Mh. Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA)

Habari mdau, MO BLOG imefanya mahojiano na Mh. Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya Mjini pamoja na msanii nguli wa muziki wa kizazi Kipya haya ni maswali machache ambayo ningeomba uyaweke kwenye blog yako kama tiza then kwa maswali mengine wadau watasoma kwenye blog yetu.

MO BLOG: Ukiwa kama msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya, wasanii watarajie nini kutoka kwako?

MH SUGU: Bunge ni chombo cha kutunga sheria na wasanii sasa watarajie ubora wa maisha yao, yaani kama vitani watambue kwamba bataliani sasa inaingia katika Jiji na utamu wa vita ama mtu kutangazwa mshindi ni dhahiri kabisa, na kwa hali hiyo muziki tumefanya kwa nia ya kukemea madhambi kwa watu, lakini sasa tutahitaji hatua za kuchukua badala ya kukemea tu.

MO BLOG: Suala ambalo umewahi kuzungumzia kuhusu kuhujumiwa kwa wazo lako la Mradi wa Maralia Haikubaliki, utalishughulikiaje katika kipindi hiki ambacho tayari umechaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini?

MH SUGU: Suala la Maralia kwanza nataka kuweka wazi, na kuhakikisha hilo sio wazi ni kazi iliyokuwa tayari na mimi nimenyang’anywa kazi ikiwa tayari na mikataba yote ikiwa tayari, kwa haki suala hilo bado bichi na halijaisha hata kidogo, na katika suala hili nataka kusimamia usemi wa Rais Jakaya Kikwete kwamba KWENYE VITA VYA HAKI USHINDI NI LAZIMA, na kwa hali hiyo nataka kuonyesha jamii kwamba malalamiko yangu ni ukweli na sitanii hata kidogo.

Na kutokana na hali hiyo, kipimo kwamba ninaweza kufanyakazi kama Mbunge kwa mafanikio na kukidhi kiu ya wananchi walionichagua ni pamoja na kutetea haki zangu binafsi, na hili la MALARIA HAIKUBALIKI, litakuwa miongoni mwa mambo ya msingi.

Nitalifuatilia mpaka kieleweke ili jamii ijue kwamba nilikuwa na lalamikia haki na sio suala la uongo.

Kwa kina zaidi ya Mahojiano haya bonyeza link hii: http://www.mohammeddewji.com/blog/?cat=5

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mimi najishangaa sana, mana imani yangu inanambia pamoja na wingi wa wabunge wa CHADEMA bungeni, lakini sugu ataibuka kuwa wabunge machachari zaidi 2010-15 kuliko wenziwe wote.

    nakufagilia sugu, sugu mto chini aah sugu moto juu ah.

    usituangushe mzee.

    Mpenzi wako

    ReplyDelete
  2. Si yetu macho na masikio, tutaona kama ni kweli. Au ndo utaishia kulewa hicho posho za wabunge

    ReplyDelete
  3. Ni dhahiri kuwa Sugu ni mpiganaji. kwa jambo hili, nakupongeza sana. na katika hili nataka kukuhakikishia ya kuwa sisi wapigananji tuko pamoja na wewe. Ukimaliza hilo na bado kina Kibondeeez! na wao kaza buti!

    ReplyDelete
  4. Huyu sugu ana damu kali sana ya kupendwa hata angegombea dar au kuleeee nyamagana angeshinda kwa kishindo kile kileeeeeeeeeeeee, big up uko juuuuuuuuuuuuuu kama mawingu ya blue!

    ReplyDelete
  5. pamoja na yote nadhani ingekuwa vema tukitaka kumwita kwa heshima yake ya ubunge tumwite MHESHIMIWA MBILINYI na si Mh Sugu. au?

    ReplyDelete
  6. Mzee wa BusaraNovember 22, 2010

    Ila mkubwa angalia sana, sisi mwalafyale tumekutuma ukatutetee na kutuletea maendeleo kwasababu unaonekana ni mpiganaji... Hizo biashara zako nyingine baadae bado asubuhi sana....

    ReplyDelete
  7. Mdau Houston TexasNovember 22, 2010

    Usikubali wakuite pembeni na kukupa pasu kwakuwa itaminya umaarufu wako na heshima yako kwa jamii.
    Dai haki iwe haki na iwe wazi kwakuwa kwa kukukuogopa wanaweza kukuita wakakupoza ili ugomvi umalizike-USIKUBALI.
    Kama ni haki yako pigana mwana

    ReplyDelete
  8. Duh O boy's head is almost as wide as his chest! Haha...wakimbize mchakamchaka Sugu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...