Marehemu Emanuel Ngelela

Na Francis Godwin

ALIYEKUWA afisa afya mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bw.Emanuel Ngelela amefariki dunia ghafla nyumbani akiwa nyumbani kwake maeneo ya Frelimo katika Manispaa ya Iringa.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bi.Teresia Mahongo amewaeleza waandishi wa habari leo asubuhi ofisini kwake kuhusiana na kifo cha afya afya huyo .

Amesema kuwa shughuli za mazishi ya afya afya huyo Emanuel Ngelela zinategemea kufanyika leo jioni katika eneo la Makanyagio Manispaa ya Iringa na kuwa kifo chake kimesababishwa na ugonjwa wa PB uliokuwa ukimsumbua.

Huu ni msiba wa pili kutokea ndani ya wiki moja katika Manispaa ya Iringa ambapo msiba mwingine ni ule wa aliyekuwa katibu wa Madiwani katika baraza la madiwani lililopita na diwani wa viti maalu kanda ya Ruaha marehemu Fatuma Kihombo aliyefariki juzi katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. hariri taarifa please kabla ya kupost
    RIP Emanuel

    ReplyDelete
  2. I knew you man, RIP Emma...poleni Manispaa ya Iringa kwa kupoteza mfanyakazi bora katika Idara ya Afya.
    Mbije,Andendekisye

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...