Ankal naomba nafasi kutoa mchango katika blog ya jamii ambao naamini utawasaidia washiriki wetu wa tusker project fame kwani ni watu wengi wataliona hili kosa endapo litawekwa kwenye hii blog ya jamii.

Watanzania tunalaumiwa kwa kutopenda kutoa support katika mambo ya maendeleo ya Watanzania wenzetu lakini mara nyingine tunapata maelekezo yasiyo sahihi au watu hawahamasishwi vya kutosha.
Katika suala la Tusker project Fame nafikiri Leah ametoka si kwa sababu watu hawakutaka kumpigia kura ila kwa sababu watu wengi walishindwa kupiga kura kutokana na maelekezo yasiyo sahihi. Kuna makosa yanayosababishwa na Watangazaji wa vyombo vyetu vya habari katika kuelezea jinsi ya kuwapigia kura hasa jinsi ya kuandika ule ujumbe mfupi wa maneno.

Mtu hatakiwi kuacha nafasi baada ya kuandika neon “tusker”(mfano “tusker 3” kwa Leah) bali ile tusker inaunganishwa moja kwa moja na namba ya mshiriki bila kuacha nafasi(yaani “tusker3). Vyombo vyetu vya habari vinatangaza kwamba “andika neon tusker, uache nafasi halafu uandike namba ya mshiriki utume 15522”. HII SIYO SAHIHI! USIACHE NAFASI BAADA YA KUANDIKA NENO TUSKER. Naamini watu walishindwa kumsaidia dada yetu ambaye tunaamini kwamba angeenda mbali sana kwenye shindano hili kwani ana kipaji cha hali ya juu ukilinganisha na hausimeti wake waliobaki.

Baada ya kufuata maelekezo haya nilishindwakumpigia kura lakini nilipotuma bila kuacha nafasi nilifanikiwa kumpigia kura 4 ambazo naamini kama 10% ya Watanzania wangepiga tungemvusha.

Tuwape support vijana wenzetu kwani kwa namna nyingine wanaleta manufaa si kwa familia zao tu bali kwa Watanzania wote kama Taifa. Bila kusahau kwamba watoto wetu wanajifunza kutoka kwao jinsi ya kuzingatia malengo yao kama ambavyo hawa vijana wanafanya. Hivyo kama mmoja wao akishinda basi inakuwa kuwapa changamoto watoto wetu na hata sisi wenyewe katika kushindana kimataifa hata katika kazi, uongozi na biashara.

Ni hayo tu Ankal ila jina langu kapuni plz.
Mdau wa Taska

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Naomba nikupongeze mdau wa Tusker, kwa ufafanuzi mzuri sana ulioutoa,naamini sasa kura zitatosha kwa washiriki wengine waliobaki,
    Jana niliumia sana kwa Leah kutoka lakini ndio shindano tena. Endelea na moyo huohuo ndugu yangu.
    Mdau mwingine wa Tusker.

    ReplyDelete
  2. Mi nadhani TBC hawatangazi vya kutosha, msisitizo unatakiwa jamani kuwakumbusha watu kupiga kura, they should advetise more and more. Hongera mdau kwa maelekezo sahihi.

    ReplyDelete
  3. Hata mi namshukuru sana mdau wa tusker kwa ku comment kwenye hili.
    Yaani roho imeniuma na nimekasirika sana Leah alivyotoka, maana wale waliochaguliwa kwny probation this week, Gaga, Gobiro na Gaelle wote hawamfikii kabisa Leah ktk kipaji chake.. they arent better than Leah at ol!!!!
    Baada ya Leah kutopata kura za kutosha za kumbakiza aendelee na mashindano, ikabidi fellow contestants wa- vote na ndipo chapa lapa likamwangukia Leah... sasa pale mi naona mates walitumia akili ya KUMTOA MPINZANI WAO MKALI ambae alikuwa ana chance kubwa ya kushinda, na ndio maana wakampigia kura Leah atoke maana kipaji chake ilikuwa ni tishio kwao.
    Ol in ol, Leah unakipaji lakini it just wasnt ur liuck. am sure utatoka kivingine.

    ReplyDelete
  4. Jamaa usifikiri ni maelekezo ishu ni watu wangapi wana simu Tanzania na wanaangalia hiyo Tusker project fame mkiambiwa ni watu asiolimia 10 tu ya watanzania wana umeme sembuse Televishi waTz mnajiona wengi kumbe mpo Dar tu.At this early stage usiexpect sana kura wait mpaka pale hata nchi nyingine itakapoweza kumpigia mtu wa Watz kura sa hizi wacha wagawane

    ReplyDelete
  5. me naona steve wa kenya alifanya vibaya sana akiulizwa kwa nini alimtoa Leah atasema ni nini?? aliona wengine hawawezi kuwa wapinzani kwake kipaji wise...ila sasa subiri...naye hapati ng'o

    ReplyDelete
  6. YAANI KILA WATU WENYE AKILI WAKITOA MAELEZO KUTATOKEA JUHA MMOJA KUHARIBU KILA KITU KWA KUJIFANYA ANAJUA KULIKO WENGINE WEWE WA "Tue Nov 09, 09:28:00 AM" WENZIO WANAZUNGUMZIA UJUMBE UNATOLEWA VIBAYA WEWE UNAZUNGUMZIA HAKUNA UMEME? WATU WANGAPI WANA TV? WATU WANGAPI WANA SIMU? HIVI HUELEWI KUSOMA AU UNACHOKISOMA HUKIELEWI? SASA HUYO ALOTOA HUO UJUMBE ANA SIMU ANA UMEME NA ANA TV PIA KURA YAKE HAIKWENDA....NYAMBAFU wewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...