
MCHEZAJI NYOTA WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA NA YANGA AMEFARIKI DUNIA LEO AFAJIRI KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM ALIKOKUWA AMELAZWA KWA SIKU KADHAA AKIWA ANASUMBULIWA NA MARADHI YA TUMBO.
HABARI TOKA NYUMBANI KWAO KIGOGO AMBAKO MSIBA UPO ZINASEMA JUMA MKAMBI ALIPOTEZA FAHAMU JANA NA USIKU WA KUAMKIA LEO AKIKUWA KATIKA HALI MBAYA KABLA YA KUKATA ROHO ALFAJIRI.
JUMA MKAMBI, ALIYEPACHIKWA JINA LA 'JENERALI' KWA UWEZO WAKE WA KUONGOZA NGOME YA YANGA NA TAIFA STARS AKICHEZA NAMBA SITA AMBAPO ALIWEZA KUPANDA NA KUSHUKA KWA USTADI WA HALI YA JUU, ATAKUMBUKWA KWA MCHEZO WAKE WA AKILI NA KISTAARABU PAMONA NA KUWA NA UMBO LA MIRABA SITA.
MIPANGO YA MAZIKO INAFANYWA NYUMBANI KWAO KIGOGO, NJIA YA DAMPO YA ZAMANI, NA ANATARAJIWA KUZIKWA KESHO SAA SABA ADHUHURI MAKABURI YA KISUTU (SIO KIGOGO DARAJANI).
MOLA AIWEKE MAHALA PEMA ROHO
YA 'JENERALI JUMA MKAMBI'
- AMIN
tumempoteza mtu muhimu sana katika wahasisi wa soka hapo nyumbani hao ndio walikuwa wanacheza mpira sababu ya mapenzi ya mpira na sio pesa poleni sana familia ya mfiwa
ReplyDeletemdau kutoka mji wa kusoma hapa united kingdom
INNA LILAH WAINALJUINA namkumbuka ndiye aliyeiokowa yanga mwaka80ktk vipigo mfululizo ya mnyama
ReplyDeletePoleni jamaa wa marehemu pamoja na wapenzi wote wa soka.
ReplyDeletepoleni wafiwa.mungu ailaze mahali pepa pemoni roho ya jenerali.namanyile sana juma mkambi.alikuwa anacheza three position in time.yagenda kushoto yagenda kulia.yaaani nina machungu sana.
ReplyDeletemdau wa Norway
Inna Lillah wa Inna Illah Rajiun hakika sisi kwake ni marejeo. na kila nafsi itaonja mauti . mola amuweke mahala pema peponi na awape moyo wa subra wafiwa Amin. lakini mtazamo wangu mbona kila mwana michezo siku hizi akifa anakufa kwa ugonjwa wa tumbo ? mfano ni Marehemu Mziray na juzi tu Marehemu Kajembe na leo Marehemu Mkambi mmmhhh ikiwa hivyo hili tumbo litatumaliza.
ReplyDeletemdau Paka la jikoni.
R.I.P Generali Juma Mkambi!!
ReplyDeletejenerali Mkambi, Mola akuweke mahali pema peponi. Ulikuwa "mvinje" wa mtu, lakini hukuutumia ukubwa wako kuwaonea waliokuwa wadogo.
ReplyDeleteTutakukumbuka kwa mema uliyotufanyia wapenzi wa soka nchini na wapenzi wa Dar-es-salaam Young Africans.
poleni ndugu na jamaa wote, Amiri jeshi alikuwa one of my all-time favourite players back in the 80s, mimi ni simba damu lakini nasema Juma Mkambi forever!!!! msomali wa dom
ReplyDeletePøleni sana ndugu ,jamaa na marafiki.Kweli kifo hakina huruma.Nakumbuka mara ya mwisho tumekutana Bagamoyo-kawambwa Cup tulivyojadili kuhusu kuendeleza soka na kuhusu nafasi kwa wachezaji wa zamani.RIP brother!
ReplyDeletePOLENI SANA TANZANIA STARS "Selengo"
ReplyDeleteR.I.P mzee wa 'LONG RANGE' mita kama 40 hivi 1980. Kwa wale tuliokuwepo enzi hizo nadhani tunakumbuka ukuta wa BERLII: Golini Kinye,kulia Bana (R.I.P), kushoto Amasha (Mathematician), nne Chama (Jogoo), mkoba Isihaka Hasan (Chukwu),six Mkambi(Generali)we acha tu. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA.
ReplyDelete