Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Jaji Mohamed Chande Othman (pichani) kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, kuanzia tarehe 28 DIsemba, 2010.
Jaji Othman anachukua nafasi ya Jaji Augustino Ramadhani anayestaafu kwa mujibu wa sheria tarehe 27 Disemba, 2010.
Kwa sasa Jaji Othman ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa na pia ni mtaalamu binafsi juu ya hali ya Haki za Binadamu huko Kusini mwa Sudan, hadi mwezi Agosti 2011.
Jaji Othman alizaliwa tarehe 1 Januari, 1952, ana shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam na Shahada ya Uzamili (MA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Webster, Geneva-Uswisi.
Amewahi kuwa Makamu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Rwanda huko Arusha na amewahi kushika nafasi sawa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Timor Mashariki.
Jaji Othman pia, amewahi kufanya kazi ndani na nje ya nchi katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kama vile Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Msalaba Mwekundu.
Jaji Othman ataapishwa kesho tarehe 27 Disemba, 2010 katika viwanja vya Ikulu saa 4:00 asubuhi.
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Ikulu
Dar es Salaam
26 Disemba, 2010
-----------------------
Moja ya kazi alizofanya Jaji Mkuu mpya
BOFYA HAPA

Hongera Jaji Chande unastahili.ana uzoefu wa kimataifa chini ya Koffi Annan amefanya kazi nyingi za UN.
ReplyDeleteMDAU James-Reading.UK.
hongera jaji Chande,hongera pia JK kwa kuchagua mtu anayestahili kupewa hii kazi,especially wakati huu wa vuguvugu la katiba mpya,naamini kabisa uungwana wako JK kwa kushirikiana na jaji mzoefu Chande mtatupa watanzania katiba mpya yenye maslahi kwa wananchi wote bila kujali rangi,kabila,dini,ukanda wala matabaka
ReplyDeleteHongera Jaji Mohamed.
ReplyDeleteDuuh nimecheki CV yake hiki ni kifaa hatari kabisa kumbe WaTanzania wapo walivunja rekodi duniani hongera Jaji Chande.
ReplyDeletenimesikitishwa na kauli za kulalamika kwa kila kitu kwa jamaaa wa Jamii Forum kwani wao kazi yao ni kushutumu tu?
sasa ni nani kwenye Jamii Forums mwenye sifa za ujaji hakupewa na JK? JAMANI tutumie muda wetu kwenye mitandao kuandika mambo ya kusaidia nchi yetu.
Hongera Jaji Chande, way to go! kamata bango uendeleze mapambano usiijali ya wana jamii forum wanaoponda kila anaeteuliwa.
ReplyDeleteWewe unazo qualifications zote za kuwa Jaji Mkuu.
Nachompendea JK hana udini kabisa !!!
ReplyDeleteKwa upande wa udhoefu amestahili kabisa, ila sasa kwa upande wa umri ndio mashaka yanapokuja, maana umri wake ni miaka 58 inamaana miaka miwili tu ijayo atatakiwa astaafu na hiyo itakuwa ni 2012. Itabidi ateuwe mwingine tena wa kumalizia ngwe yake ya Urais.
All the best.
ALLAH AMFANYIE WEPESI MH.CHANDE.KTK HARAKATI KAMA HIZI ZA KUDAI KATIBA MPYA NADHANI YEYE NI MTU SAHIHI SANA KUTOKANA NA UZOEFU ALIONAO .
ReplyDeleteJAJI UMRI WAKE WA KUSTAAFU NI MIAKA 65 @OBSERVER
MH .MOHAMED CHANDE HONGERA SANA NA ALLAH AKUFANYIE WEPESI KTK KAZI ZAKO ZA KUSIMAMIA MAHAKAMA.CV YAKO INAKUBALIKA
ReplyDeleteHongera sana Jaji Chande
ReplyDeleteKisheria Kustaafu kwa Jaji huyu ni mpaka afike miaka 65. Hivyo bado ana mchango mkubwa sana kwa Tanzania. Hongera JK
Mdau mwenye malalamiko na Jamii Forum yapeleke huko huko Jamii Forum. Ukiyaleta hapa inakuwa ni majungu tu, huwapi nafasi ya kujirekebisha.
ReplyDeleteObserver umelonga.