Pichani ndio washindi ama vinara wa Tusker Project Fame 2010,Kulia ni David kutoka nchini Uganda ambaye ameibuka nafasi ya kwanza na Peter Msechu kutoka nchini Tanzania ameibuka nafasi ya pili.

Sisi Tanzania Msechu ndio mshindi wetu wa Tusker Project Fame 2010, kwa sababu ametutoa kimasomaso kwa kiasi kikubwa hasa ukichukulia washiriki wenzake kutoka hapa Tanzania walitolewa mapema,lakini yeye Peter Msechu kapigana kiume na hatimaye kufanya vyema na kuibuka na nafasi ya pili ambayo kimsingi si ya kubeza hata kidogo,bado ni ushindi tosha kabisa kwetu.

Karibu nyumbani Peter Msechu ukiwa kifua mbele kabisa huku watanzania wenzako tukiamini kuwa ndio mshindi wetu wa Tusker Project Fame 2010.

Shindano la Tusker Project Fame safari hii linafanyika ikiwa ni awamu ya nne,likiwa limeshilikisha nchi kadhaa ikiwemo Kenya,Uganda,Rwanda,Tanzania pamoja na Sudan ya kusini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Sikubaliani na maneno uliyosema ya kuwa kupata nafasi ya pili ni ushindi.

    Ni lazima na tuwe na mentality ya kiushindi na kutoridhika na zaidi ya nafasi ya kwanza. Daima mshindi ni mmoja na usiposhinda unatakiwa kuwa na huzuni na kuangalia ni wapi ulipokosea ili mara nyengine uepuke makosa hayo. Sikubaliani na mtindo wa kuandaa sherehe kwa washindani wetu wanaporudi nyumbani katika mashindano yeyote yale ilhali hawakuleta ushindi.

    Tabia hii inaleta ujumbe kuwa ushindi au to be the best sio muhimu nchini. Ni lazima tuwe na mentality kama ya waitaliano katika soka. THERE IS ALWAYS ONE WINNER, SECOND PLACE MEANS YOU ARE THE FIRST LOSER

    ReplyDelete
  2. Watanzania hawakumpa Kijana sapoti ya kutosha, hawakumpigia kura, i hope hata hizo alizopata nyingi ni kutoka Kenya. Michu tuache unafiki, tuwape vijana support. tupige kura. Niliboreka sana, he was good.

    ReplyDelete
  3. Hivi kwenye hili jambo inahitaji utanzania au kumpigia yule unayedhani amekuridhisha na performance yake? watanzania tuache unafiki hapa inatakiwa kuangalia ni yupi ameonyesha kipaji na pia amejiandaa sio kuangalia rangi wala utaifa.

    Pia sio watanzania hawakupenda kumpigia bali inakupasa ujue ni watanzania wangapi wenye access na mashindano haya kwa kifupi ni watanzania 10% wenye umeme je ni wangapi wana interest na wangapi wanapata muda wa kuangalia kama kweli unataka kumpigia mtu kwa kuangalia utaifa

    ReplyDelete
  4. Infact Msechu was very good, I can say was overall best. but kilichomnyima ushindi uchache wa kura

    Nakubaliana na wewe uliyesema kuwa hakupewa support kwa kumpigia kura.
    Inashangaza sana kwa WaTz!! Juzi juzi tu, tuliona mamolioni yalichangwa na WaTz sisi sisi, kwa Chama fulani cha siasa. Lakini kupiga kura ili kumpa kijana wetu ushindi imekuwa ngumu, sms inayogharimu senti kiduchu sana.
    Halafu leo bila ya aibu, ati mnasema kuwa wa pili ni ushindi tosha. Nani kasema kuwa wa pili ni kushinda? Mwenzangu amesema, tusiridhike na hali ya kupoteza, tuangalie tumeteleza wapi na kufanya masahihisho ili kupata ushindi.

    Hili ni sawa na hali inayoendelea sasa kwenye Bongo Star Search. Kwa takwimu za jana inaonyesha yule kijana wa kizungu anaongoza kwa asilimia za ushindi. Naamini kabisa anapewa support na wazungu wenzake. Kama hali ndiyo hii, siyo ajabu ataibuka bingwa, kwani kipimo cha ubingwa ni idadi ya kura unazopigiwa, hakuna kigezo kingine. Haya ndiyo yaliyotokea kwa kijana wetu Msechu.

    TUACHENI UBAHILI.

    ReplyDelete
  5. Kama ulifuatilia katika mashindano yale, kijana Msechu alikuwa anawafunika wote pale. Jana alimaliza kuaacha hoi kwa wimbo wa kusifu Juliana, ukumbi wote ulikiri kuwa Msechu ni moto wa kuotea mbali, ukilinganisha na huyo aliyepata nafasi ya kwanza. Kwa keweli tumemwangusha kijana wetu sisi wenyewe. Kijana ni hazina saaaaaaaana kwetu.

    ReplyDelete
  6. Wewe unayelalamika hapo kwamba watanzania hatukumpa sapoti ya kutosha unatumia vigezo gani? wewe umepiga kura ngapi na unajua wengine tumepiga kura ngapi? sio kulalamika tu, mimi binafsi nimepiga kura nyingi sana ambazo naamini na wengine wamempigia nyingi hivyo kumfikisha nafasi hiyo aliyopata, labda tungejua ni kura ngapi kila mshiriki alikuwa anapata ili tuongeze, otherwise huwezi jua kwamba nilizopiga zinatosha au vp. kwa ujumla nawapongeza watanzania kwa kujitahidi sana kumtetea kijana wetu msechu ingawa kura hazikutosha kumpa ushindi wa kwanza, cha muhimu ni kuwa tumejua nini cha kufanya next time, ni kupiga kura nyingi zaidi ya mwaka huu kama ulipiga ishirini next time piga arobaini! all in all mshindi lazima apatikane mmoja hata kwa kura moja ya ziada! tunashukuru Msechu kwa kupeperusha bendera ya Tanzania ipasavyo, usife moyo kwamba hujawa mshindi wa kwanza bali it's a way to more success in life

    ReplyDelete
  7. Watu wanaweza kuwa walijitahidi huku Tanzania kumpigia kura lakini na yeye alitakiwa ajitahidi kupata kura kutoka mataifa mengine kwa kuchagua wimbo ambao unajulikana na kufahamika kwenye mataifa mengine kama Rwanda na Burundi maana wao hawakuwa na mtu aliye kwenye nafasi ya fainali lakini walipiga kura pia. SASA HUYU BWANA MDOGO KWENDA KUCHAGUA KUIMBA WIMBO WA ZILIPENDWA WAKATI WA FAINALI ALIKUWA NA MAANA GANI? Jamani wimbo wakati wa fainali ni muhimu alitakiwa aimbe wimbo ambao angalau ungempatia fans vijana wa kumpigia kura sio kuimba "NAPENDA NIPATE LAU NAFASI" wa zilipendwa ambao kizazi hiki hawaujui. Kwanini asiimbe wimbo ambao ni popular east africa na vijana unawagusa? Mbona ziko nyingi tu wajameni, na nyie acheni kulaumu watu kwa uzembe wake mwenyewe! He deserved the second place!

    ReplyDelete
  8. Mimi naona msechu hata hiyo nafasi ya pili inabidi ashukuru mungu kwa maana wako waliotoka kabla walikuwa wakali kuliko yeye, mfano yule dada Rachel na Ameelina walikuwa best kuliko yeye. msechu alifikia pale kwa kupendwa na watu kwa mambo yake ya uchekeshaji lakini nafasi aliyostahili ni mshindi wa 4 baada ya davis, rachel na ameleena. mimi naona tuwe na tabia ya kusupport kile kinachofanya vizuri sio tu kwa kuwa ni mwenzetu.

    ReplyDelete
  9. MDAU HAPO ULIYESEMA MSECHU AMEJIANGUSHA KWA KUIMBA WIMBO WA ZILIPENDWA UNAKOSEA SANA, KWANI HAJAKOSA KURA KWA KUIMBA ULE WIMBO. KUMBUKA VOTING LINES ZILIFUNGWA MAPEMA KABLA YA ILE FAINALI KUANZA KURUSHWA LIVE HIVYO HATA ANGEIMBA WIMBO WA KOFI OLOMIDE AU FALLY IPUPA AU WA ALPHA HATA WA 50 CENT! HAKUKUWA NA KURA ILIYOPIGWA USIKU ULE!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...