Kikosi cha Tanzanite FC
Kikosi cha timu ya Silverbacks FC

Timu ya Soka ya Tanzanite FC ya Atlanta Ga, almanusura iibuke kidedea jana katika mechi yao ya kwanza ya Daraja la tatu. Timu hiyo ambayo ilikuwa ikimenyana na timu ngumu ya Fc Silverbacks ya Nocross Ga ilifanikiwa kugawana point na wageni hao baada ya kufungana bao 2-2.

Mchezo ulikuwa mkali na wakuvutia. Wenyeji Tanzanite ndio waliokuwa wa kwanza kuona nyavu za Wageni hao kutoka Nocross kwa goli safi kutoka kwa Abbas.

Iliwachukua wageni hao dk. 20 kurudisha goli hilo kutokana na makosa ya mabeki wa Tanzanite kuchelewa kuokoa mpira ulio panguliwa na Golikipa Togoleni Kirumbi. Hadi tunakwenda half time timu hizo zilikuwa zimefungana 1-1.

Kipindi cha pili ilikuwa ni zamu ya Fc Silverbacks, kwani waliweza kuonyesha soka maridadi na kufanikiwa kuandika bao katika dk. ya 50 kwa mkwaju wa adhabu ndogo.

Haikuwachukua muda Watanzania hao kuswazisha bao hilo kwa goli safi lililofungwa na Malik Mohammed baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa kiuogo Elvis Mnyamuru " Gazza".

Mfungaji alifanikiwa kuwachomoka mabeki wa Silverbacks na kumpiga kipa kanzu kabla ya mpira kujaa kimyani.
Hadi tunakwenda katika studio zetu za " Pugu Road" matokeo yalibakia 2-2. Timu ya Tanzanite Fc itaendelea na mechi zake kila Jumapili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Washikaji kweli mnajua kujiremba kama waEngland.Mmeponea chupuchupu afu mnadai kidogo mshinde.LOL.

    ReplyDelete
  2. KIUNGO ABDUL BAGDELA VIPI MBONA UWANJANI HAYUMO KAZEEKA KAJIUZULU AU ANAENDELEZA BASKET MZEE WA MASHUGHULI TUNA MMISS.

    ReplyDelete
  3. Hahahaha Duh eti Kujiremba sasa unadhani itakuaje kila mtu ana namna yke ya kureport na wao nao watakua wameriport kwa namna yao!! Studio za pugu road Hahahaha!! Ila kitu kimoja tu nakiuliza sina majibu ni ligi daraja la tatu Mkoa (Nchi) gani!!??

    ReplyDelete
  4. Mdau apo juu! Jamaa wanacheza ligi daraja la tatu katika State ya Georgia ngazi ya Mkoa. Mkoa wa Atlanta. Ligi inaitwa ADASL unaweza uka google kufuatilia mechi zao. Hongereni Watanzania wenzetu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...