Kikosi cha Taifa Stars
Kikosi cha Morocco

Na Mwandishi Wetu.

BAADA ya kula za uso kwenye mechi ya Stars na Brazil, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeshika adabu na kupunguza vingilio vyake vya mchezo wa Stars na Moroco utakaochezwa Jumamosi ijayo kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2012 nchini Gunea.

Viingilo viivyotangazwa katika mpambano wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika(AFCON) ni pamoja na kile cha Sh 5,000 ambacho ni cha chini kabisa wakati kile cha juu ni Sh30,000.

Kutangazwa kwa viingilio hivyo vinavyoonekana kuwa nafuu kwa wapenzi wengi wa soka nchini ni kutimia kwa ahadi aliyoitoa juzi jijini Dar es Salaam Raisi wa TFF Leodegar Tenga wakati wa uzinduzi wa kampeni za kuishangilia Taifa Stars aliposema wamepanga kutoa unafuu ili wananchi wengi waweze kujitokeza.

Akitangaza viingilio hivyo,Afisa habari wa TFF Frolian Kaijage alisema kuwa kiingilio cha Sh 5,000 ni kwa wale watakaokaa jukwaa la kijani wakati kile cha Sh 30,000 ni kwaajili ya jukwaa maalum (VIP A).

Kaijage alivitaja viingilio vingine kuwa ni Sh 7,000 kwa Jukwaa la Rangi ya Bluu,Sh10,000 kwa jukwaa la rangi ya machungwa wakati VIP C kiingilio kitakuwa Sh 15,000 na Sh 20,000 kwa jukwaa la VIP B.

Alisema kuwa tiketi kwaajili ya mpambano huo zitaanza kuuzwa kesho baada ya kumalizika kwa uhakiki utakaofanywa leo baina ya shirikisho hilo,Polisi na Usalama wa Taifa.

Katika hatua nyingine Kaijage alisema kuwa waamuzi wa mpambano ambao wote wanatoka Mauritius wanatarajia kuwasili nchini kesho sambamba na kamisaa wa mchezo anayetoka Kenya.

Aliwataja kuwa ni Sochurn Raji atakayekuwa mwamuzi wa kati wakati Bootun Balkrishina na Bally Vivian wakiwa ni wasaidizi na kamishaa Muhammad Imterazi.

Katika hatuna nyingine Kaijage alisema kuwa msafara wa Morocco wenye jumla ya watu 40 unaojumlisha wachezaji na viongozi wa timu hiyo kutua nchini leo usiku saa 4.30 tayari kwa mchezo dhidi ya Stars.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Sidhani kama kweli kuna mtu mwenye akili timamu ataenda kuangalia Stars. Katika hiyo picha hapo juu hakuna hata mchezaji mmoja wote ni useless. TZ mpira uko mchangani lakini si kwa top teams kwenye ligi kwani wachezaji wote waliopo huko ni wachawi, na ndiyo maana unaona hawaendelei, Bongo si nchi ya kufungwa na Rwanda, Uganda, Kenya, hata na Burundi ila kwa kuwa tumeweka uchawi mbele tunafungwa kama vichaa.Kweli Mwinyi alikuwa anasema ukweli juu ya kichwa cha mwenda wazimu.

    ReplyDelete
  2. tickets zina numbers za viti au ndio mambo yale yale ya wizi wa mapato!

    ReplyDelete
  3. napingana na wewe anonymous oct 5,08:32:00 kuhusu uchawi zamani kweli iman zilikuwa hivyo kwasasa soka limebadilika kidogo mie ni mzalendo nitaenda hata kama tukifungwa najua mwanzo mgumu baadae Tanzania itakuwa juu kisoka tena tuna nafuu kubwa sana kwa sasa kisoka kuliko nyuma kuwa mzalendo sio kukatisha tamaa.

    ReplyDelete
  4. wee jamaa sidhani kama wewe ni mtanzania, yaani unaongea kama mzamiaji, wachezaji wakitanzania wanajitahidi sana tu! kila siku soka letu linafanyiwa marekebisho na kila aina ya huduma ila tatizo ni kwa viongozi na maandalizi yao ya zima moto. ILA KWA SASA MAANDALIZI SIKU HIZI NI MAZURI UNAONA TUNAWATOA USHAMBA WAZEE WAZIMA! au wewe uko dunia gani!! vijana wanajituma sana tu!! watu kama nyie hamfai hata katika kutoa ushauri! kwani watu kama nyie mnadidimiza na hata mnakatisha tamaa watoto wetu ambao wana ndoto za kucheza soka! ETI UCHAWI! WEE VIPI!!
    MICHUZI BWANA HUU NI WAKATI WA KUPEANA MOYO NA KUWAPA SUPPORT YA KUTOSHA VIJANA WETU WAFANYE YALE WALIYOYAFANYA KULE KWA WAARABU!
    comment kama za huyu jamaa hata hazifai kuwepo mda kama huu bwana!!
    mnatia kichefuchefu!

    ReplyDelete
  5. Mbona viingilio cheap hivyo...Duh VIP only 30,000. Kweli bongo tambarare hakuna uwiano wa vitu kabisa. Nyumba mnauza million 400 halafu ticket bei hiyo.Kama mji huo una watu wa kununua nyumba kwa bei hiyo basi na hizo sehemu vitu vyake vingetakiwa viwe ju...VIP wangetakiwa walipe $200 to $3000.

    ReplyDelete
  6. Hili game saa ngapi?

    ReplyDelete
  7. we Anoy wed oct 06, 07:04AM,
    hao wanao nunua nyumba hizo za mil 400, sio wapenzi wa mpira,.. wala hawaji mpirani...

    ReplyDelete
  8. kwa maoni yangu nadhani tanzania ndo nchi inoongoza duniani kwa kujua kila kitu...eti kuna mtu hapa anipinga tiketi kuuzwa bei nafuu duh haaa haaaa haa kua uyaone!
    mwingine eti hakuna wachezaaji wote wachawi hivi kusoma hujui hata picha huoni kweli???
    nadhani hapa issue sio hizo cha kufanya ili tushinde hii mechi ni kwa viongozi wetu wajifunze mazengwe kama ya viongozi wa africa magharibi, tununue refa kila aina ya kitu tufnye this is must win game...tusisubilie matokeo ya uwanjani tu, tuanze kuandaa ya nje pia ila tukileta ustaarabu wetu wa kibongo tutaishia hivyo hivyo miaka yote, ugenini tunafanya vizuri nyumbani tunadraw au kufungwa....WAKE UP TANZANIA THE TIME IS NOW, learn from UGANDA VS ANGOLA

    ReplyDelete
  9. We anon wa Wed Oct 06, 07:04:00 AM umethibitisha kweli mbongo kaumbwa kulalamika,yani hata ufanye zuri au baya yeye atalalamika tu!! Lol,kazi ipo nchi hii!!

    ReplyDelete
  10. HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA SOKA BADO BONGO, MAXIMO ALISEMA ALITUKUTA TUKO ICU YAANI INTENSIVE CARE UNIT.

    ReplyDelete
  11. arehe Wed Oct 06, 07:04:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

    wewe mpiga box unaongea utumbo!!

    ReplyDelete
  12. kwa kweli TFF wameishiwa. Gemu la Brazil walituona wa nini wakapanga bei kama tuko Majuu. Leo wanatubembereza tutoe buku 5, wala hatuji. Mpate fundisho.
    Tiketi kama haitakuwa na seat number tujue nyumba zao hawajamalizia. wanasubiri pesa zetu. TFF be serious

    ReplyDelete
  13. Anonymous 7:04:00am we acha tu huku bongo ndio hivyo brazil walikuja hapa wakatoza viwango vya juu uwanja ulikuwa mtupu hakuna mtu bora waeke ili na walalahoi tufaidi.

    ReplyDelete
  14. Jersey za stars...blue and black...??? blue with green stripes what the heck...yaani watu wote mmeshindwa kuchagua rangi za maana...ok...inaweza ikawa (1)plain yellow and black...zote ziko kwenye national flag...(2)yellow jersey with black stripes n black shorts....(3) green and yellow (4) Blue and yellow...hao wachezaji wanaonekana wana afya mbovu kutoka na rangi za jersey too dark and disorganized and so cheap...cmon guyz u need to upgrade...i kno u can do some.. with all those sponsorship...!!!

    ReplyDelete
  15. katika kicho kikosi ya tanzania goalkeeper ndo yupi kwani naona akuna tofauti wote wamevaa jezi ya bendera sawa. akuna tofauti ya jezi ya goalkeeper

    ReplyDelete
  16. hii team ya wasudani ama tanzania !! LOL
    mdau # 1 wa michuzi

    JIJI la paris

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...