Jumuia ya Watanzania waishio Ottawa, Canada (TAO) ikishirikiana na ubalozi wa Tanzania nchini Canada

Wameandaa sherehe ya kuadhimisha miaka 49 ya Uhuru:
Itakuwa ni siku ya Jumamosi Desemba 11, 2010
Muda: Kuanzia sa 11 jioni (17:00HRS)
Mahala: Jim Robillard Union Centre
1505 Carling Avenue, Ottawa

Sherehe hiyo pia itakuwa nafasi mwafaka ya kumkaribisha rasmi na kumtambulisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada Mhe. Alex C. Massinda. Wanachama na Watanzania wote wa Ottawa na kwingineko Canada mnakaribishwa. Waweza kuwasiliana nasi kwa namba 613 262 8677.

NYOTE MNAKARIBISHWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mkataa kwao mtumwa. Uhuru wa Tanzania au wa Tanganyika? Mbona nyie mnasoma lakini hamuelimiki. Basi tarehe 10.12.1963 ni Uhuru wa Zanzibar nao uitwe wa Tanzania? Haya na Januari 12 siku ya Mapinduzi nayo tuyaite Mapinduzi ya Tanzania? Na ile April 26 itakuwaje?

    ReplyDelete
  2. Uhuru wa Tanganyika si Tanzania!

    ReplyDelete
  3. hata hivyo lakini INA MAANA TANGANYIKA BADO INA EXIST KWA VILE NANI ANGELISHEREHEKEA UHURU WA NOTHING? NONE EXISTENCE,HAPA MI BADO NAACHWA HOI-LAKINI UHURU WA ZANZIBAR UKISHEREHEKEWA WATU WATAPIGWA BAKORA ILA KASUMBA YA MAPINDUZI NDIO ILOJAA WATU.Sasa duniani kutatangazwa nchi gani inasherehekea uhuru wa miaka 49? try to think

    ReplyDelete
  4. Mzanzibari HalisiDecember 10, 2010

    Hawa Watawala wetu wanajidai wamesoma lakini hawakuelimika,mpaka leo miaka 49 ya uhuru wao hawaujui,bado wanang,ang,ania uhuru wa Tanzania.....shame!!!!! Ebu rudini tena shule nyie wakaravindo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...