UPANDAJI WA MILIMA MIREFU KAMA KILIMANJARO UNASAIDIA SANA KUPUNGUZA KASI YA UGONJWA WA KANSA!

Na Baraka wa Chibiriti, Cesena, Italy
Nilikuwa nikipitia pitia magazeti kama kawaida kila siku, ndipo nilikutana na gazeti hili ambalo lina habari ya huyu Mwana Mama Martina Navratilova, mwenye miaka 54 ambae alikuwa mcheza Tenis maarufu. Na kwasasa ana ugonjwa wa Kansa, ndipo alipo shauriwa na Wataalamu apande Mlima wa Kilimanjaro....inasaidia sana kama moja ya matibabu ya ugonjwa kama alionao wa Kansa.

Mwana Mama huyu kwa muda aliishi Kenya, na kwa sasa ameamua kuhamia Tanzania na kufanya matembezi yake ya kuupanda Mlima huo wa Kilimanjaro. Alianza safari yake Tarehe 06/12/2010 pamoja na Watalii wapenda kupanda Milima mirefu, wapatao watu 28 kutoka sehemu mbalimbali za Dunia hii. Wataalamu wanasema hewa ya juu Milimani inasaidia sana katika kupunguza kasi ya gonjwa la kansa.

-Kila lakheri kwa wagonjwa wote wa Kansa, pia kwa Martina mwenyewe....upandaji mwema sana wa Mlima Kilimanjaro!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Inabidi kutofautisha kati ya kuvuta hewa ya juu ya kilima na kupanda mlima. Je Matibabu yatakuwepo ikiwa atapelekwa huko kwa helikopta na akakaa kilimani kwa muda wa masaa kadhaa? Je ni kansa zote zinatibika hivyo, au kuna aina maalumu?

    ReplyDelete
  2. What you are saying here about cancer na kupanda milima is sad. I was going to say its rubbish, but this is worse its toxic waste. Watu wenye saratani wana mzigo mzito sana na kuwapa false hopes kama hizo ni kama unawadodoshea hope,its sinful.We dont want to see people dying of cancer trying to scale the mountain with this type of false hope of cure
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  3. For those interested in medical history will remember that mountain air was considered almost therapeautic in the management of lung diseases. Swiss Alps became famous with the establishment of sonatoria for pulmonary tuberculosis We had our own up the slopes of Kilimanjaro, I dont know if it is still there in Kibongoto
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  4. Chibiriti huyo dokta wako ni dokta Manyaunyau na hilo Gazeti ulilosoma kama la kitaliana basi nadhani uliligeuza chini juu. hivi kweli inakuingia akilini kuwa kupanda mlima Kilimanjaro kunasaidia kutibu kansa?. kiufupi Martina alikuwa akiugua kansa ya ziwa na alishapona ila kwa kufanya charity ya kuchangia utafiti wa tiba ya kansa ameamua kupanda mlima Kilimanjaro lakini sio kama kwa kupanda mlima Kilimanjaro kunasaidia kupunguza kansa. angalia kesho usije kutuambia kuwa kupanda mlima Everest kunaponyesha Ukimwi.
    mdau Paka la Jikoni.

    ReplyDelete
  5. SIMBA MWENYEDecember 09, 2010

    HUU NDIYO ULIMBUKENI WA WATANZANIA KWANI AKIPATA KUISHI ULAYA TU ANAJIONA YEYE ANAAKILI SAAANA KUMBE HEWA MKIRUDI BONGO HATA KWA KULALA HAMNA SASA WEWE DAWA GANI HIYO UKPANDA TU MLIMA KILIMANJARO BASI UNAPONA NA NA INGEKUWA HIVYO KUSINGEKUWA NA CANCER MKOANI KILIMANJARO MAANA HEWA NDIYO HIYO HIYO. TUONYESHE HILO GAZETI AU KITABU ULICHOSOMA UKAYAONA HAYO ISIJE KUWA ULISOMA KATIKA UDAKU..

    ReplyDelete
  6. acha uongo soma hiyo habari uelewe vizuri..usikurupuke tu na kupotosha umma...yeye anafanya for awareness na sio kuponyesha hio ugonjwa..psychological yes lakini sio zaidi ya hapo...

    ReplyDelete
  7. A lot of people dont know how to get out of problems,here is a free recipe.
    Take bawa la kunguru,na mkia wa mjusi kafiri, na damu ya njiwa mweupe
    Tia kwenye chungu na koroga kwa mwiko
    Tia pilipili manga na hiliki
    Sing your problems to the tune of Happy Birthday to you
    That will solve all your problems
    Give me your feed back please

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...