Mama Mary John Mwingira

Mzee Augustine Cassian Mwingira wa Kigamboni anasikitika kutangaza kifo cha shemeji yake mpendwa Mama Mary John Mwingira kilichotokea tarehe 21/11/2010 DSM.

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Dr. Edmund Ndalama,
Kunduchi Beach (Madini) hapa hapa DSM.

Habari ziwafikie ndugu jamaa na marafiki popote pale walipo.
Bwana alitoa na bwana ametwaa,
jina la bwana lihimidiwe.
-AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. mwanamke jasiri na mfano wa kuigwa! upumzike kwa amani mpendwa wetu! pole sana upendo na ndugu wote!

    ReplyDelete
  2. Saumu Mussa poleni sana wafiwa kwa kuondokewa na kipenzi chenu mungu amlaze pema amina

    ReplyDelete
  3. Pole saaana Upendo...

    ReplyDelete
  4. Mama very influencial in Non governmental organisations. An exemplary catholic woman. Her experience in WAWATA is fubilous Rest in peace dear.

    ReplyDelete
  5. Poleni kina (John) Ngahyoma, poleni kina Mwingira, poleni watoto wa marehemu John & Mary Mwingira.

    ReplyDelete
  6. Malika Miriam MbenaNovember 22, 2010

    RIP Bibi yangu mpendwa..
    Pole sana Mwingira's, Mbena's, Ngahyoma's, Ndunguru's families..Wote tupo njia moja

    ReplyDelete
  7. HUU MSIBA NI MKUBWA SANA . HUYU MAMA ALIKUWA ANATEGEMEWA NA WENGI JAMANI , SIAMINI AMEFARIKI . MAMA MCHAPA KAZI NA JASIRI NI MFANO WA KUIGWA KWA WANAWAKE WOTE . NGO'S NA TAMWA POLENI SANA . JAMANI SERIKALI IMEMPOTEZA METEA HAKI YA WANAWAKE NA WATOTO WA MAMA MWINGIRA JAMANI POLENI SANA MMKUMBUKE UPENDO WA MAMA YENU KUSAIDIA HATA WATU ASIOWAJUA.MUNGU MBARIKI MAMA MWINGIRA JAMANI

    ReplyDelete
  8. Huyu mama alinikatia ticket kuja USA. Na alikuwa hanijui wala nini ,alikuwa na upeo mkubwa mnooooooo. Dah ,,,kweli kizuri akidumu kinaondoka . Mama mwingira ulikuwa mwema hapa duniani , ninaimani uko mbinguni na unaimba na malaika . kijiji chako na watu wote waliokuwa wanakutegemea mama umeacha majonzi sana hapa .

    ReplyDelete
  9. I am shocked to see this announcement. I worked with this strong dedicated woman when I was in Tanzania. I am really touched by her death.RIP Mary.

    ReplyDelete
  10. Poleni sana familia nzima ya Mwingira's mipango ya mungu.

    ReplyDelete
  11. Poleni wanafamilia wote kwa msiba huu mzito,tunaomba mwenyezi Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya mama mpendwa, apumzike kwa amani

    ReplyDelete
  12. MICHUZI mbona unabania comment za mama mwingira . Hata salamu za rambi rambi bwana sasa umekubali kutangaza msiba huu kwa nini . sisi hapa houston tumepost salamu zetu hapo tupo kibao na hatuoni umepost sio poa namna hiyo

    ReplyDelete
  13. Mr&Mrs Edimundi Ndalama poleni kwa kuondokewa na mpendwa mama yenu tunaomba no zenu za simu ili tuwapigie. Urusi Moscow. Rafiki zenu wa karibu

    ReplyDelete
  14. RIP Mama Mwingira. Nakumbuka ulimletea zawadi unga wa ulezi mtoto wangu wakati niko ughaibuni ulipokuja kumtembelea mtoto wako. Poleni sana wafiwa Pole sana Sabina

    ReplyDelete
  15. Kwanza nishiriki na wenzangu kutoa pole kwa wafiwa.Aidha, nijiunge na wengine kumuombea mama Mwingira pumziko la milele. Huyu mama alikuwa ni changamoto kubwa sana katika various policy debates. Mwisho, naomba yeyote anayeweza aniondoe katika ujinga huu: Hivi RIP maana yake ni nini? Huwa naona kila mara mtu anapofariki neno hilo

    ReplyDelete
  16. Mungu umemchukua mtumishi wako , ninauhakika yupo mbinguni . Mkombozi wa watu wasio na sauti. Kiongozi uliyekuwa hujilimbikizii mali jamani . Kweli mungu amechukua zawadi yake aliyotuachia jamani . Mama mwingira tutakukumbuka sana sana kwa msaada wako . Mama mwingira umefanya kazi yako duniani.

    ReplyDelete
  17. MDAU kama hujui kweli RIP ni kifupi cha REST IN PEACE.

    ReplyDelete
  18. Sikumjua mama 'Mary Mwingira' ila nimemuona kwenye youtube video akizungumza miaka mitatu iliopita katika mahojiano. R.I.P mama mpaka Yesu atakaporudi katika neema yake akufufue katika ufufuko wa kwanza na ukastarehe naye milele.

    ReplyDelete
  19. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Libarikiwe AMEN! Poleni sana kwa msiba huu wa Mpendwa MAMA!Tunamuomba Mungu ampe Mama Pumziko la Amani nanyi awajaze faraja kwani hakuna kati yetu ambaye hatapitia tendo hili ijapokuwa ni gumu lakini ndivyo ilivyo.
    Pendo Ndalama pole saana
    Mr & Mrs. Hassan Mneo (TX)

    ReplyDelete
  20. Poleni sana watoto wa marehemu: Upendo,Josephine,Sabina,Cassian,pamoja na watoto wa wadogo zako uliowalea mwenyewe tangu wadogo.Tupo pamoja kwenye msiba huu mkubwa wa mama yetu mpendwa Mary.

    Bwana ametoa, na Bwana ametwaa.Jina la bwana lihimidiwe.

    ReplyDelete
  21. Jamani poleni Upendo, Josephine, Sabina na wadogo zenu wote!! Mama apumzike kwa amani!!
    Jirani wa 1980-90s. Olympio St.

    ReplyDelete
  22. kizuri akidumu

    ReplyDelete
  23. Poleni watoto na familia nzima ya mwingira na ngayoma.

    ReplyDelete
  24. Dr.Edmund Ndalama, Upendo and family, poleni na msiba mzito. Tulimpenda sana Mama, lakini Mungu alimpenda zaidi na naimani amepumzika katika kiti cha ENZI.
    JOY wa MOI/USA.

    ReplyDelete
  25. POLE SANA UPENDO. MAMA TULIMJUA FOR 25 YEARS.

    PERAMIHO GIRLS CLASS OF 1989.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...