Ndugu Michuzi.

Kwa niaba ya kanisa zima la Umoja,ninapenda kuwakaribisha watanzania wote na watu kutoka mataifa mbali mbali ya Afrika katika ibada ya kwanza ya mwaka wa 2011.

Ibada hii maalumu ya kuanza mwaka itaanza saa kumi na moja na nusu mpaka saa moja na nusu jioni (5:30pm-7:30pm).Katika ibada hii mchungaji Absalom Nasuwa atakuletea ujumbe maalumu wa neno la Mungu utakaokuongoza katika mwaka mzima wa 2011.

Maombi mbali mbali yatafamywa kwa kila moja wetu kama silaha ya kukulinda na hila mbali mbali za shetani. Kumbuka "Yesu Kristo ni yeye yule jana na leo na hata milele"
Kwa mawasiliano zaidi tupigie kwa namba hizi:

214 554 7381, 682 552 6402, 214 773 6697

Mahali:
Kanisa la Umoja International Outreach;
6411 LBJ FREEWAY
DALLAS TX,75240

Mungu awabariki na karibuni wote

Umoja Church.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni yeye yule yule jana kesho hata milele...ni kweli..hata wewe ni yule yule toka ulipozaliwa..na mpaka sasa..na kufa kwako na mpaka utakapofufuliwa..hutobadilika..!yesu hatobadilika..na wala hakubadilika kama imani zengine zinavyodai..ni yuleyule mpaka atakapokufa na atakapofufuliwa na mungu..!
    Ameen! ukitaka ndivyo ilivyo usipotaka ndivyo ilivyo,,.!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...