Mbunge wa Jimbo la Mvomero Mh. Amos Makalla akitoa pole kwa mjane aliyepoteza mume kwa mafuriko yaliyofuatia mvua kubwa iliyonyesha Novemba 11, mwaka huu Kata ya Bunduki , Tarafa ya Mgeta, Wilaya ya Mvomero, alipowatembela Ijumaa ilopita mara tu baada ya kutoka Bungeni.
Bibi Jilietha Edward akifurahia ujuo wa Mbunge wao Amos Makalla, katika Kata ya Langali , Tarafa ya Mgeta kwa ajili ya kuwapa pole kwa maafa ya mafuriko yaliyowapata

Sehemu ya makazi ya wananchi wa Kata ya Tchezema , Tarafa ya Mgeta, Wilaya ya Mvomero lilolokumbwa na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha Novemba 11, mwaka huu na kung'oa mazao, nyumba na madaraja.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero Mh. Amos Makalla (Kaunda suti) akipata maelezo kutoka kwa mzee wa Kata ya Bunduki, jinsi mafuriko yalivyosomba mazao na kuharibu madaraja na nyumba Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mvomero, Ndg. Pololet Mgema ( kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Amos Makalla wakipita juu ya daraja la chuma la waendao kwa miguu wakitoka kuwaona wananchi wa Kata ya Bunduki Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, akizungumza na wananchi wa Kata ya Tchenzdema alipoenda kuwapa pole baada ya kupatwa na mafuriko

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Mh. Amos Makalla akipita kwa tahadhari juu ya mawe baada ya daraja la mto Msefe kusombwa na maji ya mvua wakati alipowatembelea waathirika


Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla akiwa katika daraja la mto Msefe lililosombwa na maji ya mvua






Wakazi wa Kata ya Tchenzema wakimsikiliza Mbunge wao Amos Makalla ( hayupo pichani) akitoa mikakati ya serikali ya kuwasaidia waathirika , Kamati ya Maafa ya Wilaya na Mbunge ambapo ametoa sh milioni mbili kwenye mfuko wa maafa










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hongera mh. sasa changamkia fungu la kurekebisha hiyo miundo mbinu kuzuia janga kubwa zaidi la hilo maana bora kinga kuliko tiba

    ReplyDelete
  2. Uwaziri huoo unakuja mheshimiwa.....

    ReplyDelete
  3. Angeenda pia Mvomero mjini na Turiani/Mtibwa kuwashukuru wananchi kwa kumpa kura za kishindo

    ReplyDelete
  4. Brother Makalla hongera kwa kuwakumbuka wapiga kura wako. Ushauri wangu, next time unakwenda kukagua shughuli kama hiyo ACHANA na mavazi ya kwendea ofisini. Ungeweza kuvaa nguo zinazoendana na tukio. Naomba usiwe kama wanasiasa wanawekewa mkeka chini ili wapande mti Januari Mosi (siku ya kupanda mti). Picha za JK Nyerere akienda shamba alikuwa akivaa kama mtu wa shamba kweli. Japo mavazi hayana uhusiano na utendaji wa mtu lakini yana umuhimu linapokuja swala la mvuto (impression). Vinginevyo tunatarajia uwakilishi uliotukuka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...