NYUMBA INAUZWA KUNDUCHI BLOCK F.INA HATI HALALI ILIYOSAJILIWA NA WIZARA YA ARDHI.INA VYUMBA VITATU VYA KULALA NA KIMOJA CHA MASTER.INA UMEME WA TANESCO,INA MAJI YA DAWASCO,INA KISIMA CHA AKIBA CHENYE UWEZO WA KUHIFADHI MAJI LITA 40 ELFU NA MATENKI YA AKIBA 2 YA JUMLA YA LITA 6000.
TILES ZIMEWEKWA NYUMBA YOTE,MAKABATI KATIKA VYUMBA VYA KULALA,MAKABATI YA JIKONI,INA STOO 2 NA VYOO VYA JUMUIA 2.MBELE INA GARDEN YA MAUA,NYUMA INA GARDEN YA MATUNDA.IMEZUNGUSHIWA FENSI YENYE MIKUKI KWA AJILI YA ULINZI.IMEWEKWA PEVIN BLOCK NYUMBA NZIMA.INA AC SEBULENI NA MASTER BEDROOM,INA HEATER KUCHEMSHA MAJI KATIKA BAFU ZOTE.
MAWASILIANO PIGA NAMBA 0655303997 KWA WANUNUZI




bongoo nini...weka bei watu waangalie kama wanaweza kukurupuka.sasa unauza bei iko wapi?wengine tuko ughaibuni hatuna muda wa kupiga bongo kuuliza bei.weka bei tuanze pale.mdau california
ReplyDeleteWanunuzi msiogope kuinunua, mwenyewe sio FISADI, ni mmoja kati ya wafanyakazi waaminifu SIRIKALINI na ameijenga kwa kutumia "KAMSHAHARA" anacholipwa kihalali.
ReplyDeleteNi vizuri Muuzaji angeweka bei ili mtu ajipange kama iko ndani ya uwezo wake!
ReplyDeletesorry wadau bei ni million 400 tu. pia maelewano yapo. asanteni
ReplyDeletemimi nimuumin mzuri tu na siogopi kuonyesha fikra zangu pale tu ninapoohisi zinahitajika ukweli nikwamba hii nyumba ukiitazama kwa umakini kabisa ktk hii picha haipo strong enough moja,mbili imepinda haikonyooka yaani kama vile kuna upande ipo juu na upande wa kushoto upo chini so kwa maana hio haina ubora wa kiwango cha kutosha ni hayo tu
ReplyDeletehivi chumba cha master haikihesabiki kama bedroom?
ReplyDelete@annon naona master huwa haiesabiki kama bedroom (kibongo-bongo)
ReplyDeletehii nyumba si chini ya mil 200/300
yale yale??? bei hakuna.
ReplyDeleteHii tabia ya kuuza vitu bila ya kuweka bei inawafanya wauzaji kukosa kuaminika na wanunuzi walio nje ya Bongo unakuwa umeshawaondoa katika soko lako.
We mtu uliyecomment eti nyumba imepinda, just kwa kuangalia pichani hujatueleza ni muumini wa dini gani? freemanson?
ReplyDeleteUtakuwa muumini wa dini hiyo tu na siyo muumini wa dini za kiislam au kikristo tulizozoea. Huna haya hata kidogo!
Bei ya 400 mil haina tatizo kwa nyumba ilipo na ilivyo kwa wenye nazo.
KK
Magamba coast.
Hivi wewe anon wa Mon Oct 04, 01:10:00 PM hivi kweli uko serious? Wewe utajuaje kama nyumba haiko strong kwa kuangalia picha au haijanyooka? Upande mmoja uko juu mwingine uko chini ni kutokana na ardhi yenyewe! Mimi sio mwenye nyumba, lakini ni mhandisi mzoefu, hiyo nyumba ni nzuri na inavyoonekana kwenye picha haina tatizo lolote. Inabidi kama watu wako serious inabidi waende wakaione wenyewe. Tafadhali kama huna pese usipoteze muda wa watu! Ni hayo tu!
ReplyDeleteBafu hujengewa kioo au vifaa vya kutundikia mapazia kuzuia maji kutapakaa sakafuni, we unajenga nyumba yenye bafu ya karne gani?
ReplyDeleteNyumba hiyo imepambwa kwa kuonyesha tu uzuri kuficha udhaifu wake, ndo kusema "to paper the cracks" hahahahaha
Milioni 400 nitajenga nyumba nyingine tatu za kiwango kupita hicho.
Jamani wabongo kulaliana basi tu, kazi kwenu.
Jamani hii bei ni kiboko. Ukiwa na milioni 10 zako unapata kiwanja kizuri kabisa Mbweni, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Tuangoma n.k na unajenga ghorofa kali kwa milioni 220 tu.
ReplyDeleteHii nyumba nimewahi kuiona kwenye tvadverts.com ikiwa inauzwa, more than a year ago. Ina maana ilishauzwa inauzwa tena na aliyenunua? Au ina matatizo?
ReplyDeleteNyumba ni nzuri kwa sura nimekubali, taswira nzuri kweli kweli na mapambo gadeni, dah si mchezo, ila kwanini sibuleni umepaka rangi aina mbili? ina maana rangi ya chini ni kwa ajili ya wachafu ama? mbona bufuni umepaka aina moja ya rangi, ina maana sibuleni na bufuni tunakotolea uchafu wa mwilini ndio kunastahili kuwa na rangi moja yaani hapata chafuka?
ReplyDeleteKaboka Mchiiiz
NASHUKURU KWA MAONI AMBAYO NIMEYASOMA.NAHESHIMU MAWAZO YA KILA MDAU.LAKINI HAO AMBAO WANATAJA BEI MARA 300 AU 400 MILIONI NI WAONGO MIMI SIJAWATUMA MTU YEYOTE MWENYE NIA THABITI YA KUNUNUA NA SI MBABAISHAJI BASI ANITMIE EMAIL mwijo70jojo@yahoo.co.uk.ATAIONA NYUMBA NA KUPATANA BEI.KUWEKA BEI KWA WASEMAJI KAMA NINAOSOMA MAONI YAO WATAISHIA KUSEMA MANENO AMBAYO SI MAZURI.NYUMBA HII NI MPYA IMEMALIZIKA KUJENGA MWEZI WA TISA.KAMA KUNA MTU ANASEMA ALIWAHI KUIONA NI NYUMBA NYINGINE AJARIBU KUANGALIA VIZURI MAZINGIRA,VYUMBA,JIKO NK.ATAONA TOFAUTI HATA ENEO LENYEWE NA BLOCK NI TOFAUTI.NASHUKURU KWA MAONI YA KUTUTIA MOYO.LAKINI NASHUKURU PIA HATA KWA MAONI YA KUTUVUNJA MOYO MAANA BINADAMU NDIVYO TULIVYO.USHAURI WA BURE KWA YULE ALIYESEMA VIWANJA NI MIL 10.ANAWEZA AKAPATA HATA KIWANJA CHA LAKI 5 VIJIJINI.LAKINI KWA KUNDUCHI KIWANJA TU SIO CHINI YA MIL 45.AULIZE KWA WENYE NAVYO WATAMUELEKEZA
ReplyDeleteIt is a nice house bongo tunajitahidi siku hizi, but 4oomil? thats a bit expensive. hivi bongo website ya properties hakuna?, i have seen 1 inaitwa WWW.DARPROPERTY.NET , wanajitahidi but we need more of such. sisi tuanoishi ughaibuni tunataka sana kujua bei za sasa za properties huko bongo.ni hayo tu!
ReplyDeleteWHERE IS THE PRICE ??????????????????????????
ReplyDeleteMilioni 400/- kwa nyumba hii ni bei kubwa mno!
ReplyDeleteHata kama kiwanja ni 45m/-, ukiongeza ujenzi labda 150/-, ukiweka kifuta jasho na faida 10m/-. JUMLA 200M/--250M/- tops!
Sasa wewe unaweka bei kama vile unataka kujenga zingine 2 au 3?
Acha utapeli na kubandika bei humu ndani, tuko wataalam tunaojua haya mambo!
Inawezekana kajenga kwa mkopo, wenyewe wanataka hela zao, kuwarudishia sio kwa mtindo huu mkuu, hiyo inaitwa TAMAA!
Michuzi usibane maoni yangu!
Jamani munamlaumu bure huyu, munajua bei ya viwanja katika maeneo ya Mbezi beach mpaka Kunduchi?
ReplyDeleteNi Sh. Kuanzia milioni 100 na kwenda mbele, cha barabarani ni milioni 200. HAKUNA KIWANJA CHA MILIONI 45 LABDA CHA KITAPELI.
Michuzi, nyumba yako hii nini? Naona umeng'ang'ana nayo. Komaa baba, komaa baba. Huenda ukapata commission.
ReplyDeleteHuyo jamaa aliyesema mtu aweke faida ya milioni 10 anachekesha.. Hujui bongo hapo ndio kunawaweka watu mjini? Tena hiyo ndio wanaweka kubwa kuliko ujenzi wenyewe.. Mjini hapa.
ReplyDeleteMimi nakushauri kama huko ughaibuni bora ujenge mwenyewe kama hutamind kuishi nje kidogo ya mji kuliko kulanguliwa namna hiyo!
Mimi
sasa naanza kuamini kuwa Bw Michuzi naona una commission kubwa tu kwa jinsi ulivyokazana kuitangaza hii nyumba. Hata usipo -post najua umeisoma:-)
ReplyDeletehuyo mwenye kujiona smart na kusema eti hiyo bafu haina kioo na railings za kutundika towels etc haoni hii picha ya bafu ni nusu tu. upande mwingine unaweza kuwa na hivyo vitu vingine. anyway hata kama hivyo vitu havijawekwa hii ni minor things. hii nyumba kwakweli ni nzuri na ingekua vizuri mwenye kuiuza aseme bei yake. wewe unaweza fikiri bei yako ni kubwa sana kwahiyo unaogopa kuitoa. usiogope kwani kuna watu wengi wanavutiwa baada ya kuona bei.
ReplyDeleteNdugu Michuzi umeahidiwa kamisheni ya kiasi gani kwenye hii nyumba maana naona umekazana nayo tuu mwaka wa pili huu mpaka imeshaanza kututia kichefuchefu sasa. Najua hutaiweka lakini 'messege sent':-)serious!
ReplyDeleteMwenyewe kasema mtumieni email muzungumze sasa kwa nini hamuishi makelele, mara imepinda, mara bedroom si chumba, mara ilikuwa imetangazwa zamani, kelele zanini, kama una hela kama mimi nunua, kama hauna move on to the next item on the blog.
ReplyDelete(US Blogger)
Oxford Alumni
Naenda kununua nyumba FIJI kwa mwendo huo..Ni ili nikae karibu na ndugu au ni nini kitanifanya ninunue hiyo nyumba kwa bei hiyo. Kwanza Bongo kuna nini cha kuwafanya hata maforeigner watake kuja kununua properties? Umeme, maji hamna sasa kama wanataka kuja kuishi life style ya kudig the hole when you go #2 si wanaenda amazon forest tu wanapata ranch kwa hela hiyo
ReplyDeleteNimefuatilia hoja nyingi zilizotolewa hapa juu. Mimi napata picha kwamba sisi watanzania tuliowengi ni wajinga na hatuko serious na mambo ya maana. Ni wepesi sana kuponda bila hata kuwa na mantiki. Kama unaihitaji hiyo nyumba, si umtumie kwenye email adress aliyoitoa muuzaji? Haya maneno mengine yanatoka wapi?
ReplyDeleteHalafu, ninapata picha nyingine kwamba watu WENGI (siyo wote) wanaovisit hii blog ni wahuni ambao inaonekana hata uchumi wao unasumbua kwani siyo rahisi watu wenye mitaji yao kuwaamini kwa kuwa hawako serious. Hivyo mimi ninamshauri huyu mwenye nyumba ajaribu kutafuta website ambayo inakuwa visited na watu ambao ni business class. Hapa naona watu wengi ni watoto watoto wa shule, labda na wale watanzania walioenda nje kwa kuzamia.
Ninakubaliana kuwa hiyo bei ya 400m ni kubwa, lakini muuzaji amesha sema kuwa anakaribisha maelewano, ikiwa na maana kwamba anaweza akashuka. Hivyo ninaomba maneno ya kumkejeli huyo bwana yaachwe kwani yanaonesha ubabaishaji mionmgoni mwa watanzania.
Mtumie emnail.
Kwa kuwa wanajamii watatu wanne wanasema kuwa hii nyumba ilishawahi kutangazwa kuuzwa hapo awali, inabidi mmuzaji wa sasa atutoe wasiwasi. Kwanza, iko kwenye kiwanja kisicho na mgogoro (kiurithi nk)?, Jee iko sehemu isiyotuama maji? Haijatupiwa majini? Imejengwa karibu na baa au madanguro?
ReplyDeleteNyie mnaojiita wakaa ughaibuni, endeleeni kukaa huko huko. Nashangaa mnataka kumdanganya nani? Mimi mwenyewe nimefika California na nimekaa pale for about three months kwenye nyumba ya shemeji yangu. Nilishangaa sana kuona nyumba ya ovyo yenye bedrooms 3 na choo kimoja cha ndani cha ku-share, tena ya mbao, eti amenunua kwa dola laki mbili tena mwaka 2000. I was so shocked. Huyo anayeuza hiyo ya kwake, pamoja na kutokutaja bei, lakini kwa milioni 400 ni sawa kabisa ukizingatia na eneo lenyewe. Tatizo lililopo kwa wabongo ni kuponda vya wabongo wenzao, lakini ingekuwa majuu wangeinunua hata kwa zaidi ya hapo. Mimi nakaa maeneo ya huko mbezi beach na hivi ninavyoandika hapa, jirani yangu kauza kiwanja chake medium density kwa milioni 230 wiki iliyopita tu. Maeneo hayo, thamani ya kiwanja iko juu kuliko ujenzi. So, if you think it is expensive, hiyo ni kwako wewe, kwa wenzio hiyo ni bei ya kawaida. You can choose to live Tandika, Tuangoma etc na uachane na ndoto za kuishi kwenye maeneo ambayo ni ghali.
ReplyDeleteMSIMAMO WANGU UPO PALE PALE BONGO SIRUDI MPAKA SIKU NIKISIKIA ANKAL MITHUPU AMEKUWA RAIS
ReplyDeleteKILA NYUMBA LAZIMA IWEKWE MAVYUMA MADIRISHANI NA MILANGONI UTASEMA NI JELA AU BANDA LA SIMBA
MAISHA YA HUKO NYUMBANI NI MAGUMU MNO TUNAISHI BILA AMANI KILA SIKU ROHO JUU UMELALA HUKU UNAWASIWASI LABDA WAZEE WA KAZI WATAKUINGILIA USIKU WAKUACHE UKIWA UCHI
MAANA AMANI NI NDOGO SANA HUKO NYUMBANI NI MTU UNASHINDWA KUJISIKIA UPO HURU NYUMBANI KWAKO UKITAKA KUJENGA NYUMBA NI LAZIMA UZUNGUSHIE MICHUMA UTASEMA UNAISHI KATIKATI YA MBUGA YENYE SIMBA WENGI
SIRUDI NA NARUDIA SITORUDI KUISHI NDANI YA FENSI KANA KWAMBA NI MFUNGWA.
ASANTE ANKAL.
Its a very very beautiful house, wanaojitia kuikosoa ukienda kucheki wanazoishi wao hata robo ya hiyo haifikii kwaiyo ACHENI KUCHONGA. Wengine mnajipangia na bei kabisa, mwenyewe kawatajia?? Amewaambia ambaye yuko serious awasiliane nae na contact katoa. But samahani, mimi nina swali moja tu kwa muuzaji "why would someone want to sell such a beautiful house?" nashangaa
ReplyDeleteSasa nyie watu wa whitecastle real estate...THIS IS HOW YOU ADVERTISE A HOUSE...sio kutupigia kipicha cha kuiba from gate ya jirani kwenye gari....eti mnauza nyumba...JIFUNZENI jinsi ya ku advertise a house.
ReplyDeleteHakuna kitu 400m/- kwa nyumba hii ni bei kali mno, inaonekana anataka kutajirika mapema tu.
ReplyDeleteHebu angalia uchumi wetu ulivyo, sasa kila mtu akijipangia bei ya kama hiyo itakuaje, lazima kuwe na regulators wa bei za nyumba.
Niko very interested kumpeleka valuator wa nyumba aende pale, halafu atupe bei kamili plus cha juu, na uhakika hata 200m/- haitafika!
Eti anajidai bei ya viwanja imefika 100m/-! Kiwanja kiwanja gani kunduchi ununue kwa bei hiyo? Basi lazima wewe uwe na elimu ndogo na kutokua makini na hela zako.
Weka bei ya kiukweli hapa na sie tutasema kweli kwa bei hiyo ni haki, na sio kutaka kutupiga changa la macho kwa bei kama hiyo, ingia tz adverts uone nyumba kama hizo zinauzwa ka kiasi gani.
Hata usemi nini, hiyo bei HAPANA HAPANA, hata kama unataka maelewano lakini mbona umeanzia juu sana, typical bei za kibongo, watu wanajitajia tu, ni kama karibu vitu vyote bongo, mpaka wakuangalie juu mpaka chini, ndio wanakupa bei, hata kwa kinyozi, sijui kwanini hatuna tabia ya kubandika bei za vitu na services, yote tumezoea utapeli tapeli tu!
Bure kabisa!
mishahara kima cha chini haizidi laki 2 kwa mwezi
ReplyDeleteWEWE ANON OCT 6, 02:29PM UNA MATATIO SANA.
ReplyDeleteKWA RAHA ZAKO USIRUDI BONGO HATUNA SHIDA NA WATU WA AINA YAKO.
HAPA BONGO MAMBO POA SANA, PESA IKIKUBALI HATA VOGUE INAKUJA , TENA KWA NDEGE!!!
WE DRINK THE BEST WINE BILA KUBEBA MABOKSI!!
NDIO MAANA HAPA PANAITWA BONGO.
USIPORUDI HAPA IT IS YOUR OWN FUNERAL!!
ALIYEPOST HIYO NYUMBA,NAMPA PONGEZI NA NI NYUMBA STANDARD KWA HAPA BONGO.NINGEKUWA NA PESA SASA HIVI NINGENUNUA,NGOJA UCHAGUZI UISHE.
MICHUZI MIMI NASIKITIKA NA WATU WANAOTAKA KUTUHARIBIA BLOG YETU NZURI YENYE HESHIMA.JAMANI MIMI NDIO MWENYE NYUMBA,NIMESEMA ANAYETAKA KWELI AMBAYE NI MNUNUZI AWASILIANE NAMI AIONE NYUMBA TUELEWANE BEI.HIZO MILIONI 400 ZINAZOANDIKWA NANI AMESEMA?MBONA HIYO MIMI SIJAANDIKA BEI?WEWE KAMA UNA HELA YAKO WASILIANA NAMI NIMEKUPA EMAIL,NIMEKUPA SIMU HAYA YOTE YANATOKA WAPI?NINGESHAURI TUWE WASTARAABU WEWE KAMA HUWEZI KUNUNUA USIANZE KUPANGA BEI KWENYE MALI ISIYOKUWA YAKO.NILISEMA MWENYE NIA TUWASILIANE SASA SHIDA IKO WAPI?POLE
ReplyDeleteMUUZA NYUMBA,
ReplyDeleteNina wasi wasi kwamba wapanga bei ni watu ambao umeshawasiliana nao kabla? ndo hawa wamekuja kutubwagia bei hapa.. sasa kama ni waughaibuni ukawapiga hiyo 400ML ya haraka haraka... hahaha mimi nataka utundike bei halisi..budget yangu ni 180ml tu..
pesa 400,000,000.00 TZS ni sawa 191,888.710 EUR kwa hapa Ulaya huwezi kupata nyumba kubwa kama hiyo kwa gharama kama hiyo. Pesa iliyowekwa ni ndogo mno. Kwa hela kama hiyo ni apartment tu yenye sebule, chumba kimoja kijiko na choo, tena unalipa kidogo kidogo kwa morgage labda kwa miaka 20. Shida Hapa muuzaji anataka keshi aondoke zake. Kupata kiwango hicho kwa walio wengi ni shida na mabenki ya Tanzania kutoa mkopo au morgage ni kazi na interest utakayopigwa utaishia kulipa mkopo mara mbili
ReplyDelete