Kiwanja (Residential) chenye ukubwa wa 631 Sq. M. Kinauzwa. Kipo eneo la Mwongozo - Kigamboni, wilaya ya Temeke. Kipo karibu na bahari ya Hindi toka umbali wa takriban mile tatu. Kiwanja hiki kina hati miliki ya Serikali. Upepo mwanana toka Baharini. Eneo tambarare na barabara za mitaa zimeshatengenezwa.
Kwa maelezo zaidi piga simu no.
+44 (0) 7404531448.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mbona muuzaji yupo UK????? mi nipo bongo nilitaka kukiangalia na wewe ukiwepo, ila kigambonino mh?? ngoja kwanza ishu ya mji wa kisasa ipite. taja bei labda tutafikiria lakini kwa bei ya serikali ni (3000 per sqm x 631=1,893,000/=), sasa kwa kuwa mdau nawewe unataka faida kidogo kama 3.5m italipa nijulishe ni ku call.
    Mdau
    Chapaulaya

    ReplyDelete
  2. Kwa mdau uliye-comment hapo juu.
    Inaelekea una mtizamo mdogo sana wa kimaendeleo. Kwanza kabisa elewa haizuii chochote kwa muuzaji kuwa popote duniani katika karne tuliyonayo, kuna njia nyingi mno za kufanya bishara za kihalali duniani sasa hivi.Ili mradi mali ipo 'fixed' mahali kama ni mnunuaji basi ni kwenda kuiona. Pili, kwa mtizamo wako huo mdogo ndio maana unaamini Kigamboni, ati "Imeuzwa". Tatu na mwisho, sijuhi unakaa kijiji gani bongo kwani jaribu kutafuta eneo zuri na lenye maendeleo ya kisasa kama hilo kwa maeneo ya Dar (wilaya yeyote) kwa hiyo bei yako uliyo'quote' hapo juu, kisha kanunue. Nilidhani ungekuwa na mwamko zaidi wa kutaka kununua kwani umekwisha 'note' hapo juu kuwa Kigamboni itakuwa mji wa kisasa, hivyo endelea kuishi 'Mbagala'.

    ReplyDelete
  3. We Muingereza na wewee unaleta usanii kama vile haujakaa nje bwana. When you want to sell something you need to provide atleast the price for it! Also the pictures of the property will definately be helpful.

    ReplyDelete
  4. KIGAMBONI NI NOMA, KUNA PROJECT KUBWA SANA INAPITA KULE VIWANJA VYOTE VITACHUKULIWA NA HAO JAMAA WA PROJECT SO GUYS WATCH OUT!of course fidia mtalipwa ila ni usumbufu.

    ReplyDelete
  5. Sasa Muuza kiwanja unauza maneno tu, toa picha, bei per sqr meter, total size na namna ya kufika hapo mahali,. si halali yako bwana na wewe unauza mali yako halali - basi toa mwelekeo watu waangalie Ardhi kama kweli mali yako ndio tupige simu kukutafuta muuazaji. hivi hivi maneno matupu? - anayetaka anipigie inaenda vipi. Mbuzi kwenye gunia au? halafu unajifanya una mwelekeo awa kisasa, unakaa ulaya na technoilogia!!!!
    Give facts, let people go, see it - Advertise it properly - au unataka kuingiza watu mjini - "REMOTELY"

    ReplyDelete
  6. we mdau wa pili ndo huna AKILI hata moja, tena ya elekea wewe ndo ulietuma hilo tangazo, mdau wa kwanza yupo right, unaponunua mali kama hiyo mwenyewe lazima uwepo, sasa ukituma muwakilishi mimi taamini vipi kama siingizwi changa la macho??? je ukini kana kuwa huyo aliyepokea hela hukumtuma??? pili mnapouziana kabla hajaanza kufanya land transfer lazima awe na hati ya mauzo yenye signature zenu. we po UK sitatoa hela mpaka u sign kwanza, na wewe huta sign mpaka uone account yako imetuna. na mimi sitamuamini muwakilishi yeyote utakae mtuma. nasema hivi naushahidi wa watu zaidi ya watu washalizwa kigamboni. kiwanja kimoja kinauzwa mara tatu.
    rudi bongo uuze hutapata serious buyer

    ReplyDelete
  7. PROJECT HEWA NDIO INATAKA KUPITA. TANZNAIA INAUWEZO GANI WAKUJENGA SEHEMU KAMA ILE ZAIDI YA KUTAFUTA WAFADHILI NJE??? NA AKILI YA SISI WAFRICA PROJECT HII ICHUKUE MIAKA MINGAPI IKAMILIKE, AU UNADHANI UTAWALA YA MH. KIKWETE IANZE AMALIZIE MWINGINE??

    NA PILI MWENZENU ANAUZA KIWANJA NA SIO UZURI. AMETOA NAMBA YAKE MAKUSUDI KAMA KUNA MTU YUKO NA INTERST AWASILIANE NAYE. WATU WALIVYOKUWA NA UFAHAMU FINYU WANAKUWA SO CRITICAL. LAKINI KAMA KAWAIDA KIPOFU HAAICHI FIMBO YAKE. SIS WATZ TUMEZOEA KUWA NA TABIA HII KILA LINAPOTOKEA JAMBO AMABALO MWEZAKO ANATAKA KUFAIDIKA. KAMA MTU MNUNUZI HUWEZI KUSUBIRI BEI IANIKWE KAMA NGUO ILIOFULIWA, NA NINAAMINI HUTOTAKA MWENZAKO AKUZIDI KETE, LAZIMA UTAWAHI TU. KWAHIYO WOTE WANADEMAND KUANIKWA KWA BEI SIO WANUNUZI LABDA NI MADALALI.
    FRM. YAKE MTU HAYAMTAPISHI.

    ReplyDelete
  8. Wadau wote hapo juu;Hebu tukomae kimawazo jamani mbona tunazidi kurudi nyuma kimawazo?Ingawa si wote.Mtu katoa tangazo lake na baadhi ya maelezo muhimu na jinsi ya kumpata kama unahitaji mali.Suala la mali kuwa mbali na muuzaji siyo tatizo kwani manasheria wamekuwepo kwa kazi gani;eti wajameni?na ameshasema ana hati miliki ya serikali;mambo yamebadilika nduguzanguni hatupo tena kwenye double land allocation nchini mwetu.Haya, mtashangaa shangaa na kuandika comment za namna hiyo hapo juu wakati wenzenu wa Africa mashariki wanajinunulia na kujilimbikizia mali nchini mwenu kwa manufaa yao ya baadae, kisha mnalalamika ati "Ooh,wa-Kenya wanatunyang'anya kazi nchini mwetu", muda si mrefu mtasema wameikomba ardhi yetu na sasa hatuna pa kukaa! Ushauri wangu ni kama una pesa basi acha longolongo na Invest kwenye ardhi ya nchini kwenu. Baada ya miaka michache mno hamtoweza kuipata ardhi maeneo hayo kwa urahisi hivyo. Mdau.

    ReplyDelete
  9. Waogopa nini kutangaza bei kama kweli kinauzwa kihalali????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...