Waziri wa Ajira, vijana na maendeleo ya wanawake na watoto, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Asha Juma, akiwa katika Mkutano wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayoshughulika maendeleo ya Jamii. Katika Mkutano huo, Waziri Asha amesema Tanzania imeridhishwa na namna ambavyo Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Kimtaifa illivyotambua umuhimu wa ushiriki na ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya millenia
WATU WENYE ULEMAVU NI SEHEMU
MUHIMU KATIKA UTEKELEZJAI WA MDGs
Tanzania imeelezea kuridhishwa kwake na matokeo ya mkutano wa kilele wa wakuu wa Nchi na Serikali uliotathimini utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millennia (MDGs) kwa kutambua umuhimu wa ushiriki na ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika utekelezaji wa malengo hayo.
“ Kama nchi ambayo kwa kushirikiana na wenzetu wa Philippines tulisimamia mchakato wa majadiliano yaliyozaa tamko kuhusu nafasi na haki ya watu wenye ulemavu katika utekelezaji wa MDGs, tumeridhishwa kwamba hatimaye jumuia ya kimataifa imelitambua hilo”
Waziri anayeshughulikia masuala ya ajira, vijana, maendeleo ya wanawake na watoto, Asha Juma kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Ameyasema hayo wakati alipokuwa akichangia majadiliano ya Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia maendeleo ya jamii. Mkutano huo Makao Makuu ya Umoja huo jijini New York.
Akasisitiza kuwa watu wenye ulemavu ni sehemu muhimu katika suala zima la maendeleo ya jamii katika ujumla wake, na kwamba kutozingatia ushiriki na ushirikishwaji wao kunaweza si tu kuchelewesha utekelezaji wa MDGs lakini pia kuna hatari ya kundi hilo la jamii kuachwa nyuma.
Waziri Asha Juma aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo , licha ya kuelezea umuhimu na haja ya ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika utekelezaji wa MDGs, pia alielezea hatua mbalimbali zilizofanywa na serikali katika kuchagiza maendeleo ya jamii.
Akasema kwa mfano serikali imeandaa na kutekeleza sera zinazotilia mkazo ushirikishwjai wa makundi mbalimbali ya jamii katika ushiriki na kutoa maamuzi yanayohusu maendeleo yao.
Aidha akabainisha kuwa serikali za mitaa ambazo ndizo hasa zinazohusika kwa karibu zaidi na maendeleo ya wananchi zimepewa madaraka zaidi.
Kwa upande wa nafasi ya mwanamke katika kujiletea maendeleo yake, Waziri Asha Juma ameueleza mkutano huo kwamba, mwanamke wa kitanzania anayonafasi kubwa ya kujiletea maendeleo yake na kukabiliana na umaskini kwakuwa serikali imemjengea uwezo na mazingira ya kufanya hivyo.
“ kupitia marekebisho ya sheria kadha wa kadha ikiwamo sheria ya ardhi, mwanamke wa tanzania amepewa nguvu za kisheria za kumiliki ardhi yake mwenyewe na hii ni natua kubwa sana kwa maendeleo ya mwanamke na taifa kwa ujumla.
Kuhusu kilimo, Waziri amesema kuwa serikali ya Tanzania imebaini kwamba vita dhidi ya umaskini haitaweza kufanikiwa kama sekta ya kilimo haitapewa umuhimu unaostahili.
Na kwa kulitambua hilo, na kwa kuzingatia kwamba sekta hiyo ndiyo inayoajiri watu wengi hasa wale wa vijijini, serikali imeanzisha progamu ya kukuza na kuendeleza kilimo maarufu kama Kilimo Kwanza.
Akihitimisha mchango wake, Waziri Asha Juma amesema licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali za kuboresha maisha ya watanzania, bado watanzania waliowengi ni maskini.
Akatumia nafasi hiyo kuchagiza ushirikiano endelevu kati ya serikali na jumuia ya kimataifa ili kuongeza kasi ya kuwaletea maendeleo wananchi wengi zaidi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hawo wa Morocco awajatua tu !! wekeni picha basi

    ReplyDelete
  2. Hongera Mama Asha Juma kwa kutuwakilisha vyema katika anga za umoja wa mataifa. na pia kidumu Chama cha Mapinduzi kwa kutambua wanawake wenye uwezo na kuwapa madaraka.

    sielewi comments za huyo anonymous hapo juu, kwani watu wa Morocco wanahusiana vipi na habari hii.

    ReplyDelete
  3. Ni bomu huyo Asha juma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...