Mwisho Mwampamba akipokea shada la maua kutoka kwa ndugu zake mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jana jioni akitokea Afrika kusini kwa ndege ya shirika la ndege la SAA ambako alishiriki shindano la BigBrother Africa na kushika nafasi ya tatu huku mshiriki Uti kutoka Nigeria akijinyakulia kitita cha Dola laki mbili za Kimarekani.
Leo Mwisho anatarajiwa kutembelea vyombo mbalimbali vya habari na kueleza mambo mbalimbali yaliyojiri kwa muda wote wa miezi mitatu walipokuwa kwenye jumba la Bigbrother na washiriki wenzake na keshokutwa atazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika picha kushoto ni baba yake mzee Mwampamba.
Mwisho Mwampamba akisindikizwa na ndugu zake pamoja na walinzi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jioni ya leo akitokea nchini Afrika Kusini alikoshiriki katika shindano la BigBrother Africa Allstars na kushika nafasi ya tatu. Picha na John Bukuku.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. kashika nafasi ya 3 ama 4, hongera mwisho karibu nyumbani

    ReplyDelete
  2. Karibu home kijana wetu mwaya bado tunakupenda japo tungekupenda zaidi na dola 200,000 lakini yote maisha

    ReplyDelete
  3. correction mwisho alikuwa wa nne sio wa tatu. congrats

    ReplyDelete
  4. Mwisho alikuwa wa 4 si wa 3. Halafu baba yake ni Dr. Mwampamba na si mzee Mwampamba.Asante.

    ReplyDelete
  5. NAOMBA NIPATE UFAFANUZI NA UWELEWA,
    WA JUMBA HILI LA BBA HIVI TOKEA IMEANZA MIAKA 4 ILIYOPITA KWA MILA NA DESTURI ZETU TUNAJIFUNZA NINI NA TUMEJIFUNZA NINI? HIVI TUNAJINASIBU NA KUSHANGILIA KITU GANI? NA TUNAWAPA MAFUNZO GANI WATOTO WETU? NILISHINDWA KUSHANGAA MWAKA JANA RICH ALIKUWA NI MGENI RASMI NA KIVUTIO KULE DODOMA BUNGENI ALIKUWA ETI SHUJAA!! NI KWELI MAADILI MEMA?

    ReplyDelete
  6. Acheni kubwabwaja..Mwisho, Sheila na Lerato hawakupata kura za nchi yoyote..ikabidi watolewe basing on alphabetical order..

    ReplyDelete
  7. Let me take thisopportunity to explain to the anony anayetaka ufafanuzi abt BBA.
    Kwanza remember that programme ya BBA inaangaliwa Africa nzima na dunia kwa ujumla kwa kupitia TV na websites mbalimbali. So, through this Tanzania inatangazwa kwa hali ya juu. BBA huwa na tasks tofauti kila siku ya alhamis, na most of those tasks housemates huwa wanaongea masuala mbalimbali kuhusu Bara la Africa na specifically nchi wanazotoka.

    Pili, kuwekwa ndani ya nyumba kwa siku 90 ni njia mojawapo ya kuweza kuwasoma watu na tabia zao, culture zao. Piakuweza kuonyesha jinsi gani unaweza kuwa mvumilivu.

    Tatu, kushiriki BBA niexposure tosha. Ukitoka pale ni rahisi kupata kazi za contracts....ningi zikiwa kama acting, matangazo, kazi za jamii (act as an ambassador wa Multichoice katika masuala ya kutoa misaada kwa jamii).

    Nne na ya mwisho kwa leo, unadhani ukipata dola 200,000 si utakuwa umejikwamua kimaisha? Kwahiyo ni jambo la busara kujaribu bahati yako kwani hujui ngekewa itaangukia wapi.

    Asante.... kama utakuwa na maswali zaidi utaniambia through michuzi huyu huyu...ili nikufafanulie zaidi.


    Olivia.

    ReplyDelete
  8. Kwa anonymous unayetaka Mzee Mwampamba iwe Dr Mwampamba: Watu wengine bwana ulimbukeni tu unawasumbua. Kwani ukishakuwa Dr ndio jina lako linabadilika? Mie mwenyewe Dr lakini sipendi tabia ya Watanzania ya hata mkeo na watoto kukuita Dr. Yaani wagonjwa wakuite Dr na mkeo nae nyumbani akuite Dr!!! Dr ni title na wala si jina.

    Ulimbuke huu unafanya Watanzania wengine siku eti waitwa mathalani Mchumi John, Engineer John, Advocate John nk nk. Ukimwita mtu bila hicho kiambatanisho hupati huduma ati. Huu wote ulimbukeni tu.

    ReplyDelete
  9. Hao wote waliokuja kumpokea hawawezi kusukuma hilo tololi? au ni kwa ajili ya picha? yaani ndugu + rafiki zangu waje airport kunipokea halafu nibuluze toroli wakati nipo nao? haya mambo.......

    ReplyDelete
  10. hongera mwisho kwa kufika tano bora karibu nyumbani bado tunakupenda

    ReplyDelete
  11. we mdau hapo juu acha ukoloni, huo ni mchezo kama michezo mingine mshindi anaondoka na kitita, angekuwa mwanao karudi na hela usingeleta huu upupu wako humu!

    ReplyDelete
  12. ANON. Tarehe Thu Oct 21, 01:13:00 PM, We endelea kushangaa na kushindwa kuelewa, wenzako wanakunja vitita na wanaendeleza kazi/biashara au career zao. We endelea kutafuta maaadili na mpango mzima wa kujifunza!lol.

    ReplyDelete
  13. maadili maadili tumewachoka sasa hiki sio kipindi cha ujamaa, kaa na mkeo au mumeo na watoto wenu na hayo maadili yenu

    ReplyDelete
  14. Naungana na wewe Thu Oct 21, 01:13:00 PM: Sikujua la Rich kuitwa shujaa na kukaribishwa bungeni. Ni maajabu. Unajua hivi vitu vya kuiga dunia ya kwanza vinatupelekesha sana! Kwa kweli maisha wanayoishi mle ndani ya jumba iwe uk, netherlands na kwingineko kokote wanakofanya hii Big brother siyo ya kuigwa kabisa haswa na vijana wetu wanaokuwa, hivyo kwa kumkaribisha mtu atokae huko kama shujaa bungeni nadhani ni ukosefu wa busara. Kama media na entertainment industries they can do that cause in turn wanapata kumarket business zao, but not GOVERNMENT!

    ReplyDelete
  15. KARIBU KAKA MWISHOOOOO.SHEMEJIIIIIII ANAKUJA LINI AU ILIKUWA ZUGA TU??????????

    ReplyDelete
  16. Wewe Anon Thu Oct 21, 01:13:00 PM, kama unataka kujifunza kaangalie documentary. Kawambie shangazi zako wakufundisha mila na desturi siyo BBA. Sisi tunataka burudani, toka hapa na ushamba wako...Get a life, get a pedicure...whatever!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...