Uwanja wa Amaan Stadium, Zenji, unavyoonekana leo baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa ambapo tayari zuria la riadha limeshawekwa na nyasi mpya kupandwa huku majukwaa yote na kuta yakiwa yamepigwa rangi na sehemu za mapumziko na maliwato kutengenezwa. Hoteli ya Amaan iliyoko pembezoni nayo haijasahaulika na sehemu hii sasa inatoa taswira njema. Uwanja huu, unaotarajiwa kufunguliwa mapema mwezi ujao, umekuwa hautumiki kwa muda kutokana na ukarabati huo. Hivyo michezo yote, hasa mpira wa miguu, ilihamia uwanja mkongwe wa Mao Tse Tung.
Home
Unlabelled
uwanja wa amaan stadium, zenji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Bado sijafika Zenj, kumbe stadium yao ni sawa na uwanja wa mpira wa wilaya ya Bumbuli, duh makubwa hayo, ndo maana sherif ananadi sera za kujenga kakiwanja ka kisasa, mpeni kura basi abadilishe huo uwanja wa Bumbuli.
ReplyDeleteOk bora usifike maana nyie huko ndio kwanza Juzi mmepata uwanja wakati wenzenu wana uwanja wa maana tu siku nyingi.Kabla ya uwanja wa NESHINO kulikua na uwanja gani wenye majukwaa upande mmoja tu!!! Ushike adabu yako!!!! SAFARI HII UWANJA WA NDEGE WA TAIFA UTAHAMIA ZENJI MAANA KILA KITU CHA TAIFA KIPO BARA..
ReplyDeleteNaona uwanja huo kwa bara unaweza kuulinganisha na ule wa Karume, sijui mashabiki elfu thelethini kama unaweza chukua. Nashauri mjenge kama ule wa Majimaji-Songea au Alhasan Mwinyi-Tabora itavutia wengi kuingia vinginevyo unavyoonekana inanipa wasiwasi kama nitapata nafasi ya kukaa, naona kama kuna mistari si zaidi ya kumi kwenye safu ya mzunguko
ReplyDelete