Na Ally Kondo, New York
Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani wanachama wa Umoja wa Mataifa kupinga vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani miaka 50 iliyopita dhidi ya Cuba.
Nchi 187 wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania ikiwemo zilipiga kura ya ndio kuunga mkono Azimio lililowasilishwa na Cuba kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutaka vikwazo hivyo vilivyowekwa na Marekani viondolewe.
Upigaji kura huo ulifanyika wakati wa kikao cha 65 cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kinachoendelea mjini New York tarehe 26 Oktoba 2010. Nchi mbili, Marekani na Israel zilipinga Azimio hilo. Aidha, nchi tatu, Palau, Micronesia na Marshall island hazikuunga mkono upande wowote.
Akihutubia kikao hicho Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue alieleza kuwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Cuba vimesababisha matatizo makubwa kwa watu wa Cuba na kurudisha nyuma jitihada za nchi hiyo za kujikwamua kiuchumi na kijamii. “kwa kiasi kikubwa vikwazo vimekwaza juhudi za Serikali ya Cuba za kuondoa umasikini na kuinua hali ya maisha ya wananchi wake” Balozi Sefue alisikika akisema.
Balozi alisema kuwa, vikwazo vimesababisha madhara makubwa kwa kinamama na watoto wa Cuba na zaidi ya hapo vinainyima Cuba haki ya kufanya biashara na nchi nyingine duniani pamoja na kukwamisha juhudi za Serikali ya nchi hiyo kufikia Malengo ya Milenia.
Balozi Sefue alieleza kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba haviathiri nchi hiyo tu bali pia vina madhara kwa uchumi wa nchi nyingine. Tanzania inaviona vikwazo hivyo kuwa ni ukiukwaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa na Sheria za Kimataifa.
Balozi alimalizia kwa kueleza kuwa, Tanzania inashirikiana na Cuba katika maeneo mengi ikiwa ni pamoja na uchumi, elimu na afya. Alieleza kwamba, ushirikiano huo utaimarika na kuwa mzuri zaidi ikiwa vikwazo dhidi ya nchi hiyo vitaondolewa.

are we still non aligned?
ReplyDelete