

Picha na habari na
Thobias Mwanakatwa
Ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Tropical-Air Z yenye namba SH-PCN U206F imeanguka majira ya saa 6;39 katika eneo la Uyole nje kidogo na jiji la Mbeya muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege Mbeya kuelekea Dar es Salaam. Thobias Mwanakatwa
Ndege hiyo ilikodiwa na Mfuko wa Bima ya Afya kwa ajili ya kuja kumchukua Mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa ni marehemu.
Mwanafunzi huyo aliyefariki amemaliza kidato cha Nne mwaka huu katika shule hiyo ambapo alikuja kuchukuliwa kukimbizwa kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya,Suma Kibopile, alisema kufuatia ajali hiyo wamepokea majeruhi watatu ambao ni pamoja na Dakrati wa Rufaa kitengo cha Mifupa, Dk.Jons Chitemo, ambaye alikuwa akimsindikiza mwanafunzi huyo kumpeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kibopile alisema majeruhi wengine wa ajali hiyo ni Rubani wa ndege hiyo,Keyuln Fakhard raia wa Iran ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kupata mshituko baada ya kupata taarifa kuwa mwanafunzi aliyekuja kumchukua amefariki dunia na Muuguzi Frorence Stephen ambaye ametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mh. Venance Balama, ambaye alifika eneo la tukio amesema kuwa ajali hiyo imeleta historia nyingine kwani mwaka 2006 kulitokea ajali ya ndege katika uwanja huo ambapo Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Juma Akukweti alipata ajali na kufariki wakati ametoka kuangalia soko la Mwanjelwa lililoungua mwaka huo.
Balama alisema ajali ya ndege iliyotokea jana nayo imekuwa siku chache tu baada ya kuungua kwa Soko kuu la Uhindini mapema mwezi huu.
Hivi hii siyo ndege hii hii ya wairan iliyotua barabarani kule zanzibar hivi karibuni?
ReplyDeleteMabingwa wa Kiswahili, namoba mnijulishe. Hii "rufaa" inatoka wapi? Itakuwa siyo sahihi kama ni tafsiri ya "referral"; ambayo ni tendo la "referral", kama daktari anam-refer mgonjwa kwa specialist daktari au hospital. "Rifaa ni "appeal,"" kama hukuridhika na hukumu ya mahakama ya chini, kwa hiyo unataka kesi yako isikilizwe na mahakama ya rufaa.
ReplyDeleteAhsanteni
Pole sana Jaribu, hiki ni kiswahili wala sio tafsiri kama wewe unavyotaka kutuelezea.
ReplyDeletehivyo "vi mmbu" huwa rahisi sana kupeperushwa na upepo, akha mie sipandi ng"oo, nikikiona tu kwanza huwa nasikia "kizunguzungu!!!!"
ReplyDeletePoleni...
ReplyDeleteWaziri wa usafiri na usalama kulikoni wajameni? Ninauliza tena.
Pole zangu ziwafikie kwa waliofiwa na waliojeruhiwa, Mungu amlaze mahala pema popote.
ReplyDeleteMichuzi wakati umepost article ya kampuni mpya ya hizi ndege ndogo about a week ago Refer to this link
http://issamichuzi.blogspot.com/2010/12/nyalandu-azindua-bold-air-awataka.html#comments
niliandika hivi:
My hope is that all planes passes all the security and safety measures and be checked with people who qualify which is not typical in Tanzania, hence Precision and ATC. Does Tanzania have standard requirement for inspection of commercial aircraft? I am talking about people’s lives here.
If the proper inspection was not performed, I hope you’ll do the right thing Mr Ndunguru. Make sure it’s done and set an example.
If all this was conducted and approved, I would like to congratulate and wish you success on you business.
I hope Mr Ndunguru ataelewa nnachosema sasa!
Mchuma naona bado uko kwenye goodshep hapo swala ni kuinyanyua, engine inawashwa then watu wanaruka . Kitu kidogo sana hicho
ReplyDeletePoleni wafiwa lakini msianze kusema ati moto wa soko na ajali za ndege vinalink...Fuatilieni mjue nini kimeangusha ndege na nini ni chanzo cha moto na sio kuweka non-scientific hypotheses hapa.
ReplyDeletekweli tumesikitishwa na ajli hiyo. lakini tuangalie chanzo hasa ckilichosababisha mgonjwa asafirishwe kwenda Dar. ni kuwa ukanda wa Nyanda za Juu Kusini wote hauna mashine ya CT Scan. mgonjwa allitakiwa kupigwa hiyo mashine ili daktari afahamu zaidi kuhusu ugojwa wake na kuamua matibabu sahihi. hivyo akaagiza mgonjwa asafirishwe Muhimbili kwa kipimo hicho,maana hali yake ilikuwa mbaya sana. Ndipo usafiri wa ndege ukaonekana ni muafaka ili kumsaidia kijana huyu,tegemeo la baadae la Taifa.huyu si mgojwa wa kwanza kuelezwa kupewa rufaa kwenda MNH kwa ajili ya CT Scan. sifahamu bei yake halisi, ila ni aibu kwa Taifa hili kushindwa kununua mashine hiyo, huku wakikumbatia mashangingi ya watu wachache.Nchi hii!!
ReplyDelete