Na Mwandishi Wetu.

CHAMA cha Msalaba Mwekundu Nchini,(Tanzania Red cross Society-Red Cross) kupitia kikosi chake maalum cha Uokoaji na Maafa mkoa wa Dar es Salaam (Action Team) kimejipanga vyema kuhakikisha kinatoa huduma ya kwanza na ya dharura kwa kiwango cha juu siku ya Oktoba 31,wakati wa uchaguzi mkuu.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Red cross Mkoa wa Dar es Salaam, Mayasa Mikidadi muda mfupi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi wapya wa kikosi hicho.

Mayasa alisema kuwa Red Cross imejiandaa vya kutosha kutoa huduma ya kwanza na ya dharura wakati siku ya kupiga kura na matatizo yote ya dharura. “Ni hakika kazi iliyopo mbele yetu ni ngumu, lakini hakikika uwezo tunao na tutaifanya kwa nguvu zote ilikuakikisha kila mtanzania anapata haki ya kupiga kwa usalama kura zake” alisema Mayasa.

Aliendelea kusema kuwa, kikosi hicho kitafanya shughuli za uokoji siku hiyo ambazo zikiwalenga watu watakao kuwa wamezidiwa katika foleni, wagonjwa pamoja na kuwasaidia walemavu wa aina yote kusaidiwa kwa lolote litakalotokea wakati wa upigaji wa kura hizo.

Aidha, katika uchaguzi huo, ambao awali viongizi hao walikuwa kwa muda kwa kipindi cha miaka kadhaa, waliweza kujiuzuru na kupisha uongozi mpya ambao ulifanywa kwa njia ya amani huku wakichaguana kwa kanuni ya kupiga kura.

Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni pamoja na: Dk. Suphian Juma (Kamanda Mkuu), Feruzi Mpili (Kamanda Msaidizi) huku nafasi ya Katibu ikichukulkiwa na Amina Mwalimu.

Uongozi huo mpya ulishukuru kwa kuchaguliwa kwao kutokana na kuwa na imani nao huku na kuaidi kushirikiana nao bega kwa bega na wanachama wa matawi yote mkoa.

Kwa upande wake, Kamanda mpya, Dk Suphian aliwashukuru wanachama wote kwa kumchagua huku akiwataka kila mwanachama kushirikiana bega kwa bega ilikufanikisha uongozi makini. “Naomba ushirikiano na kila mmoja ilikukijenga kikosi kwa hali ya juu na kuwa cha mfano wa kuigwa” alisema Dk. Suphian.

Katika uchaguzi huo ambao pia ulisimamiwa na Mratibu mkoa wa chama hicho, Grace Mawala, pamoja na Mwenyekiti wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Mambo ambao wote kwa pamoja waliwataka wanachama kuakikisha wanashirikiana na uongozi mpya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwani ni nini kitatokea mpaka hao Red Cross watoe huduma ya kwanza siku ya uchaguzi??????? mbona mnaanza kututisha Wantazania!!

    ReplyDelete
  2. We mdau hapo juu acha utoto wako wa kizamani wa Red Cross ni wanyonya damu ama wakwapo ujue kunavita.
    hao jamaa kazi yao ni kuangalia na kusimamia dhara lolote linaloweza kutokea kwa mpiga kura na kuwahi kulitibia kwani mwaka huu 2010 wengi watapiga kura hivyo foleni zitakuwa ndefu kuna kuanguka kwa kuzidiwa na uchovu n.k

    Kwani huendagi mpirani?

    ReplyDelete
  3. Haya bwana nimekupata mdau hapo juu na nitaacha utoto wa kizamani!!! lkn mamtoni huwa hatufanyi hivyo unaweza kupiga kura hata ktk simu yako au cp!!!technology imekuwa jamani tubadilike!!sorry mt wg km bado unapigwa na jua la bongo!!kila la kheri ktk uchaguzi huo!!! lol!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...