Mwenyekiti wa Tasnia ya ufuatiliaji wa sekta ya madini inayosimamia uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za madini nchini (TEITI) Jaji mstaafu Mark Bomani akizungumza na Mwenyekiti wa Tasnia ya ufuatiliaji wa sekta ya madini inayosimamia uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za madini kimataifa (EITI) Dkt. PeterEigen(katikati) na Kamishina wa madini wa Wizara ya Nishati na Madini Dr.Peter Kafumu mara baada ya kufungua mkutano wa kimataifa wa EITI leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Tasnia ya ufuatiliaji wa sekta ya madini inayosimamia uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za madini nchini (TEITI) Jaji mstaafu Mark Bomani akizungumza na wadau wa sekta ya madini wa ndani na nje nchi wakati wa mkutano wa kimataifa wa Tasnia hiyo unaozihusisha nchi zenye utajiri wa gesi, mafuta na madini ambapo Tanzania ni mwenyeji wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Wadau wa sekta ya madini kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijili wakati wa mkutano wa kimataifa wa EITI leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Sidhani kama tunahitaji mikutano baada ya mikutano baada ya mikutano baada ya mikutano. Tunahitaji mikataba mipya ya madini, wawekezaji asilimia 50 na umma wa watanzania asilimia 50. Halafu wawekezaji wanalipa ushuru, pamoja na mrahaba wa asilimia 3 hadi 5 kwa ajili ya kuendeleza maeneo ya machimbo.

    Zaidi ya hapo ni ushabiki, maneno matupu na sherehe zisizokuwa na mpango.

    Najua muheshimiwa sana Dr. Michuzi huwezi itoa hii kwasababu ya ushabiki. Globu ya jamii = Globu ya Serikali???? Just thinking out loud!

    ReplyDelete
  2. Ni kweli hatuitaji Mikutano.
    Hivi kwanini serikali inashindwa kusimamia utajiri wetu. Mbona Nigeria wanafaidi utajiri wao wa Mafuta. Sisi tuna madini kibao lakini nchi ni masikini pamoja na watu wake. Wanafaidi wawekezaji tuu, bado hawajapewa na miaka mitano ya msamaha wa kodi, baada ya miaka mitano wana badilisha jina la kampuni. Jamani viongozi angalieni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...