Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akiongea na waandishi wa Habari katika kikao alichokiitisha kwa ajili ya kujibu maswali ya waandishi ikiwa ni pamoja kuelezea mipango na mikakati mbalimbali yakuliimarisha Bunge. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge Ndg. Jossey Mwakasyuka Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akiongea na waandishi wa Habari kama wanavyoonekana katika picha kwenye kikao alichokiitisha kwa ajili ya kujibu maswali ya waandishi ikiwa ni pamoja kuelezea mipango na mikakati mbalimbali yakuliimarisha Bunge. Rodgers LAkiuliza swali kwa Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda kwenye mkutano na waandishi wa Habari ulioitishwa na Spika kwa ajili ya kujibu maswali ya waandishi ikiwa ni pamoja kuelezea mipango na mikakati mbalimbali yakuliimarisha Bunge. Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akisikiliza swali kutoka kwa mwandishi wa idhaa ya Kiwahili ya BBC Hassan Mhelela katika kikao alichokiitisha kwa ajili ya kujibu maswali ya waandishi ikiwa ni pamoja kuelezea mipango na mikakati mbalimbali yakuliimarisha Bunge. Picha zote na mdau Owen Mwandumbya wa Bunge
------------------------------------------

DATA ZA UCHAGUZI WA SPIKA
Kura zilizopigwa - 325
Kura zilizoharibika - 9 (2.7%)
Mabere Marandu - 53 (16.2%)
Anne Makinda - 265 (74.2%)
-----------------------------------------
ALICHOONGEA MH. MAKINDA NA WAANDISHI
SPIKA mpya wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda (61) amesema, yeye si fisadi, hakuna mtu au kikundi cha watu kilichomuweka kwenye nafasi hiyo na hakuna anayeweza kumtumia.

Makinda amesema, katika ratiba ya maisha yake alipanga kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, hivyo hayupo hapo kwa bahati mbaya.

Amesema, alitaka kuwa Spika, ni sehemu ya ratiba ya maisha yake, na kama angetumiwa asingetaka kuwa kwenye nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa Makinda, kuna watu walimshawishi agombee uspika wa Bunge mwaka 2005, ilikuwa lazima agombee wakati huu lakini kama Samuel Sitta angegombea yeye (Makinda) angejitoa.
Habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. you have not communicated, hujatwambia kasema nini!!!

    ReplyDelete
  2. Hivi kwa wazee wakubwa wazima hao, kura zinaharibikaje?

    ReplyDelete
  3. .....Ankal umewassilisha nini!?

    ReplyDelete
  4. mzee hassan nimekubali mambo yako kumbe huko bbc karubu huku mji wa kusoma tumekumiss babu
    ni mimi mzee wa house of fraser Reading branch

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...