Mwenyekiti wa Chama cha Pool Tanzania (TAPA), Isack Togocho akitoa shukrani kwa wadhamini wakuu wa mchezo wa Pool nchini,Bia ya Safari Lager kwa kufanikisha safari nzima ya timu ya taifa na kuhakikisha mchezo wetu wa Pool unaendelea kukuwa na kupata hadhi ya juu hapa nchini.katika mkutano wa na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Inter Grated,Kinondoni Morocco jijini Dar.
Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Tanzania, Amos Kafwinga akitoa maelezo mbele ya waandishi wa habari namna walivyoweza kushiriki katika mashindano ya Dunia yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini Ufaransa.
Baadhi ya wanahabari waliofika katika mkutano huo wakisikiliza kwa makini.

======= ======= ========

Chama cha mchezo wa Pool Table Tanzania (TANZANIA POOL ASSOCIATION- TAPA) kwa kushirikiana na mdhamini mkuu wa mchezo wa pool table Tanzania Bia ya Safari Lager,inayozalishwa na Tanzania Breweries Limited (TBL).

Leo imetoa rasmi taarifa na matokeo ya timu yetu ya taifa kwenye mashindano ya Dunia yaliyofanyika katika Ukumbi wa hotel ya Cheops iliyoko katika mji wa Limoges nchini Ufaransa.

Mashindano yalianza tarehe 08.11.2010 mpaka tarehe 13.11.2010 kwa kushirikisha nchi 12 badala ya nchi 32 kama ilivyokuwa matarajio ya hapo mwanzo. Sababu kubwa iliyopelekea nchi zingine kutohudhulia katika mashindano hayo ni kutokana na kukosekana kwa wadhamini wa Align Centerkuwalipia gharama za ushiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu mkuu wa chama cha pool Tanzania, Amos Kafwinga alisema; Timu yetu haikuweza kufanya vizuri baada ya kushika nafasi ya 10 kati ya nchi 12 zilizoshiriki ( nchi zilizoshiriki ni wenyeji France, N. Ireland, S. Ireland, Catalonia (Spain), S. Africa, England, Wales, Gibraltar, Scotland, Tanzania, Libya na Morocco) lakini tumeweza kupanda kiwango cha ubora wa nchi kutoka namba ya 16 mwaka 2008 mpaka namba ya 12 mwaka 2010 haya ni mafanikio makubwa yanayoonyesha wapi tunakwenda kupitia udhamini wa Bia ya Safari Lager.

Mwenyekiti wa chama cha pool Tanzania (TAPA), Isack Togocho; kwa niaba ya Chama Cha Pool Tanzania alitoa shukurani zake za dhati kwa Bia ya Safari Lager kuweza kufanikisha safari ya timu ya taifa na kuhakikisha mchezo wetu wa Pool unaendelea kukuwa na kupata hadhi ya juu hapa nchini. Pia aliwapongeza sana mkurungezi wa masoko wa TBL Ndugu, David Minja na meneja wa Bia ya Safari Lager Ndugu Fimbo Butallah na kampuni ya promotion ya Integrated Communication kwa kuweza kufanikisha safari ya timu ya taifa katika mashindano ya dunia mwaka huu.

Kwa kweli TBL kupitia BIA yake ya SAFARI LAGER wamekuwa Ni mfano mzuri katika udhamini Kwa kutekeleza ahadi Na kutoa ushirikiano mkubwa katika mchezo huu, na hivi leo mchezo wa Pool umekuwa na taswira tofauti na yenye matumaini makubwa hapa nchini na kuifanya nchi yetu ijulikane kimataifa kupitia mchezo huu wa pool table.

Leo hii kwa kupitia mchezo wa pool raisi wa dunia wa mchezo pool ametuomba tumwalike kwenye mashindano yetu ya Taifa ya pool mwaka 2011.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Tuambieni mlishika nafasi ya ngapi katika hayo mashindano? Kwa tafsiri ya haraka ni kwamba mmepanda kiwango kwa sababu wengine hawajashiriki maana mmekuwa wa 12 kati ya nchi 12 zilizoshiriki.

    ReplyDelete
  2. wamwisho, kutoka mwisho ni wakwanza, kutoka juu ni wamwisho. ukigeuza hiyo how they stand..watakuwa ni wakwanza!

    ReplyDelete
  3. Kweli wabongo ukweli unatushinda, kwanini wasiseme tulikuwa wa mwisho kati ya timu 12zilizoshiriki. Eti, kiwango kimeongzeka na ni mafanikio makubwa. Kushika umwisho????? Shame on you guys for lying to the public. Niheri msinge ongelea kabisa suala hilo. Huo nao ni ufisadi ndugu zangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...