Katibu mkuu wa CHADEMA Dkt.Wilbroad Slaa akimkaribisha katika chama Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya Bw.Sambwee Shitambala ambaye awali alijiuzuru kutokana na tuhuma zilizoelekezwa kwake, Dr.Slaa alimtaka Bw.Shitambala kufanya kazi za chama kwa ushirikiano na kwamba tuhuma zilizoelekezwa kwake zilikuwa ni na uzushi na majungu.Picha na mdau Rashidi Mkwinda


watu walisha tafuna mpunga longtime !!LOL
ReplyDeletemdau paris
Kama tuhuma zilikuwa za majungu na uzushi, kwa nini Mh Dr Slaa alimtuhumu Bw Shitambala hadharani kabla ya kumpa nafasi ya kujieleza??? Uongozi wa jazba si kitu cha busara.
ReplyDeleteMhhh, kwanza unamchafulia mtu jina lake halafu ndo unamwambia sorry. Niliposoma sheria nilijifunza kuwa "innocent until proven guilty" NA SIYO "guilty until proven innocent".
ReplyDeleteHALAFU JAMAA ANAMWANGALIA KWA HASIRAAAA HUYOOO!!
ReplyDeleteCHADEMA wameshaanza kuharibu. Sasa wana gogoro kibao. Kila siku tunasikia mapya.
ReplyDeleteMAJAZBA NAMNA HII MSIPOANGALIA, MPAKA 2015, MTAKUWA HOI. HAPO BADO RUZUKU HAJAPEWA, IKIINGIA, MAFARAKANO. ANGALIENIENI SANA, VINGINEVYO, DR. SLAA KAMWULIZE MREMA, ATAKUAMBIA KILICHOMRUDISHA VUNJO KUGOMBEA UBUNGE.
ReplyDeleteINATAKIWA BUSARA SANA SASA HIVI. WATAWACHONGANISHA MPAKA MTASAMBARATIKA. KAMA MNABISHA, SIKU MOJA MTANITAFUTA KUKUBALI MANENO YANGU.
SIMAMA JIPANGE SAWA SAWA.
"tuhuma zilizoelekezwa kwake zilikuwa ni na uzushi na majungu."
ReplyDeletewanasiasa bwana kwa mujibu wa Shitambala tuhuma zilitokea makao makuu na kumlazimisha ajiuzulu sasa inakuwa uzushi na majungu? sasa makao makuu kwanini wamchafue kisha sasa hivi wajifanye wanamsafisha?
Siasa ni mchezo mchafu sana
chadema imeanza kunukia udikteka tangu mzee nanihii akuzwe. tunaitaka chadema yetu ya kidemokrasia kama ile vision iliyokusudiwa na kina mzee edwin mtei, bob makani na mh Mbowe. martin.
ReplyDelete