Mbunge wa Arusha Mjini mh. Godbless Lema
akiongea na waandishi leo jijini Arusha

Na Arusha Mambo

Ofisi ya Mbunge ya Jimbo la Arusha Mjini imeanza kazi zake rasmi na kuipa ahadi ya Elimu kipaumbele ili kuhakikisha watoto kati ya mia tano hadi elfu moja wanawezeshwa kujiunga na Elimu ya Sekondari ifikapo Januari 2011.

Huu ni utekelezaji wa ahadi ya Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Godbless Lema aliyoitoa wakati wa Kampeni, kuwa atashirikiana na wananchi wa Jimbo lake kupata fedha ili kulipa ada kwa watoto hao wasiokuwa na uwezo watakaokuwa wamefauli kujiunga na elimu ya Sekondari na wale wanaoendelea na masomo katika shule za Serekali.

Mheshimiwa Lema amesema, tayari Kamati ya Maendeleo ya Jimbo (THINK TANKERS) imeundwa ili kuanza mikakati ya kuandaa matembezi ya hisani yatakayofanyika tarehe 17/12/2010 kufanikisha kupata fedha kabla ya mwezi Januari ili ada hizo ziweze kulipwa.

Amesema uteuzi wa wajumbe wa kamati hiyo aliyoiteua umezingatia jinsia, elimu, vigezo vya uwajibikaji, kuheshimika mbele ya jamii, uwezo wa uelewa na uhamasishaji, michango ya wateuzi katika kazi za kijamii, uwezo wa kufikiri na sifa zao kwa Jamii bila kujali itikadi.

Kazi ya kwanza ya kamati hiyo ni kuunda na kusimamia kamati ndogo itakayosimamia Mfuko wa Elimu wa Jimbo na kuandaa mchakato wa uwazi wa upatikanaji wa watoto na kusimamia tukio la upatikanaji wa fedha.

Hata hivyo Mheshimiwa Lema ameomba wananchi wa Jimbo lake bila kujali itikadi wajitokeze kwa wingi siku hiyo na kutoa michango yao ya hali na mali bila kujali udogo au ukubwa wa vipato walivyonavyo ili kwa pamoja waweze kuijenga Arusha Mpya.

Amesema kabla ya tarehe 13 mwezi huu atakuwa ameshaiapisha kamati hiyo na siku hiyo ndipo wananchi, waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa maendeleo watakapoelezwa mfumo wa uchangiaji, uchangiaji huo utakavyoendeshwa, jinsi ya kupata watoto wenye uhitaji pamoja na matembezi yenyewe yatakavyofanyika.

Aidha ameomba mshikamano toka kwa wananchi wa Jimbo la Arusha na wale wa jumuiya za kimataifa wanaoishi Arusha kujitokeza kuchangia maendeleo na kuleta mawazo yao yatakayoleta changamato za maendeleo katika jimbo hilo na amewasihi wananchi wa jimbo lake kuwa kuanzia sasa watu wajifunze kujali na kuwasaidia wahitaji wanaoishi nao.

Amesema vipaumbele vingingine vitakavyofanyiwa kazi haraka baada ya elimu ni miundombinu, afya ikiwemo usafi wa Jiji, watoto wanaoishi katika mazingira magumu ma upatikanaji rahisi wa huduma za kijamii.

Mheshimiwa Lema (Mb.) ameomba Makampuni, Taasisi mbalimbali zilizopo Arusha na Watanzania wote waliopo nje ya Tanzania wanaopenda kuchangia maendeleo katika Jimbo lake wajitokeze kusaidia maendeleo katika jimbo hilo ili kuweka historia ya maendeleo ya kweli kupitia Nguvu ya Umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. inabidi ukaze buti,maana dr batilda bado anazidi kujipanga na kuendeleza maendeleo,so ukilelema maa kidogo 2015 jimbo linarudi ccm,

    ReplyDelete
  2. mfano mzuri sana Mheshimiwa Lema anaonyesha kwa wabunge wengine wa chadema hasa wale ambao hata halmashauri zimechukuliwa na chadema mnahitaji kuiga mfano huu wa kuhamasisha shughuli za kielimu kimkoa

    ReplyDelete
  3. safi sana kaka!! Ukimaliza hiyo hamia kwenye barabara! tupo pamoja na tutasimama pamoja!!

    ReplyDelete
  4. Thamim, New Albany OhioDecember 07, 2010

    Waandishi wa siku hizi ovyo ovyo kabisa, mnashindwa kutuambia huyo aliyekaa pembeni kwa Mh. Lema ni nani? Au mnangoja mpaka ulimi uteleze halafu ndio mseme hatuna adabu?
    Hongera "First Lady" wa Arusha kwa kumuongoza vyema Mh. Lema.

    ReplyDelete
  5. Sasa wee wa pili hapo juu na maana gani? Ina maana vyama vingine vyote wao walale tu kazi yote muwaachie chadema? Kwanini wasihamashishe kwa nchi nzima yaani Chadema tu ndio wakaze buti wengine walale...Hovyoooooo...
    Hongera muheshimiwa.....Without education there is no real democracy

    ReplyDelete
  6. Mbunge Mteule wa Jimbo la Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema, akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) Katika Hoteli ya Kibo Palace Arusha akieleza mkakati wa kuchangia elimu kabla ya Januari mwakani ili watoto 1000 waweze kujiunga na elimu ya Sekondari katika Shule za Serekali. Pembeni yake ni Mbunge wa Viti Maalumu Chadema katika Jimbo hilo Bi. Joyce Mukya.

    ReplyDelete
  7. Hayo ndo mameno Mheshimiwa.......simply YOU MEAN BUSINESS.....siyo yule msukuma aliyetoka mwanza mpaka ikulu bila udhamini...HAPO NDIPO WASUKUMA WALIPONIACHA HOI

    ReplyDelete
  8. This is what I want to hear!! You have all my support!! Peoples Power!!!!!! Kitu muhimu kwa maendeleo ya Mtanzania sio itikadi ya chama tunahitaji wachapakazi, "Good leadership" Mwanzo mzuri sana huu.

    ReplyDelete
  9. NI JAMBO LA KUPONGEZWA KWA KWELI MHESHMIWA MBUNGE KUAMUA KUANZA NA MATEMBEZI YA HIARI ILA KUTOKANA NA UFINYU WA UHURU WA MTU BINAFSI MHESHMIWA MBUNGE WA ARUSHA UNGEWEZA KUFANYA DOOR TO DOOR KUNA WENGI PIA WANGEPENDA KUCHANGIA KWA STYLE HIYO, PIA MHESHMIWA MBUNGE UNGEEANZISHA TARATIBU MAALUM ZA KUPOKEA MAONI YA WANANCHI JINSI GANI KUONDELEZA MKOA WETU WA ARUSHA KIMIUNDO MBINU HUSUSANI BARARA ZETU ZA NDANI ZIKITENGENEZWA ZINAWEZA KUCHOCHEA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI, KUNA MBINU NYINGINE YA UNGEWEZA KUANZISHA BLOG MAALUM KUKUSANAYA MAONI MBALIMBALI JINSI GANI YA KULETA MAENDELEO MKOANI HUU MKOA NI MKOA WENYE SIFA N VIVUTIO VINGI SANA VYA UTALII MAPATO YA MKOA HUUU UNGEWEZA SANA KUFANYA ARUSHA KUWA NA STAND YA KISASA SOKO LA KISASA BARABARA NZURI HOSPITAL NZURI MAPOLISI WETU KUISHI MAHALI PAZURI MBINU ZIPO WATU WENYE UPEO WA KUELEWA MAMBO UPO, WITO KWA VIONGOZI WA VYAMA NA SERIKALI USHIND WA CHADEMA USISABABISHE KUWA NA MGAWANYIKO KATIKA SEHEMU MBALI MBALI TUUNGANE PAMOJA TUJENGE NCHI YETU MAENDELEO YA ARUSHA NI FAIDA KWA CHAMA CHOCHOTE CHA KISIASA SIO KWA CHADEMA PEKEE.

    KIPEPEO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...