Wiki kadhaa zilizopita, kituo cha kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kilicho chini ya Tanzania Mitindo House(TMH), kilitimiza miaka mitatu(3) tangu kianzishwe.
Katika shamrashamra za kusheherekea miaka hiyo mitatu,BC ilipata nafasi ya kuongea na Bi.Khadija Mwanamboka,mbunifu maarufu wa mitindo nchini Tanzania ambaye pia ndio mwanzilishi wa kituo hicho ambacho kwa mujibu wa mahojiano niliyoyafanya naye miaka mitatu iliyopita,kuanzisha kituo kama hicho ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.
Ndani ya mahojiano haya,Khadija,anaongelea mambo mbalimbali hususani changamoto ambazo wamekabiliana nazo,mafanikio ambayo wameyapata tangu kuanzishwa kituo hicho na mipango yao ya baadaye.Fuatana nami katika mahojiano hayo;
BC: Bi.Khadija,kwanza kabisa nianze kwa kukupongeza wewe na watu wote wanaohusika na Tanzania Mitindo House(TMH) kwa kutimiza miaka mitatu. Je,ndani ya miaka mitatu iliyopita,mmekabiliana na changamoto zipi na unaweza kusema mpaka sasa mmepata mafanikio gani?
KM: Kwanza naomba nianze kwa kutoa shukrani,kwa niaba ya wenzangu wote tunaoshirikiana bega kwa bega katika kuendesha Tanzania Mitindo House.
Tukizungumzia mafanikio; Katika miaka mitatu iliyopita Tanzania Mitindo House imeweza kuboresha maisha ya watoto yatima ambao,kwa namna moja au nyingine, walishakata tamaa ya kuishi.Kutokana na kuwepo kwa kituo kama hiki, leo hii kila mmoja ana ndoto yake katika maisha.
Mafanikio mengine ambayo tumeyapata ni kwamba tumeweza kufikia lengo letu la kuwa na kiwanja cha kuchezea watoto yatima ili na wao wawe na uhuru wa kucheza na kufurahi kama watoto wengine walio na wazazi.
Pia tumeweza kutimiza lengo letu kuu la kusaidia jamii kwa kupitia mavazi au mitindo kwa kutangaza kazi zetu za ubunifu mikoani kama vile Dodoma ambapo tulifanya onyesho mwezi wa sita mwaka jana.Katika onyesho hilo,baadhi ya wabunge wetu walivaa mavazi yetu na kupita jukwaani kama wanamitindo. Pia tulifanikiwa kufanya onyesho la mavazi ambalo lilihudhuriwa na Rais wetu Jakaya kikwete kama mgeni rasmi kule Ngurdoto Arusha katika mkutano wa CPA. Vilevile kwa upande wa nje ya nchi, mwezi Octoba mwaka huu tulifanya maonyesho ya mavazi kule New Jersey na Washington DC nchini Marekani.
Changamoto kubwa inayotukabili ni ukosefu wa fedha ili kutimiza mipango mbalimbali tuliyonayo. Hapo ndipo tunapowaomba wahisani mbalimbali iwe ni mashirika ya umma au watu binafsi waendelee kujitokeza kutusaidia ili tutimize malengo mengi zaidi.
fuatilia mahojiano haya
KWA KUBOFYA HAPA

Mama,
ReplyDeleteHii ni kazi na wajibu mtakatifu na Mola atakulipa kwa mema yako yote!
Sisi wengine tuko pamoja na wewe na wale wote ambao watabariki juhudi zako.
Mungu atujalie sote kwa nia njema, Amina,
Wadau wa www.sokainbongo.com