu ajiridhishe kuwa usalama wake hauna shaka.

    ReplyDelete
  5. Hoysterbay Labda unaweza kupata, maaana ipo Maswa vijijini.

    ReplyDelete
  6. Massoud Mitindo, UpangaOctober 06, 2010

    Wewe hunifai, nina wasiwasi na watoto wangu wa kike utawalaghai tu na chipsi na vijizawadi vya lambalamba

    ReplyDelete
  7. Jibaba, OysterbayOctober 06, 2010

    Je una silaha yoyote unayoimiliki kihalali au isivyo halali??
    Una rekodi yoyote na vijana wa IGP Mwema?
    Watoto huna, je Mume, Mke au Hawara??
    Huwa unakunywa pombe za kupitiliza( mlevi usiye mstaarabu)??

    ReplyDelete
  8. Matari, MafiaOctober 06, 2010

    Anza kujenga kibanda chako, hayo maeneo unayotaka watakushitukia.
    SIKU HIZI ASKARI KANZU NI WENGI, UTAKAMATWA BAADA YA SIKU MBILI TU.

    ReplyDelete
  9. yaani wewe mie nitajaribu kukupangisha. kuna jibaba fulani hapa mjinga sana, limenichosha kuchungulia mke wangu hadi akikojoa mimacho hiyo, wabongo bwana hawana wema hata siku moja

    ReplyDelete
  10. heee manyanyaso sasa ayo dah,bora tujenge vibanda vyetu tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...