Mbunge wa Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundombinu wa Serikali ya
awamu ya tatu Andrew Chenge, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela
au faini ya Sh 700,000 na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ambapo
aliwasilisha faini hiyo mara baada ya hukumu hiyo kutolewa leo
asubuhi.

Akitoa hukumu hiyo jana Hakimu Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza kesi
hiyo Kwey Rusema alisema uamuzi huo wa Mahakama unafuatia kukamilika
kwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa pande zote mbili katika kesi
hiyo iliyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi minane.

Akisoma ushahidi wa awali Rusema alisema Chenge anashitakiwa kwa
makosa manne yakiwamo kuendesha gari bila uangalifu, kusababisha vifo
vya wanawake wawili ambao ni Beatrice Costantine na Victoria Geogre,
kuendesha gari kwa uzembe na kuharibu pikipiki aina ya bajaj pamoja na
kuendesha gari lilikuwa na bima iliyokwisha muda wake.

Katika ushahidi wa awali Chenge aliukana na upande wa mashitaka ambapo
waliitwa mashahidi sita kati yao wanne walikuwa Askari Polisi akiwamo
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Fortunatus Musilimu.

Ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ulidai tarehe 26 Machi 2009 majira
ya usiku wa manane Chenge akiwa katika matembezi yake binafsi alikuwa
anaendesha gari lake aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili
T512ACE kwenye barabara ya Haille Selasie Oysterbay jijini Dar es
Salaam aligonga bajaj na kusababisha ajali iliyosababisha vifo vya
wanawake wawili.

Maelezo yaliyotolewa mahakamani hapo kuhusu kuendesha gari kwa uzembe
na kuharibu bajaj Chenge aliyakana na kwa madai kuwa alikuwa katika
mwendo wa kawaida kati ya kilo mita 30 hadi 50 na kudai kuwa dereva wa
bajaj alimfuata upande wake kwani yeye alikuwa upande wa kulia zaidi.

Hukumu hiyo ambayo ilitakiwa kusomwa Desemba 16, mwaka huu,
iliahirishwa baada ya Hakimu kukubali ombi la Wakili wa Chenge
aliyeomba kuahirishwa kwa hukumu hiyo kwa kuwa mteja wake alipata
udhuru.

Mponda alidai kuwa mshitakiwa asingeweza kufika mahakamani hapo kwa
kuwa alisafiri kwenda Mwanza kwenye msiba na kuiomba Mahakama
kuahirisha hukumu hiyo.

Kwa mara ya kwanza, Chenge alifikishwa mahakamani hapo Machi 28, 2009
akikabiliwa na mashitaka matatu likiwamo la kuendesha gari kwa uzembe
na kusababisha vifo vya wanawake wawili, kuharibu pikipiki ya matairi
matatu pamoja na kuendesha gari lisilokuwa na stika ya bima.

Katika ushahidi wake mahakamani hapo, Chenge ambaye ni Mbunge wa
Bariadi Magharibi, alidai kuwa shahidi wa tatu wa upande wa mashitaka,
Fortunatus Musilimu, ana ugomvi naye.

Chenge alidai shahidi huyo ambaye aliwahi kutoa ushahidi kuwa mabaki
ya ubongo wa marehemu yalikutwa kwenye gari la Chenge na kuwa
aliwasilisha bima batili, kuwa ni mwongo na ana ugomvi naye.

Ilidaiwa kuwa Machi 27, mwaka jana katika Barabara ya Haile Selassie
Oysterbay, Chenge akiendesha gari aina ya Toyota Hilux Pick Up lenye
namba za usajili T512 ACE, aliigonga pikipiki ya matairi matatu
(bajaj) yenye namba T736 AXC na kusababisha vifo vya Beatrice
Costantino na Vick George.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. Hii ni kesi ya Jinai na Mahakama imemtia hatiani. Je, kwa hukumu hii inamuondolea sifa ya kuwa kiongozi katika Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania?

    ReplyDelete
  2. Hukumu ZA TANZANIA ni aina mbili: KWA WATU WA KAWAIDA NA KWA VIONGOZI:Lakin Kule ZENJI naona hukumu hizo hazipo ndio maana MALIM SEIF alikaa ndani kipindi hicho,pia viongozi wa CUF walika ndani kipindi cha SALMIN

    ReplyDelete
  3. Nchi hii kwa ufisadi imezidi. Yani wana compare uhai wa watu wawili kwa sh laki saba.
    MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI

    ReplyDelete
  4. yeeeah,walimtonya? alijuaje ukabeba kabisa?ok je ingekua elfu 30 na kifungo cha mwezi 1?alikua amejiandaa? anyway tusubiri BAE sasa moja umechomoa mzee.

    ReplyDelete
  5. ni habari za kusikitisha kwamba kuendesha gari kwa uzembe mpaka kusababisha vifo vya watu wawili mwisho wake ni kulipa sh.700,000 au sh.350,000kwa kila mfu.kosa kama hilo sidhani kama linafundisha kwa wazembe wengine.hata hivyo je amefungiwa kuendesha gari kwa muda gani?nadhani natarajia ni kati ya miaka 5 na saba au kufuta kabisa leseni yake na kuanza upya.

    ReplyDelete
  6. Are you serious? Hata mlalahoi anaweza kuitoa hiyo faini na bado akabakiza chenji ya kunywa kangara.Huu ni upuuzi.

    ReplyDelete
  7. Waaaaaaii. Me nlijua lupango inamhusu. Sometimes sheria siosio.
    Ama kweli vijisent noma.

    ReplyDelete
  8. Chenge amepatikana na hatia. Kwa sheria ya sasa atafungwa miaka mitatu au faini Sh700,000/=. Kama wananchi hii adhabu ni ndogo basi bunge libadili hiyo sheria. Huo unaitwa utawala wa sheria. Sio mtu akasababisha ajali watu wamuuwe. Kuhusu Maalim Seif ana kesi ya kutoa amri ya kuzalilishwa askari wa kike kwenye mkutano wa CUF mwaka 1995.

    ReplyDelete
  9. Tujue hatua zinazofuatia kuhusu leseni yake inahifadhiwa kwa manufaa ya umma au ataendelea kutuua?

    ReplyDelete
  10. Kumbuka kwamba hiyo faini ni ya kuvunja sheria na sio fidia kwa vifo alivyosababisha. Familia za marehemu zinatakiwa kumshitaki ili awalipe fidia. Anatakiwa pia avuliwe uongozi wowote wa kiserikali aliokuwa nao kwani hafai kuwa mfano bora kwa watu.

    ReplyDelete
  11. Seriously? Kwa hiyo hao wafiwa wana haki kabisa ya kumshitaki huyu kwenye civil court ili kulipwa fidia ya kupoteza ndugu zao. Only in Tanzania mtu unaua unapewa kifungo cha miaka mitatu...

    ReplyDelete
  12. Kwa hiyo ni felony criminal huyu sasa hivi. Right? Hivyo basi anatakiwa kuachia ubunge...Na nchi nyingi hata ruhusiwa kutembelea kwa vile hawataki felony criminals kwenye nchi zao. Vijisent vyetu tutavispend wapi?

    ReplyDelete
  13. Mwanasheria Mkuu wa Serikali hana Bima...hivi Uongozi Tanzania ni Mchezo wa kuigiza? Haya tutawaona kuwa mta-last kwa muda gani na huo ujinga wenu....!!

    ReplyDelete
  14. Kusema ukweli Tanzania inaenda shimoni pole pole..kama mtu, tena public official anaua watu, na mahakama inasema yuko guilty arafu tunamwambia ondoka mzee umesamehewa... kweli hatuna maana..

    Mtu wa kawaida atafikiria nini akiona hukumu kama hii??/

    ReplyDelete
  15. Whoa...AMA KWELI BONGE TAMBARARE, UHAI WA WATU WAWILI KWA Shs 700,000(Dolla 500)...BEI RAHISI KULIKO HATA NOKIA PHONE, KWELI BONGO TAMBARARE.

    ReplyDelete
  16. This is a joke!

    ReplyDelete
  17. Maisha ya watu wawili ni sawa na laki 7.Kweli bongo kama NY aka tambarare.Huyu mtu ni muuaji kama wauaji wengine.Amepatikana na kosa la mauaji(vehicular homicide or vehicular manslaughter) anatakiwa afungwe jela hata kama ni mwaka mmoja kisha leseni yake ifungwe.Baada ya hapo hatakiwa arudi bungeni.Ni upuuzi huu.Maisha ya binadamu yazibwi na pesa ya aina yoyote ile.Unaishi mara moja,pesa inazunguka mikono.

    ReplyDelete
  18. Amakweli Mafisadi wanaimaliza Tanzania kiSiasa, Kimali na Kisheria . Yaani kuua mtu unchajiwa laki saba then unaendelea na madaraka ..... hii BiG Soo , wananchi wanabidi waandamane huyu Fisadi anatakiwa afungwe life in prison.

    ReplyDelete
  19. Huu ni ujinga na upumbavu/ueshenzi kabisa!! Hata jaji anasimama mbele ya mahakama kumsomea huyu mtu faini ya shs Lakini Saba. Naamini jaji ni wala rushwa hata kama mtanibania comment yangu lakini ukweli ndo huu. Fani ya laki saba!! Tanzania mbona imekuwa nchi ya ajabu sana!! Pumbavu sana nyie Majaji. Hata usipoweka hii comment yangu lakini majaji ni wapumbavu sana. Ilikuwa haina haja ya kuposti upuuzi kama huu watu kusoma.

    ReplyDelete
  20. Deus Malya, yule kijana aliyekuwa akiendesha gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha Mbunge wa Tarime Chacha Wangwe mwaka 2008, alitupwa jela miaka mitatu bila faini. Hapa kuna haki kweli? Bongo jela ni kwa masikini tu.

    ReplyDelete
  21. NDIO TANZANIA YETU HIYO. WEE VIGOGO WANISHI KAMA MUNGU.

    ReplyDelete
  22. mh!nasikitikia sana nchi yangu..uhai wa watu wawili plus kuendesha gari bila bima PLUS kuendesha kizembe PLUS kuharibu bajaji ya mlala hoi IS EQUAL TO TZS 700,000 yaani chini ya dola za kimarekani 600?..we need to revise our old fashioned laws

    ReplyDelete
  23. Aisee huu ni utani kabisaaaaaaaaa!!!! Mahakama zetu bongo bado hazitoi haki kwa wote, maamuzi ya kesi yanategemea na wadhifa wako katika jamii....Kwa kuthibitisha hilo, mtaona hukumu atakayopewa yule dereva aliyesababisha mauti ya waziri mama Salome Mbatia miaka kama mitatu iliyopita. Alikamatwa hivi karibuni na kesi yake itaanza kusikilizwa muda si mrefu. Ni dhahiri kwamba kifo cha Mbatia kitaonekana cha thamani zaidi kuliko cha wale wanawake wawili aliouwa Chenge.....Jamani uhai wa mtu ni uhai tu, haijalishi alikuwa waziri au kabwela!!!!!! Nasubiri kwa hamu maamuzi ya kesi.

    ReplyDelete
  24. Kweli serikali ya TZ ipo nyuma na katu haito endelea, unaua watu wawili una chajiwa laki 7 ambay haya mlala hoi anaweza ilipa, Mungu ibariki TZ na mafisadi dawa yenu ipo jikoni, mtachomwa moto

    ReplyDelete
  25. Sheria kuhusu ubunge inesemaje kama mbunge akitiwa hatiani kwa kosa la jinai?. Inatakuwa na ubunge umeisha

    ReplyDelete
  26. Hiyo picha inaeleza habari kamili. Jamaa katiwa hatiani halafu ametoka anatabasamu.

    ReplyDelete
  27. Jamani sisi wakwenda miguu tuwe makini zaidi wakati tunavuka barabara hasa hizi mashangingi zikiwa zinapita. Watatuua maana laki saba ni vijisenti kwao! Mungu tusaidie hawa mafisadi waumwe presha na kisukari!

    ReplyDelete
  28. Huu ni usanii tuuu. je ingekuwa mtu wa kawaida angepewa option ya faini ya laki saba? Laki saba itafidia vifo vya watu wawili waliokufa? Si huyu huyu chenge alisema hivyo ni vihela? si unamwona anawacheka askari wanaomsindikiza labda na hata hakimu aliyehukumu kesi hiyo?

    ReplyDelete
  29. Yaani ufisadi uko wa kila aina hapa bongo! Acha hawa viongozi, siku hizi ni kote kote! Hawa mafisadi wasubiri adhabu ya mungu na kama watepeta duniani, basi siku ya kiama wataipata! Mheshimiwa Tibaijuka eneo ya wazi nyuma ya Umoja wa Vijana ni ya nani? Je imechukuliwa kifisadi?

    ReplyDelete
  30. Deus Malya = Miaka mitatu bila faini
    Chenge = Laki saba.

    Walala hoi mtafute nchi ya kwenda, Bongo si yenu

    ReplyDelete
  31. Kwa stahili hii tutawaachia bongo wenye FWEZA ngoja tuendelee kupigwa na snow na kubeba maboksi..bongo ni mwendo wa kunja na tiketi go and return...maana unaweza ukagogwa na kigogo ukisalimika uliyegogwa ndio unafunga..

    poleni wafiwa mi bado nipo chimbo tampere Finland nakula zangu makara mabaridi na UHAI na MAISHA yangu full secured...

    Askofu New Church
    Tampere

    ReplyDelete
  32. haki iko mbinguni. haya ni yale yale ya bro ditopile, tunamuhesabia siku tu na yeye bw vijisenti.

    ReplyDelete
  33. Jamani huyu ni mtu safi. Ameshatumikia hukumu yake sasa ataendelea kua mbunge wenu. CCM hoyee. Mwacheni atumikie familia yake ebo anamajukumu

    ReplyDelete
  34. KISHERIA INAKUWAJE HAPA? MFn. DEUS MALYA JELA MIAKA 3, CHENGE SH. LAKI7??????????????????????????????????? NA WOTE WAMESABABISHA VIFO VYA BINADAMU.............EEEEHHHHHH..........AU KWA NN VISIENDEANE FAINI NA KIFUNGO?? AU KWAKUWA NI MKUBWA JAJI KAMUANGALIA MACHONI!!!!?!??

    ReplyDelete
  35. mimi sio mshabiki wa chenge wala simjui lkn hivi kweli wote waliotao maoni wanajua kuwa hii traffic case kama nyingine zote zilizowahi kutokea sasa mlitaka ahukumiwe maisha au alipe fidia kiasi gani? watanzania tuache ushabiki na tuiswe wavivu kujua hata sheria ndogo ndogo kama ajali za barabari na hukumu zake. la sivyo tutakurupuka sana na kutupa lawama bure.

    ReplyDelete
  36. Sio 350,000/= kwa kila mtu, ni 100,000/= kwa kila mtu. hizo 500,000/= ni 250,000/= kwa kuendesha gari kizembe na 250,000/= nyingine kwa kuendesha gari bila bima na 200,000/= zilizobakia ni kwa kuua watu wawili .................. mpo hapo???

    ReplyDelete
  37. Kweli Walalahoi Tutafute pa kwenda!! Bongo Hatujulikani ww Uhai wa Mtu kwa lk 7!! Hivi ni vichekesho au Vioja Mahamani!! Hawa wakubwa wakiwa majukwaani kuomba kura utadhani watu!! Lakini kumbe wanaweza kutuua alafu wasifanywe chochote. Katiba Mpya inaweza kutusaidia sisi tusiokua na kitu! Mungu pekee ndio alobaki kututetea sisi wanyonge. Mungu atawafuta wafiwa machozi yao!! NA NAAMINI ANASIKIA KILIO CHA WANYONGE!!! AMINA.

    ReplyDelete
  38. Hasira zilizonishika hapa nibora nireserve comment yangu. All I can say Mungu yupo. Poleni ndugu na jamaa wafiwa.

    ReplyDelete
  39. hakuna haki humo iliyotendeka lakisaba kosa la mauaji na wakiti wengine kesi za kuku tu faini milioni,hiyo nchi waangalie wanapoendea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...