Boston(Spirit of America)Jana ilitowa onyo Kwa Stars United,Baada ya kuwapa Dozi ya Bao 4 – 2

Na ilikuwa iwe mbaya zaidi Kwa Meneja wao DJ Luca,Kwani Vijana wa Boston Hawakuweza kwenda na wachezaji wao Muhimu kama Makala Francis,Richard Mwandamane,na Golikipa wa kutegemewa ambaye alichezea Timu ya Jamhuri Pemba Salum Matambi

Boston ilianza kwa moto mkumbwa Baada ya dakika ya nne tu ya mchezo,mshambuliaji machachali Ramadhani Lenny alipanguwa ngome yote ya stars mpaka Kipa wao na kupachika Bao Maridadi

Stars nao wakasawazisha goli kwenye dakika ya 6 baadae, goli lilofungwa na Shaaban. Boston nao wakawaonyesha kuwa ni Moto wa kuotea Mbali Kwenye dakika ya 22 Baadaya kufunga stars goli lililofunga Na mchezaji machachari sana, Raheem Chomba,Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya ajabu na mpaka kuifanya timu ya Stars kupachika bao la kusawazisha mnamo dakika ya 47 ya mchezo kupitia mshambuliaji wake Shaaban,hata hivyo bao hilo halikudumu kwa muda mrefu Boston wakawabandika bao maridadi Bao lililofungwa na Frances kinyagoli.

Mechi hiyo ilikuwa ya aina yake haijapata kutokea Referee kutoka Sudani alikuwa akionyesha dhahiri kuwapa kila aina ya advantage lakini haikusaidia kitu, wapenzi wa Stars waliokuja na Vuvuzela zao, na huku wapezi wa Boston walikuwa wakiimba nyimbo yao “WANATETEMEKA WANATETEMEKA”

Stars walijikuta wanapata kibano cha aina yake mnamo dakika 78 baada ya kupachikwa bao maridadi kabisa lilolofugwa na Moto Nchanyambi ndipo Boston ilipotowa onyo kuwa wao ni moto wakuotea mbali kaa chonjo

Maelezo zaidi Tembelea
http://www.newenglandumoja.net

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...