Katika juhudi za kuendeleza michezo na undugu baina ya watu wa mataifa
mbalimbali waishio na kufanya kazi Arusha miaka kadhaa iliyopita
ilianzishwa timu moja ya michezo ya Arusha Wazee Sports Club.
mbalimbali waishio na kufanya kazi Arusha miaka kadhaa iliyopita
ilianzishwa timu moja ya michezo ya Arusha Wazee Sports Club.
Timu hiyo inayokua siku hadi siku ina wanachama zaidi ya 150 kutoka mataifa zaidi ya 20 ikiwemo Tanzania. Jumapili iliyopita wanachama wa timu hii walikutana kiwanjani kwao hapo General Tyre kufanya uchaguzi wao mkuu ambapo Danford Mpumilwa, mwanzilishi wa klabu hiyo, kwa mara nyingine tena alichaguliwa kuwa Mwenyeki ti wa Klabu hiyo ya watu wa enzi za Kifimbo. Wengine waliochaguliwa ni Makamu wake Aatsa Atogo toka Cameroon, Katibu; Ally Mamuya (Tanzania), Makamu wa Katibu; Saidou Guindo (Mali), Mtunza Fedha; Olomi (Tanzania), Naibu Mtunza Fedha; Ms Sophia Burra (Tanzania), Afisa Uhusiano; Emmanuel Ntoko (Cameroon), na Mwanasheria; Francis Kiwanga (Tanzania ).
Timu hii ambayo vilevile huendeleza vipaji vya watoto wadogo katika michezo
siku hiyo ilikaribisha timu mbili za watoto hao ambazo ni washirika wake za
Future Stars na Daraja Mbili zilizoonyesha ufundi wao. Burudani ilitolewa
na makamanda wa kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa la Oljoro ambako mkuu
wake Luteni Kanali Mmari ni mwanachama wa Wazee.
Sasa hivi Klabu ya Wazee iko mbioni kujenga nyumba ya klabu na viwanja vya
michezo hapo uwanja wa Nanenane mjini Arusha ambako itakuwa na makazi ya kudumu.

Nampongeza mpiga picha wetu.Inaonekana anajua kutunza "films za 1980s".Kwa muonekano hizi picha zinaashiria zimechukuliwa enzi za mwalimu wala sio jana.Samahani wakubwa ndo navyoziona.
ReplyDeletePicha nzuri sana zinaonyesha hali ilivyokuwa enzi hizoooo wala sio hizi
ReplyDeleteMalafyale Danford, kwanza pole sana kwa kuukosa ule ubunge .Kukubali kushindwa ni uungwana.
ReplyDeleteNakutakia kila la heri na mafanikio kwa shughuli zako hapo AR.
Nduguyo Malafyale Lawrence, POPOs Club-Bahari Beach
Danford "Lutengano". Nachoweza kusema ni "Long live Wazee Club". Eddy.
ReplyDelete