Mkurugenzi wa masuala ya Bunge na Halmashauri wa CHADEMA, John Mrema, akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma leo mchana meitangaza safu ya viongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni walioteuliwa baada ya Kikao chao kumalizika leo.

Mrema alitamka kuwa Freeman Mbowe ndiye atakayekuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni akisaidiana na Naibu wake, Kabwe Zitto. Bwana Tundu Lissu yeye atakuwa Mnadhimu Mkuu.

Vyama vya TLP, CUF na NCCR-Mageuzi vyenye wawakilishi vimekataa kujiunga na CHADEMA na vinatarajiwa kutangaza safu yao baada ya makubaliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Now I can accept that Tanzania is a lawless country/the laws state,opposition leader in the parliament will be elected not by majority of votes but by seats,CUF are second why CHADEMA THEN?

    ReplyDelete
  2. HII KALI, UPINZANI NAKO KUNA UPINZANI.

    ReplyDelete
  3. ..mbona CHADEMA wanajigaia keki wenyewe? they think they can to it all alone bila mdaada wa vyama vingine!!!

    ReplyDelete
  4. kumbe hata chadema nao ni wabaguzi? mbona hawashirikishi vyama vingine?
    Naunga mkono cuf kwa kuunda upinzania wao na kwa mtaji huu, ccm itakuwa juu kila siku.
    Chadema acheni umimi.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa Fri Nov12, 05:13:00AM. Ingawa ni kweli Tz uvunjifu wa sheria ni mwingi kwa hili CHADEMA ndio official opposition party bungeni kwa vile wana 45 seats (majimbo 22 + viti maalum 23). CUF wana 32seats (majimbo 24 + viti maalum 8). Idadi hii inaweza kuongezeka kwa viti maalum viwili zaidi kwa kila chama CCM,CUF na CHADEMA kutegemeana na chaguzi za majimbo 7 yaliyobaki. Nimeandika kiswahili sijui utakielewa!!!!!!

    ReplyDelete
  6. anon 5:13am check again no research do not comment

    ReplyDelete
  7. ndani ya bunge wapinzani ni 53 tu 45 toka chadema 9 toka ccm wapiganaji waliobaki wote ni ccm..sasa wapi uliona tawi la ccm linaungana na upinzani??? Go chadema goooo tuko nyuma yako mpinzani pekeee

    ReplyDelete
  8. ki utaratibu wako sawa hila kumbukeni cuf wameungana na ccm kule visiwani awawezi kukubaliana hata kidogo na pia kumbukeni mrema alivyoenda dodoma kwenye mkutano mkuu wa ccm aliongea nini pia mbona bunge lililopiota walukubali ujue hawa cuf wanatatizo kweli

    ReplyDelete
  9. Chadema wamevisaliti vyama vyote vya upinzani. Tulikubaliana kuwa endapo katika jimbo la uchaguzi chama chochote kikiwa na candidate ambaye ni mwenyekiti wa chama cha upinzani kitaifa basi vyama vingine vya upinzani havitakuwa na candidates humo. Tazama walivyomgeuka Mbatia. Sisi tuliokuwa na ndoto ya kuwa wapinzani tunaweza kuungana tumepata reality check mbaya sana kutoka kwa hao wenzetu wa Chadema. Nawaomba tu viongozi wa Chadema wawe wakweli wanapo-deal na vyama vyetu 'vidogo' kama vile TLP na NCCR. Hatua hiyo ya kutudharau na kututenga (kutu-marginalize) haitawasaidia.

    ReplyDelete
  10. Anon wa 10:48:00 AM, Usisahau kuwa TLP na NCCR ina wabunge pia, japo wachache. It looks like Chadema has decided to go it alone!!!

    ReplyDelete
  11. Jamani hii Chadema iangalie isije ikawa kama Nccr-mageuzi ya kina Lamwai.imekuaje siyo Kabwe tena aliye Declare?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...