Hii ndio ajali ilyotokea asubuhi hii upande wa Kigamboni ambapo gari aina ya Toyota Hilux pick up linalo tumika kusambaza nyama katika maduka ya nyama ya Kigamboni limepata ajali ya kuzama baharini baada ya kile kinachosemekana kujaribu kuwahi kuingia katika Pantoni bila mafanikio. Habari zizizo rasmi zinasema dereva wa gari amekufa na msaidizi wake amenusurika, na kwamba mwili wa marehemu umeshaopolewa lakini gari bado iko majini huku juhudi za kulitoa zikiendelea. 


oh wao!!this is sad.
ReplyDeletehuyo dereva hana akili utawahi vip pantoni kama umeona imeshaanza kuondoka?
ReplyDeletena wale wafungua mageti pale walikua wapi hadi kuruhusu gari iende wakati pantoni imenza safari some thing fish was going on!!!!!!!!!!!!!
Huyo anaeshughulikia ufunguaji na ufungaji wa gate ndiyo awajibishwe kwani huu ni uzembe usio na mfano ambao umesababisha kifo cha bure.
ReplyDeleteAshitakiwe kwa kusababisha mauaji
kuwahi io tatizo sasa ilo [pantoni likiondoka linakua milango wazi?
ReplyDeleteislaeri tu alikuwa anamwita mwamba, zake nae zilifika ndomana kafunguliwa milango yoote
ReplyDeletehapo moja wanaofanya kazi hapo lazima washitakiwe lazima wajifunze kuzuia magari na watu, hapo pantoni ndio liondoke kwa usalama, turudi kwenye hilo gari wote hatuna huwakika amefariki vipi labda kapata mstuko wamoyo kashindwa kusimamisha, mwenyezimungu amuweke mahali pema peponi. mz
ReplyDeleteKwa kwlei kuna ajali mbaka unashindwa kuelewa, how pantoni iondoke mlango wazi na zile gate silikuwaje, je ni gari ilirudi kinyume nyume yani una shindwa kuelewa how.
ReplyDeleteBinadamu anafariki hafi
ReplyDeletehuyo anonymous aliyesema dereva hana akili, yeye ndo hana akili. Lakini jambo lingine inakuwaje wanaoruhusu magari kuendelea kuruhusu wakati wanajua panton imejaa? hao ndio waliosababisha balaa hili.Dereva naye wa Panton huwa anapata mawasiliano kutoka kwa nani, au anaangalia tu magari yanavyoingia, na anapoona hakuna kitu ndo anaanza safari au vp? Kuwe na mawasiliano yanayoeleweka, tusije siku moja tukajikuta tunapoteza mamia ya roho za watu.
ReplyDeleteHalafu utasikia watu wanasema kuna mkono wa mtu ooh mara kuna jini maeneo hayo,ooh siku zake(dereva wa gari)zilifika.Uzembe na Ujinga wa madereva ndiyo chanzo cha ajali nyingi bongo.Hizi dhana za sijui "islaeri alikuwa anamwita" kama mdau mmoja alivyosema ni za kizamani.Tuachane na hizi fikra za kizamani utakuta dereva alikuwa amelewa halafu anasababisha ajali inayouwa watu kibao lakini bado kuna mijitu itasema ni kazi ya Mungu wakati ni uzembe wetu.Watanzania tunamsingizia Mungu kwa kila kifo kinachotokea.
ReplyDeleteInavyoonekana marehemu dereva aliamini kila kitu kinawezekana baada ya kuangalia sana hollywood movies.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.Amen.
ReplyDeleteIngawaje ni msiba, kwa kweli comments zimenifurahisha sana asubuhi ya leo. Suala linabakia pale pale kuwa kuna uzembe mkubwa sana kwenye kuhakikisha usalama wa Watanzania. Nahondha lazima alikuwa anaona gari linakuja, kwanini asubiri kidogo? Watu wa gate nao kwanini waruhusu? Na ilikuwaje wakaruhusu gari kubeba abiria zaidi ya dereva baada ya kuvuka gate,,,, na mengine mengi
ReplyDeletemi ninavyojua ni kwamba pale yanaanza kuruhusiwa magari kwanza then abiria ndio wanakua wamwisho kuingia imekuaje hili gari ndio liwe la mwisho baada ya abiria kuingia huu ni uzembe wa wale watu wa getini coz wao ndio wanaoruhusu magari kuingia na kuna idadi ikifika yanazuiliwa then abiria nao wanaruhusiwa kuingia
ReplyDeletekifo kipo,kilikuepo na kitaendelea kuwepo,hakuna mawazo ya kisasa wala kizamani,general Tito wa Yugoslavia alizungukwa na madaktari bigwa kutoka karibu dunia nzima na walishindwa kuzuia kifo chake,hivyo kwenye kifo hakuna mawazo ya kisasa wala kizamani, cha msingi ni kujua ilikuwaje mpaka mwenzetu ametutoka kinamna namna...
ReplyDelete