Mhifadhi wa Mambo ya Kale Gilbert Aloyce Twente (aliyekaa juu ya kiomdo) wa Wizara ya Maliasili na Utalii akitoa maelezo mafupi ya ukweli wa aliyegundua Kimondo cha Mbozi kilichopo katika Kijiji cha Ndolezi. Mhifahi huyo alitoa maelezo hayo jana katika Kijiji cha Ndolezi wilayani Mbozi kwa Maafisa Habari , Elimu na Mawasiliano wa Serikali walitembelea eneo hilo kwa ajili ya ziara ya mafunzo yajinsi ya kutambua vivutio vilivypo nchini na kusaidia kuvitangaza ndani na nje ya Tanzania kupitia maeneo yao ya kazi.
Baadhi ya Maafisa Habari , Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika Kimondo cha Mbozi chenye uzito wa tani 12 . Maafisa hao walifanya ziara hiyo jana katika Kijiji cha Ndolezi wilayni Mbozi ikiwa ni ziara ya mafunzo ya kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.Picha na Tiganya Vincent-Mbeya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kimondo ni nini? kinatokeaje?
    Tell us.

    ReplyDelete
  2. Eng.Tulinumpoki MwakalukwaDecember 24, 2010

    Ni kweli tuna vivutio vingi, si mbuga tu za wanyama.Jitihada zinahitajika kuvitambua na kuviangaza kwa bidii maana miaka ijayo pengine watu watachoka na mbuga za wanyama.
    Eng T.A.Mwakalukwa.

    ReplyDelete
  3. Ukikata kipande cha hicho kimondo nasikia ni deal sana Ulaya.

    Kuna mzungu mmoja alikata kipande mwaka 1930. Ilimchukua siku tatu kukata kajiwe kadogo tu saizi ya ngumi ya mtu mzima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...